Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Rais ana nia nzuri ya kuipeleka nchi kwenye neema ila tatizo lake kawa kama aliyepotea njia baharini. Rada, Kompasi na GPS katika meli vyote vimezima havifanyi kazi na kwa majisifu yake ambaye ndiye nahodha kwamba anajua kila kitu hataki hata kuwauliza wavuvi wa madau kaskazini ni ipi.

Ameamua kukivurumisha chombo kiende kinakokwenda mpaka atakapoifikia nchi kavu kokote. Ndio Magufuli na Tanzania.
 
Tunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu na Elimu bora .
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .
Nilifikiri matumizi sahihi ya kodi yanajadiliwa bungeni katika hali ya uwazi na shirikishi kwa wananchi wote.
 
Watanzania tuna akili fupi sana ndo maana hatusonge mbele kama taifa na mtu mmoja mmoja, maada ni nzuri inawweza kutusaidia kuibua njia mpya za kumsaidia rais kama ushauri, mtoa mada hana nia mbaya na rais bali anajaribu kutushirikisha tuangalie mwelekeo wa sisi kama taifa, kwa hiyo tuache kumkebehi tuchangie mada kwa mtazamo chanya kwa kutoa michango na ushauri wa kujenga taifa.
Ushauri chanya kwa rais
1.Akuze demokrasia
2.Aongeze ushiriki wa wananchi katika masuala ya bunge kwa kurudisha bunge live
3.Awe msikivu kwa sauti ya wananchi
4.Awajengee watanzania desturi ya kuvumiliana licha ya tofauti za kiitikadi.
 
mkuu mbn unazidi kutuchanganya.......nia nzuri bt huna hakika kama anajua anakoelekea
Amebadili gia angani kama comrade Mboowe. Teh teh. Jana Lowassa alikuwa kubwa lao, leo he's the most decorated politician.
 
A nation or civilization that continues to produce soft-minded men purchases its own spiritual death on the installment plan. - Martin Luther King Jr.
 
Taifa lilizizima ndani ya CCM kwenye chaguzi za kumpata mgombea uraisi kwa tiketi hiyo, magazeti nayo yalitia chumvi kila kona jina lilikuwa Edward Lowassa na baadhi ya majina yalisikika ya wataka uraisi kupitia CCM.

Vita ikahamia Dodoma baadaye jina la Lowasa 'kukatwa' kwa msemo wao wa ccm wajumbe wakagawanyika wengine wakiunga mkono na walio wengi kubakia kuunga mkono jina hewa la mgombea Lowassa kutokuwepo wakapiga na pambio, ' tunaimani na Lowassa' mbele ya mwenyekiti wa ccm hali hii ikaonekana kama fedhea kwa mwenyekiti huyo.

Baada ya hapo jina la Dr John Joseph Pombe Magufuli likachomoza kwa bahati, naye Lowassa kujiengua na kujiunga na CDM na kupeperusha bendera ya ukawa.

Kampeni zikaanza zikishadidiwa na wasanii kila kona ya nchi ilisikika, "Hapa kazi tu' kwa CCM na, "Lowassa' mabadiliko, mabadiliko Lowasa" na nyimbo za kila aina mara ' ccm mbele kwa mbele.........' Lowassa huyo na Tanzania mpya'

Baadaye tukashudia PUSHUP majukwaani wakati wengine wanazungusha mikono wananchi wakapenda PUSHUP ndiyo kila mtu akaitumia watoto wa shule wakigoma wanapiga PUSHUP, nk .

Kwa sasa inanisikitisha sana kuona watanzania wanalalamika kuwa hakuna Uhuru wa vyombo vya habari, Uhuru wa kushiriki mikutano ya kisiasa, makongamano, sheria za nchi zinakiukwa, na bunge kupokwa haki na wajibu wake na kuongozwa kibabe nk watanzania mmesahau nini maana ya PUSHUP na pia tulikuwa tunasema taifa lilipofika haliitaji siasa linahitaji kiongozi mwenye Dira, maono, mkali, asiyeyumbishwa, mwenye maneno machache yanayofuatiwa na vitendo, mwenye nidhamu, maadili na uzalendo wa nchi na wananchi wake. Yako wapi maneno yetu hayo?

Uko wapi ushiriki wetu wa PUSHUP? Uko wapi wimbo wetu wa "CCM mbele kwa mbele.......... mwaka huu wataisoma, ccm ni ile ile........" kauli mbiu yetu ya "HAPA KAZI TU" & MAGUFULI FOR CHANGE (M4C) Je hatukujua kwamba kura zetu ni kifungo cha miaka mitano?

Kwa hiyo tu yanayotokea sasa ni matokeo ya juhudi zetu hapo juu na hivyo tuunge mkono kazi tuliyoianzisha tusimwachie Magufuli peke yake kwani mwanzo tulikuwa naye na tuendelee naye SAFARI YA KUBAHATISHA BAADAYE NI MAJIGAMBO.
 
ccm ni ile ile, ndio maana hata magufuli anasema ' serikali ya magufuli badala ya ccm! hata yeye anaiogopa kwani haiaminiki!
 
Huku kijijini kwetu tushakata tamaa na Magufuli kabisa kiongozi. Hali imekua ngumu kuliko enzi za Jk. Polisi wako juu ya mahakama zetu za mwanzo na wilaya. Kila kitu ni mabavu!!

Kwasasa tunasali usiku na mchana hii miaka minne iishe huyu mtu aondoke, bora CCM mtuletee hata Membe anaeijua diplomasia na utawala bora.
 
Ana nia nzuri sana, ILA TUPO DSM TUNATAKA KWENDA ARUSHA, safari yetu tunaanzia dsm-moro-dom- singida- manyara then AR! swafiii! kufika ni kufika tu! ILA Democrasia inaenda 'Kabrini'.
 
Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
Kweli wewe huna ufahamu! Nchi inaendeshwa kama raisi anavyoona inafaa? Hii kali jamani! elimu yako p,se?
 
Bora kifungo kuliko lowasa ndio angetuuza na kutufanya watumwa
 
hahaaaaaaaaaaa siajawahi ona awamu kama hii inavunja katiba na sheria anzia wa chini hadi juu full taabu
 
Magufuli hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi.hajui katiba,hafuati sheria...za nchi.
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
tatizo alilo nalo ni moja anatamani kesho reli ya kati iwe imekamilika, kesho kutwa awe amenunua ndege tatu, mtondogoo awe amenunua mabehewa ya train na vichwa vya kutosha kitojo anataka barabara za juu Nchi nzima yaani ndani ya mwaka awe amewafunga mafisadi wote! kumbe mambo yote haya yanahitaji mipango na subira! tatizo siyo nia njema ni resources huwa hazitoshi. anahitaji kujipanga vizuri sana. kitu cha kwanza angeimarisha reli ya kati na TAZARA ili viwanda atakavyo jenga(?) wasafirishe bidhaa zao kwa njia rahisi kuwapunguzia gharama za uendeshaji. lakini pili, aainishe viwanda gani wanakusudia kuvijenga na kwanini ili serikali na sekta binafsi wawe na common focus.Viwanda endelevu vinajengwa na watu binafsi siyo serikali.
 
Ndiyo hali halisi miongoni mwa Watanzania kwa sasa, maisha yao yamejaa hofu hofu na masahaka, wengi wanaelekea kupoteza tumaini walilokuwa nalo kuhusu Nchi yao. Ukosefu wa bidhaa muhimu na kupungua kwa mzunguko wa fedha kunazidisha hofu hiyo.

Kwa maafisa wa Serikali hofu ni zaidi, hawawezi kushauri tena wamebaki kusubiri la kutokea, hofu imewajaa hawajui kesho yao. Concentration hair tena, ubunifu haupo tena, ni kamata kamata hakuna kukosoa malaika. Taasisi zimekufa, mifumo imezikwa rasmi.

Taifa la hofu , mwisho wake ni majuto.
 
Mimi mwenyewe nina hofu natamani tungefanya amendment ya kwenye katiba kipengele cha uhuru wa kutoa maoni kifutwe.Kwa sababu maoni yetu wakati mwengine yanatafsiriwa ni uchochezi au matusi pale unapotumia neno ambalo hata bungeni linatumika.

Kwa sasa hivi mtu akitoa thread ya kumkosoa malaika wa nchi sitochangia wadau milioni saba ya kulipa faini sina na kifungo cha miezi sita naogopa sana.


AFRICA IS NOT POOR BUT SHE IS POOR CONTROLLED.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom