Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Habari zenu wakuu,sina dhihaka wala utani na watawala wangu ila kuna mambo naona hayako sawa katika awamu hii ya tano nchini mwetu,mambo hayo mengi yamekubikwa na neno UKOSEFU kama ifuatavyo:
1.Ukosefu wa ajira kwa vijana ambao ni wahitimu wa kada mbalimbali kutoka vyuo vikuu nchini.
2.Ukosefu wa vitabu vya hati za kusafiria nje ya nchi.
3.Ukosefu wa chanjo kwa wajawazito na watoto wachanga.
4.ukosefu wa uhuru wa habari na vyombo vyake pamoja na ukosefu wa uhuru wa kuzungumza(Freedom of speech)
5.Ukosefu/upungufu wa mizigo bandarini ambao umegubikwa na kauli kinzani nyingi.
6.Ukosefu wa soko zuri kwa ajili ya mazao ya kilimo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma tumeshuhudia mfano wa nyanya.
7.Ukosefu/Upungufu wa maombi kwa mkuu wetu wa kaya katika nyumba za ibada.
8.Ukosefu wa pesa za wanafunzi wa elimu ya juu walokwenda kufanya mafunzo kwa vitendo(IPT)
9.Ukosefu wa hekima na busara katika awamu hii katika kuyaendea mambo ya kitaifa.
10.Ukosefu wa kuali za faraja kwa wahanga na wananchi kwa ujumla bali ni kauli za maumivu na kuligawa taifa.
Mimi nimefikiri kwa harakaharaka nimepata haya kwa mwenye nayo mengine.
NB:Tujadili kwa pamoja nini kifanyike ili haya yasiendelee nchini mwetu.?
Tanzania nchi yangu nitaipenda na kuithamini kwa moyo wangu wote.
Magufuli rais wangu nitamsifia inapobidi tu tena kwa furaha na shangwe.
 
heheheheh ukosefu bana.sijui kwann anazaliana kwa wingi nchi hii.it seems tuna mazingira conducive sana yanayompelekea akue kwa wingi
 
Tumbua Tumbua,,kuwaita unavyojisikia wastaafu, kukataa deal na vimemo,kupambana na kuwatisha wafanyabiashara , nakumbuka rafiki yangu mmoja alivyoikosa kazi yake nzuri automatically hata mimi maumivu ya kiuchumi niliyasikilizia. Utamkopa nani fasta? Uchumi unategemeana, namkumbuka Pinda kwa upole kabisa bungeni alikuwa anajibu waheshimiwa hili tunalijua na hata orodha tunayo ila tukifanya kwa haraka sana nchi itatikisika na uchumi utayumba.

Hili nadhani alilijibu hivyo baada ya kukaa na washauri, wabobezi wa uchumi, hesabu na mambo ya fedha, japo na sababu za kimasirahi zinaweza kuwepo. Vitu fake vimetamalaki kwenye bidhaa nyingi, tufanyeje? Zitto ni mwanasiasa wa masirahi lakini neno Lake la mwanzo linakuwaga na maana kubwa.

Leo hii viroba, K vant vinatumika kuliko au mtu akishakunywa bia mbili anakimbilia nyumbani kama anakimbizwa na Simba. Wafanyabiashara wasiojua principles za uchumi wanakimbizana kushikana uchawi, ni shida aisee. Katika pita pita yangu mikoa tofauti kila mtu analalamikia ugumu wa maisha sekta zote.

Mungu tusaidie hekima, busara turudi katika uchumi imara na kama kuna vitu vinawekwa sawa katika uchumi watawala watuambie maana hali ikiwa hivi hivi miezi mitatu mbele sijui itakuwaje. Na wote tuseme Amina!
 
Jiandae kupakia ndege mpya. Wanadai uchumi umeimarika sana
 
NIKWELI KABISA MADILI YENU YOTE MIAMYA IMEFUNGWA AAA. MAANA SIKU HIZI HATA MAGALI YA WALIOKUWA WAPIGA DILI YAMEOZEA KWENYE GEREJI BUBU. HAAAHAA


NIMEKUBALI MAGUFULI NI KIBOKOO CHA WAHUJUMU UCHUMI
 
TRA wanajisifu kuvuka malengo ya ukusanyaji kodi TRILIONI POINT KWA MWEZI

Bandari wanalalamika hakuna mizigo bandarini (SASA HIVI PANYA WANAPATA SEHEMU YA KULALA BILA BUGUDHA)

Kituo cha uwekezaji kimeshuka (WATU WAMEGOMA KUWEKEZA KUPITIA HICHO KITUO)

RAIS ANALALAMIKA KUWA KUNA WAHUNI WAMEFICHA FEDHA KWENYE MAKABATI YA MAJUMBA YAO.

SWALI: Hizo hela walizokusanya TRA kama kodi wamezipata wapi?
(ANA NDO TUNAONGOPEWA HADI KATIKA MAMBO YA MSINGI)
 
TRA wanajisifu kuvuka malengo ya ukusanyaji kodi TRILIONI POINT KWA MWEZI

Bandari wanalalamika hakuna mizigo bandarini (SASA HIVI PANYA WANAPATA SEHEMU YA KULALA BILA BUGUDHA)

Kituo cha uwekezaji kimeshuka (WATU WAMEGOMA KUWEKEZA KUPITIA HICHO KITUO)

RAIS ANALALAMIKA KUWA KUNA WAHUNI WAMEFICHA FEDHA KWENYE MAKABATI YA MAJUMBA YAO.

SWALI: Hizo hela walizokusanya TRA kama kodi wamezipata wapi?
(ANA NDO TUNAONGOPEWA HADI KATIKA MAMBO YA MSINGI)

Zakuambiwa changanya na zakwako.
 
Eti shilingi imepanda thamani, hapo ndiyo utajua sisi ni watu wa aina gani
 
Sala ni maunganisho ya binadamu na Mungu wake kiroho. Ni tukio kubwa na la heshima kwa mwanadamu ambalo halitaki UNAFIKI, UTANI au KUJARIBU.
Mzee wangu Yohana kila siku amekuwa anasema anaomba mie na wananchi wenzangu tumuombee sawa, lakini ili kuombewa ni lazima mtu aonekane kweli anastahili kuombewa kwa kitenda haki.
Juzi vijana wa Yohana kule udongo ulipotingishika wakafanya kitendo cha ajabu, kaja Bw Eddo kuwasalimia na kuwasaidia ndugu zake basi walipojikusanya kwa upole mkuu kumpokea wakapigwa mabomu na virungu na mzee Yohana hajakemea vijana wake.
Juzi vijana hao hao wakamwona Pro-pesa Harun ana barua ambayo hajaandikiwa yeye anakusanya vijana na kuandamana naye nao wakafunga tela kumsindikiza mpaka jengo alilokusudia.
Wakakaa kwenye ma defender yao lango kuu likivunjwa, walinzi wakipigwa na kunyang'anywa bunduki kisha milango ya ofisi ikivunjwa.
Hakuna walilofanya ila ni kuripoti kwenye redio zao labda kwa wakubwa wao au kwako kabisa Mzee Yohana.
Huyu kwa sababu unampenda vijana wako hawakuingilia kati aliyofanya.
Mpaka hapo kweli unaona ninayo sababu ya kupiga goti nakukuombea? Utakuwa hunitakii mema maana Muumba atajua tuu kuwa nafanya unafiki na adhabu ya unafiki naijua na siitaki.
Jirekebishe mzee Yohana NIKUOMBEE la sivyo hutaki JIOMBEE mwenyewe.
Kwa vile unanguvu nyingi kama John Cena waweza kuchukia na kusema kamata huyo anawachochea watu wasiniombee, basi nitajifanya nakuombea baraka kumbe nakuombea Mungu akupe Ukoma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom