kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Kipindi cha kampeni alipokuwa anasafiri kwa gari sisi tulisema anaogopa kupanda helkopta,lakini ile ni dalili kuwa ni mbishi na anapoamua lake hasikilizi mtu,ikafikia akapiga push up jukwaani tukasema aah rais wa push up ile ilionyesha kuwa yupo tayari kwa lolote na haogopi kelele zenu na atapambana peke yake,akamalizia na gwanda za jeshi,tukaulizana uhalali yeye kuvaa zile gwanda,ile ni ishara kuwa serikali yake itaendeshwa kijeshi na atakaeleta mchezo atashughulikiwa,mwisho akakutana na majaji hapo sasa ndio watu watafungwa sana dalili zimeshaonyesha kuwa maandamano na mikutano imepigwa marufuku,mpaka sasa upande wetu umeonekana kuchoka mapema bila kuwa na hoja za maana,mfano mtu tuliemtegemea kwa hoja anakuja na hoja ya raisi alikwenda rwanda kujifunza kudhibiti upinzani,lazima tukae chini tutafute mbinu mpya tusisubiri kama zitto alipoomba ccm mdhibiti no lazima ipatikane mikakati bila ya hivyo kweli tutamwita majina yote fashist,dikteta lakini ameziba pamba anafanya msiyoyataka,na kumwita mtu majina mabaya ni dalili ya kushindwa
kurudi nyuma kujipanga si kosa,tulishindwa kusoma dalili mapema kabisa.
kurudi nyuma kujipanga si kosa,tulishindwa kusoma dalili mapema kabisa.