Taifa lilizizima ndani ya CCM kwenye chaguzi za kumpata mgombea uraisi kwa tiketi hiyo, magazeti nayo yalitia chumvi kila kona jina lilikuwa Edward Lowassa na baadhi ya majina yalisikika ya wataka uraisi kupitia CCM.
Vita ikahamia Dodoma baadaye jina la Lowasa 'kukatwa' kwa msemo wao wa ccm wajumbe wakagawanyika wengine wakiunga mkono na walio wengi kubakia kuunga mkono jina hewa la mgombea Lowassa kutokuwepo wakapiga na pambio, ' tunaimani na Lowassa' mbele ya mwenyekiti wa ccm hali hii ikaonekana kama fedhea kwa mwenyekiti huyo.
Baada ya hapo jina la Dr John Joseph Pombe Magufuli likachomoza kwa bahati, naye Lowassa kujiengua na kujiunga na CDM na kupeperusha bendera ya ukawa.
Kampeni zikaanza zikishadidiwa na wasanii kila kona ya nchi ilisikika, "Hapa kazi tu' kwa CCM na, "Lowassa' mabadiliko, mabadiliko Lowasa" na nyimbo za kila aina mara ' ccm mbele kwa mbele.........' Lowassa huyo na Tanzania mpya'
Baadaye tukashudia PUSHUP majukwaani wakati wengine wanazungusha mikono wananchi wakapenda PUSHUP ndiyo kila mtu akaitumia watoto wa shule wakigoma wanapiga PUSHUP, nk .
Kwa sasa inanisikitisha sana kuona watanzania wanalalamika kuwa hakuna Uhuru wa vyombo vya habari, Uhuru wa kushiriki mikutano ya kisiasa, makongamano, sheria za nchi zinakiukwa, na bunge kupokwa haki na wajibu wake na kuongozwa kibabe nk watanzania mmesahau nini maana ya PUSHUP na pia tulikuwa tunasema taifa lilipofika haliitaji siasa linahitaji kiongozi mwenye Dira, maono, mkali, asiyeyumbishwa, mwenye maneno machache yanayofuatiwa na vitendo, mwenye nidhamu, maadili na uzalendo wa nchi na wananchi wake. Yako wapi maneno yetu hayo?
Uko wapi ushiriki wetu wa PUSHUP? Uko wapi wimbo wetu wa "CCM mbele kwa mbele.......... mwaka huu wataisoma, ccm ni ile ile........" kauli mbiu yetu ya "HAPA KAZI TU" & MAGUFULI FOR CHANGE (M4C) Je hatukujua kwamba kura zetu ni kifungo cha miaka mitano?
Kwa hiyo tu yanayotokea sasa ni matokeo ya juhudi zetu hapo juu na hivyo tuunge mkono kazi tuliyoianzisha tusimwachie Magufuli peke yake kwani mwanzo tulikuwa naye na tuendelee naye SAFARI YA KUBAHATISHA BAADAYE NI MAJIGAMBO.