Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Uchochezi
 
Umenijumbusha kitendo cha Mwanafalsafa Socrates kutembea na taa ya chemli mchana wa jua kali mtaani. Alipoulizwa kulikoni? Kajibu, "Katika mwanga huu wote, kuna ambao wako gizani, hawaoni"! Mwisho wa kunukuu.
 
Kwani kwenye ile miaka 10 ya Kikwete uliona nini?

Uliyaona maisha bora kwa kila Mtanzania?

Kutarajia kuona mabadiliko chini ya CCM ni sawa na kusubiri embe chini ya mwarobaini.
Uko sahihi kabisa mkuu huwezi kuona mabadiliko chini ya watu wale wale.
 
sioni zaidi ya mabango ya hapa kazi tu kila mahali,sehemu nyingine wamekaa wapiga soga wanjano na kijani lakini kuna bango la hapa kazi tu
 
Umenijumbusha kitendo cha Mwanafalsafa Socrates kutembea na taa ya chemli mchana wa jua kali mtaani. Alipoulizwa kulikoni? Kajibu, "Katika mwanga huu wote, kuna ambao wako gizani, hawaoni"! Mwisho wa kunukuu.
Iii kauli ya mwanafalsafa imenitoa machozi nikama aliwaangalia watanzania du huruma sana
 
Uko sahihi kabisa mkuu huwezi kuona mabadiliko chini ya watu wale wale.
Ndio maana mkamchukuwa Lowassa kutoka CCM aje awaletee mabadiliko,nimekuhurumia baada ya kuangalia picha hii chini;
 
Attachments

  • upload_2016-9-7_8-42-48.png
    54.4 KB · Views: 34
Mabadiliko ndiyo haya uliyoyaelezea
 
Uko sahihi kabisa mkuu huwezi kuona mabadiliko chini ya watu wale wale.
Mabadiliko ni wewe mwenyewe,usiulize serikali ya awamu Hii imekufanyia nini?,jiulize umeifanyia nini serikali?,kwa kushinda unalalamika humu JF huwezi ona hata moja zuri lililofanywa na serikali.Hata kuondolewa service charge ya Tanesco,kodi za wakulima kuondolewa,watoto kulipiwa ada,madawati,kurudisha nidhamu serikalini ili pesa za maendeleo yawafikie wananchi wa chini n.k yote hayo huoni?,nyie UKAWA mmekalia kulalamika tu na kutetea mafisadi,na mnaolalamika sana ni mliozoea madili madili,huu ni wakati wa kazi.
 
Mwananchi wa kawaida amenufaika vipi hiyo mirija kubanwa? Hali ya ugumu wa maisha imepungua?
1. Wanafunzi hawakai chini.
2. Wagonjwa hawalali chini.
3. Tunaokoa 25bn kwa mwezi kutokana na wafanyakazi hewa.
4. Safari zisizo na tija zimepigwa chini kwa maslai mapana ya taifa.
5. Quality ya huduma serikalini inapanda kwa kasi ya ajabu.
6. Na mengineyo mengi sina muda wa kuyaandika kwasasa....
Anyway, ajira ya ukibaka imefutwa mpaka 2025...jifunze kuzoea
 
CCM ni laana kwa watanzania.
 
Mbona unapaniki huu mchezo hautaji hasira
Nasubiri ajira kwenye serikali ya viwanda.
 
Ndio maana mkamchukuwa Lowassa kutoka CCM aje awaletee mabadiliko,nimekuhurumia baada ya kuangalia picha hii chini;
uwe unajiongeza basi .
Mbona unaleta siasa kwenye mambo msingi ukitaka thread kuhusu Lowasa kaanzishe utajibiwa huko.
 
Mbona anaenda vizuri mimi ugimvi na mama mwenye nyumba umeisha kwa kuwa napata mshahara mapema.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…