Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mkuu wa familia kazi yake kuumbua wenzake kwa kuwasema hadharani wakati yeye mwenyewe ana yake na wala hayasemi na hata yakiandikwa au kusemwa hayatolei ufafanuzi.

Hivi sasa anakabiliwa na kashifa ya kupata kiwango fulani cha elimu kwa magumashi.Wanamasema na kumtaja mpaka kwa jina ila yuko kimya anajifanya haoni wala hasikii.


Kuna mwanae nae aliibuliwa kashifa ya kuingia masomoni kiutatautata ila hakuwa hata kujitokeza kujibu akakaa kimya jumla na wakati huo huo akadharau watoto wa wenzie kwa kuwapa majina ya ajabu ajabu tena hadharani ingawa watoto wa watu hawakuwa na kosa.

Majuzi kaibuka na lingine ambalo alipaswa kulimaliza huko huko ila akaamua kumuumbua tu mtu wa watu!

Hii yote ni kwasababu yeye anasitiriwa ila yeye hili haoni bali anaamini wanamuogopa na ndio maana hashituki lakini ingekuwa ni katika nchi za wenzetu kila kitu kingeanikwa na hata waandishi wasingesita kumuhoji.

Ukitaka uaminiwe anza kwanza na yako na ndio utaeleweka na si kujifanya wewe umsafi sana kumbe ni wale wale.

Tambua "silence means yes"

Kweli tuko kwenye Bara la giza.
 
Kila nikiitazama kauli mbiu hiii iliyobebwa kwaajili ya kuzima kelele za Vijana juu ya ukosefu wa ajira.... Sasa je hiki sio kiini macho maana hakuna makakati wowote Bali ni kupewa matumaini hewa tu....





NB UKITAKA KUMTAWALA MTU MNYIME ELIMU
UKITAKA KUMUONGOZA MTU MPE ELIMU
 
Kuna Makundi mawili yana Kinzana, Moja linadai Nchi inaenda kwa Mwendo wa Kasi saana Utawala huu wa awamu ya 5. Hili kundi linaegemea Mfano Kufufuliwa wa ATCL, Tumbua tumbua Majipu na Watumishi hewa.

Kundi la Pili linasema Nchi imesimama. Hili kundi linaegemea kuona Raia Kama hawaelewi kabisa kuwa kwanini mpaka sasa ahadi tu ndiyo zinaendelea kama kipindi cha Uchaguzi ila kuzitekeleza haijulikani itakuwa lini. Wanauliza, Nchi kupita TRA inakusanya Mapato mengi ( Kwa Mujibu wao) ila haijulikani yanaishia wapi?
Wengine wameenda mbali saana na Kusema kuwa pesa mtaani hakuna hivyo shughuli nyingi za Maendeleo zimesimama, ukimya umetawala na hamna jipya zaidi ya Matamko.

Je, wewe unasemaje, nchi inaenda vile ulivyotarajia ama sivyo?
 
Reactions: BAK
Mimi nadhani hakuna tofauti na ilivyokuwa Enzi za Mwalimu naona kila mahali pamedumaa tu
 
Nchi haiwezi kusimama hata siku moja. Inaweza kurudi nyuma.
Lakini kwa sasa inaenda mbele kwa watu waadilifu.
Kwa wezi, mafisadi, wavivu wasiotaka kufanya kazi itasimama sana na bado.
Sehemu kubwa ya mizigo iliyopungua bandarini ilikuwa hailipiwi kodi au tozo za bandari
 
Nchi inakwenda kwa ups and downs fifty fifty. In some areas and issues we need corrections. In general, tunahitaji ma analysts wa uchumi na siasa cause it needs deep understanding and research.
 
Watanzania hebu tuiombee nchi yetu na tumsaidie mkuu!
hali ni mbaya kila kona, uchumi na hali ya maisha kwa ujumla!
Afya na tiba vipo mashakani!
elimu na taaluma imekuwa havisemeki!
siasa ndio taabani!
haki na demokrasia navyo vimeporomoka!
wote tunapaswa kuelewa kuwa serikali hii ina watu wapya sana katika siasa!
tuwavumilie kuwa walikuwa over-ambitious pale mwanzoni kwa kuwa walikuwa wanataka kuishi ndoto zao, ila sasa ni wazi jahazi limewazidi, wanatamani wasaidiwe!
haya shime watanzania, nchi hii ni yetu sote na hatuna wa kumsusia, shime, shime tuungane kuimbea nchi na kumsaidia mkuu na team yake!
 
Hata bado watakuja mabundi povu linawatoka na kukauka kwa kumtetea malaika
 
Siku zote wenye busara hujali kila mtu bila kuangalia kasoro na itikadi.Together we made it.Mungu ibariki Dunia,Africa na Tanzania kwa ujumla.
 
Dah, yan huyu Rais wa CCM sijui alifikaje Ikulu ya Magogoni, sijawahi kuona kiongozi kilazer kama huyu!
 
mawazo ya kipinzani uliyonayo ndio yanayokupofusha usijue tunakoelekea...
 
1.kubomoa nyumba za watu kama vile kuna dharura
2.Kusitisha vibarua vya watu wanaotafuta maisha
3.Kutamka hakuna kuwapa chakula wenye njaa
5.Kuwaambia waliopatwa na maafa wasitegemee kusaidiwa kujengewe nyumba zao.
6.Kuwatumia vijana tena wanaonza kazi bila kuwalipa mishahara kwa miezi kadhaa
7.Kuwatimua vijana masomoni bila hata huruma
8.Kutowatembelea na kuwajulia hali wahanga wa janga kubwa la asili
9.Kuwaambia walioahidiwa kujengewa nyumba baada ya kukumbwa na maafa miaka ya nyuma kuwa mpango huo sasa haupo.

Kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!!
 
wewe na mkeo ndo mmepotea sisi bado tupo imara safari ipo salama
 
Anatupeleka kwa nchi ya asali na maziwa ....
Mungu aendelee kukubariki na akutangulie katika shughuli zako za kuwaongoza watanzania...
Na Imani na Mkulu kwa kila jambo analolifanya maana yeye ndio mkombozi wetu sisi wanyonge....
 
Nyie vijana wa lumumba ni nani aliyewaloga?! make alipozuia ile sukari ya bakhresa mlisema 'safi sana mheshimiwa' hapa juzi kati kaiachia mkasema 'safi sana mheshimiwa'. hivi mmesimamia wapi?!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…