Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! Ni hivi , uongozi mkubwa kama urais ni karama kutoka kwa Mungu , karama hii hailetwi na vifaru .
Mimi nimeshukuru sana kwa haya yanayotokea na naombea Hawa Masikini wa nchi hii waendelee kukomeshwa kwa dhiki na shida nyingi zaidi ili iwe fundisho kwa masikini wengine duniani .
Tumekuwa tukiwaelimisha kwa miaka mingi sana lakini hawaelewi , sasa Mungu kawatandika kibao cha uso waache wakome , asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu .
Adui mkubwa wa nchi hii ni ccm hakuna fukara yoyote wa nchi hii asiyelijua hili , akifuatiwa kwa mbaali na mwovu shetani , lakini wao wameendelea kumkumbatia tu , wacha wakione cha moto .