Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Serikali ya wanyonge sasa mlo kwa mnyonge ni mmoja tu baada ya kuongeza bei ya sukari na gharama za maisha kupanda tu nakula ugali saa 10 jioni tu imetoka
Luwasa sasa hivi ni mweusi eeee! Baada ya kuhubiri kwa miaka 8 kote nchini kuwa yeye ni fisadi papa. Ukawa/wachumia tumbo bana,, jamaa aliwaweza yaani amewanunua wote! Its pathetic!!
Serikali ya wanyonge kina lugumi imejahidi kuwasafisha kina lugumi sasa ni weupe kama malaika
 
Luwasa sasa hivi ni mweusi eeee! Baada ya kuhubiri kwa miaka 8 kote nchini kuwa yeye ni fisadi papa. Ukawa/wachumia tumbo bana,, jamaa aliwaweza yaani amewanunua wote! Its pathetic!!
Eti kuna fisadi anapata sh 7m per min? Tanzania hii? Au nyingine?
 
Serikali hii imeibua watumishi hewa, imewachukulia hatua wezi wa mali za umma pamoja na kuanzisha mahakama ya mafisadi, imethibiti mapata bandarini, imeleta nidhamu kwa watumishi wa umma, inasimamia ukusanyaji wa kodi n.k, haya yote yameokoa mabilioni ya fedha.Hahaha! Katika Serikali hii ikiwa inaendelea kutumbua majipu Wale wa upande ule wakaanza kuwatetea wale wezi na waliowanyonya wanyonge kwa muda mrefu. Katika serikali hii upinzani unaendelea kupotea kwakuwa mpaka sasa wanatapatapa kwa kukosa hoja zenye mashiko. Ila si haba kwani tumeshuhudia wakifanya maigizo bungeni kitendo ambacho kilichekesha wengi na kuona wamepotoka. Hawa watu ni wa kupuuzwa.
ni kweli yamefanyika, sasa tujipime mwaka jana 2015 mwezi wa 6 na mwaka huu 2016 mwezi wa 6 ni kipindi kipi maisha ya mtanzania yalikuwa mazuri?
 
Mmeshaambiwa hamna tena haki ya "kuisema" serikali. Nafikiri kuisema maana yake ni "kuikosoa". Mnapaswa kuisifia tu. Ni serikali inayopenda misifa sifa tu, maana kila kitu inachofanya ni sahihi kwa asilimia 100.
 
Nimefurah sana maana huu mwakampya wa fedha ....machungu yake tuna yapitia wote
 
Mliozoea "Mapindo Mapindo" ngoja mnyooshwe kama Rula'!
Wenye kujua tulikotoka na tulipo sasa,tunajua dhamira njema ya Rais wetu!
Anataka kila mtanzania afaidi Utajili wa nchi yake.
 
Mada hazichangiwi kilumumba wala kiufipa, huchangiwa kimantiki.
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
Hakuna vision wala mission
 
Magufuli anatupeleka hapa:-
1. Nilikuwa nanunua mafuta ya gari 2,200 October 2015, sasa nanunua 1,782
2. Nilikuwa nafuatilia hati ya kiwanja changu Kigamboni toka 2011 nasumbuliwa, nimeenda January mwaka huu 2016, hati yangu imetoka March 2016.
3. Nilikuwa nikienda kwenye ofisi za uma kuhudumiwa ni kama vile naomba, sasa hivi nikiingia nahudumiwa kama mfalme.
4. Nilikuwa nafuatilia kuweka maji ya dawasco kwenye nyumba yangu toka 2014 nasumbuliwa, sasa hivi dawasco wamenifuata wenyewe waniwekee maji bure nitalipa kwa miezi 12 ijayo.
5. Nilikuwa nikishuhudia wafanyabiashara wakubwa wote wakikwepa kulipa kodi hapa bandarini, sasa hivi naona wote wakikimbilia TRA kulipa kodi wenyewe, na hakuna tena ki"memo" cha kutoa mzigo
6. Nimeshuhudia bajeti ya maendeleo ya Taifa ikiongezeka tofauti na miaka yote iliyopita, huku matumizi ya ndani tukiyagharimia kwa pesa zetu wenyewe.
7. Nilikuwa natumia masaa mawili toka sinza hadi mjini, sasa hivi MWENDO KASI natumia dakika 25.
8. Ninapotumia gari yangu Moroko hadi sayansi nilikuwa natumia saa nzima, sasa hivi nahisi natumia dakika 3-5 hivi
9. Wale waliokuwa wanafuja pesa na kusababisha vitu vinapanda bei, kwa kuwa wao hawabageni kwenye kununua, mfano kiwanja mtu anauza 20 million, wewe unajibana umbembeleze akuuzie 12 million, anatokea mfuja pesa zetu ananunua kwa 25 million, sasa hivi hakuna tena jeuri ya pesa zisizokuwa zako.
10. Ninashuhudia mengi ambayo nikimtafakari Magufuli, nahisi kuna haja ya kubadilisha katiba atawale miaka yote kama Mgabe.
 
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....

HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!
Ilani zilikuwepo toka enzi ya Nyerere lakini bado Nchi inayumba, imani zinatamka tu kama anavyotamka JPM ila hazieonyeshi dira wala speed ya tunakokwenda, yaani tutafikaje, mawaziri ndo weupe kabisa hawana hata strategic plan wapowapo tu, wanacheza Legee wakati inapigwa boringo, hawajuhi hata wanatakiwa kufanya nini kwa wakati huu....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom