Nafikiri Mhe Rais ni kiongozi mzuri,ila kama ilivyo kawaida ana mapungufu,pengine mengi tu. Kwa mtazamo wangu anaweza kutupa mafanikio na akawa Rais wa mfano endapo atafanyia kazi haya yafutayo:-
(i) Asiwaamini sana ccm; katika teuzi zilizopita inaonekana kuwa mwana ccm ni kigezo muhimu kwa mtu kuteuliwa. Tumeshuhudia maafisa wa ccm wameteuliwa kushika nafasi mbalimbali za kiutendaji serikailini huku wengi wao wakiwa hawana uwezo na kwa vyovyote watatangiliza maslahi ya ccm mbele.
(ii) Asiwaamini sana wazee; wazee wana umuhimu wao lakini Mhe Rais anatakiwa kuwaamini zaidi vijana na awape nafsi waongoze mashirika ya serikali. Mpaka sasa vijana ndio wanafanya kazi nyingi tatizo hawana fursa ya kutoa maamuzi na wakati mwingine ushauri wao unapuuzwa na wazee. Kama kwa mfano VODA, TIGO, AIRTTEL yangekuwa yanaongozwa na wazee sidhani kama wangepata mafanikio waliyonayo
(iii) Mhe Rais awatumie watanzania wanaoishi nje ya nchi; kutokana na exposure waliyonayo na uzoefu katika nyanja mbalimbali wanatakiwa kushawishiwa waje kulisaidia Taifa lao hasa katika maeneo yenye ulazima wa kufanya hivyo
(iv) Mhe Rais awamini watumishi na asiwakatishe tamaa. Kuna dhana potofu ambayo ni kama inajengeka kuwa watumishi ndio wanakwamisha mambo yote jambo ambalo sio kweli. Isije ikawa kama mwanafunzi aliyepewa mtihani wenye maswali matano lakini huyo mwnafunzi akang'ang'ania kufanya swali moja tu mpaka muda unaisha na matokeo yake ni kufeli. Lazima kuafanyike combination of strategies na siyo fukuza fukuza tu
(v) Mhe Rais awaajili na awasikilize wataalam wa masuala ya uchumi na maendeleo. Asiwategemee mawazili na maafisa wa serikali maana wakati mwingine huwa wanatoa ushauri wa woga ama wanafanya mambo kwa mazoea
(vi) Mhe Rais ahakikishe watanzania wanaungana, kusiwe na misuguano ya kisiasa ambayo siyo ya lazima. Yeye kama kiongozi wetu asubili 2020 ndipo akisemee chama chake.
Kwa ujumla JPM ana nia njema japo kuwa na nia njema peke yake haitoshi, la muhimu tumuunge mkono katika yale mazuri aliyoanza nayo.