Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
usiposhirikiana vizuri na watumishi na wafanyabiashara, na kutothamini umuhimu wao..

matokeo yake ni yale ya sukari, vila.za vinavyokuja vya elimu bure, wakurugenzi 13 kukacha kuapishwa, makameu kutaka kujiuzulu kwa kukosa ushirikiano mzuri, n.k.

eti unataka kujenga mapenzi na mtu aliejichokea nyumbani anaecheza bao na kunusa ugoro,ambaye pia analishwa na mtumishi au mfanyabiashara..
tusubiri matokeo....
 
Tangu aingie madarakani amekuwa si wa kuleta matumaini zaidi ya vitisho. Kauli zake zinaonyesha Kama ni mtu anauefurahia mateso ya wengine. Mfano kutaka watu,waishi Kama shetani badala ya kuishi Kama malaika, kisimamisha watu kazi bila kufuata taratibu, kuwambia waathirika Wa mvua ya mawe wasitegemee masaada walioahidiwa, kuwaambia waathirika Wa tetemeko wajiju na mengine mengi.
Naona kuna tatizo ambalo wangi wanaliona Ila kwa sababu za kisiasa wanalinyamazia. Tuyaathirika sote tusipopaza sauti zetu kwa pamoja
 
Tangu aingie madarakani amekuwa si wa kuleta matumaini zaidi ya vitisho. Kauli zake zinaonyesha Kama ni mtu anauefurahia mateso ya wengine. Mfano kutaka watu,waishi Kama shetani badala ya kuishi Kama malaika, kisimamisha watu kazi bila kufuata taratibu, kuwamnia waathirika Wa mvua ya mawe wasitegemee masaada walioahidiwa, kuwaambia waathirika Wa tetemeko wajiju na mengine mengi.
Naona kuna tatizo ambalo wangi wanaliona Ila kwa sababu za kisiasa wanalinyamazia. Tuyaathirika sote tusipopaza sauti zetu kwa pamoja

Watanzania tumepigwa na bumbuwazi, we are in a great shock, wengi hatuamini kinachoendelea maana hatujawahi kuexperience hali kama hii, si viongozi waandamizi wala wananchi wa kawaida, itachukua muda mrefu sana watu kupaza sauti, na wakati huo ukifika sitaki kuimagine itakuwaje! God save our mother Tanzania
 
Mpaka saaa hivi tumeshapigwa 3-0, hana habari kama nchi hii ina watumishi wa umma!! Cheeeeeeehhh!!
 
Tunaisoma namba na hao ccm wanai soma namba, lol mbavu zangu, nilijua tuu kuwa wote tutasomeshwa number!
 
Kale kawimbo ka mtaisoma namba kalitubagua wakati ule wa kampeni tu lakini sasa hakabagui haka kawimbo mpaka CCM wenyewe wanaisoma namba kibaya zaidi Pleti namba yenyewe ilikuwa mpya ila imechoka katika kipindi kifupi sana na cha ajabu zaidi barabara yenyewe ni ya vumbi alafu mkuu wa kaya yuko mbele sisi nyuma hatuoni hizo namba kwa kweli acheni tu.Rais huyu haeleweki tunaweza tukaambiwa zile pesa za wahanga wa tetemeko walipwe vijana wa elimu ya juu ambao wanafanya mafunzo kwa vitendo au ikaelekezwa katika shughuli zingiune za msingi zaidi.
Tanzania nchi yangu nitaipenda na kuithamini kwa moyo wangu wote.
Magufuli rais wangu nitamsifia inapobidi tu tena kwa shangwe na furaha.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Kichwa cha habari hakiendani na mada, labda kama sielewi maana ya neno "sadist" kwa kuwa ni neno la kiingereza. Neno sadist maana yake ni mtu anyefurahia matatizo, mateso, maumivu, masikitiko ya watu wengine. Mambo mengi uliyoyaelezea ni kweli lakini yanawekusababishwa mtazamo, dhana na namna tofauti ya kutekeleza mambo. Na hayaonyeshi kuwa yametendewa kwa makusudi ya kuwaumiza Watanzania. Kwa kuwa umetoa tuhuma nzito, unawajibika au kufuta kichwa cha mada yako au utoe ushahidi wa tuhuma hii nzito.

Nayasema haya kwa kuwa mimi ni mtu huru na ningependa nitoe hukumu ya haki kwa kila mtu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom