Ni lazima abomoe kwanza ili ajenge vizuri. Nyufa zilikuwa kubwa mno. Linchi lilikuwa linajiendea endea tu. Mavyeti feki kibao! wafanyakazi hewa kibao! wanafunzi hewa kibao! ufisadi kibao kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata haja ya mtu kustrugle, maana kufanikiwa kwa mtu kulitokana na madili na kufahamiana tu. Si elimu wala strugle ya mtu. Nchi ilikuwa imeharibika sana na ilikuwa ikikatisha tamaa watu ambao kweli wanastrugle kufanikiwa. Mtapiga mayowe sana lakini MAGUFULI anainyoosha nchi na kurudisha utaratibu. Sasa tutaheshimiana tu. Asante Baba Magufuli Mungu azidi kukutia nguvu uirejeshe heshima ya kufanya kazi kwa bidii na watu kufanikiwa kwa bidii ya kweli na si kwa madili.