Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hivi kama ni kweli kama wanavyodai CCM wenyewe kuwa kazi anayofanya Magufuli imerejesha imani ya Umma wa watanzania na hivyo kufanya wapinzani wakose hoja za kuwaambia wananchi, hebu CCM hao hao niwaulize maswali machache.Mpaka sasa mitaa inalia kwa sababu ya maisha magumu
Wale wa vijijini wanaokolewa na watu wa mjini
Elimu bure lakini bado kuna michango ya misosi huko shuleni
Madaftari kalamu pen penseli na vifaa vyote vya shule bado wazazi wananunua
Kama kuna watu walitaka mfumo wa vyama vingi enzi za nyerere na wote walikua wa chama kimoja basi ni vigumu sana kuzuia upinzani usikue tanzania eti kisa magufuli kapewa uenyekiti ccm!!
Mtu kama nyerere ambae hakua na doa kiutawala na bado watu walitaka kuwe na vyama vingi sembuse magufuli ambae ana kasha ya kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa
Kuisababishia hasara nchi kwa kukamata kwa kukurupuka meli ya samaki na sasa tunatakiwa kulipa
r upinzani tanzania utazidi kukua mpaka kuchukua dola kwa kua tuna viongozi wasiozingatia katiba ya nchi wasiojali ugumu wa maisha wanayopitia watu wa vijijini
Hivi kweli ni upinzani gani unakufa namna hii??
1.Ni kwa nini basi CCM hiyo hiyo ina hofu ya kupindukia hadi kufanya Rais Magufuli apige marufuku shughuli zozote za kisiasa zisifanywe na vyama vya siasa vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati chama chake cha CCM akikiruhusu kufanya shughuli zake za kisiasa bila kubughuziwa na Polisi?
2.Kama kweli Umma wa watanzania umerejesha imani kwa CCM kwa asilimia 100 kama ambavyo CCM wanavyotaka kutuaminisha, ni kwa nini basi CCM hiyo hiyo ina hofu kubwa kiasi ambacho haitaki kabisa Bunge lionyeshwe LIVE ili angalau tuwaone hao wabunge wa upinzani ambao CCM wanadai kuwa upinzani umeishiwa hoja?
3.Ni kwa nini yule mdada akiyekalia kigoda kule mjengoni Dom anaonyesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa CCM hadi kusababisha wabunge wa CCM wanawatukana waziwazi wabunge wa upinzani bila kuwachukulia hatua zozote wakati akiwabambikia makosa wabunge wa upinzani ili awatimue mjengoni ili atimize azma yake ya kulifanya Bunge hilo badala ya kutimiza wajibu wake Mkuu wa kuisamamia serikali, badala yake chombo hicho cha kuwakilisha wananchi kigeuke kuwa kama kikao cha NEC ya CCM kwa kuikingia kifua serikali?
4.Ni kwa nini teuzi zote za muhimu za utumishi wa Umma zimegeuka kuwa teuzi za kuwapa 'ulaji' makada wa CCM badala ya kuwa teuzi za kuangalia utendaji wa mtumishi mwenyewe bila kuangalia itikadi yake ya kisiasa kwa kuwa mtumishi wa Umma hapaswi kuonyesha mapenzi yake waziwazi kwa chama chake kwa kuwa utumishi wa Umma ni utumishi kwa watanzania wote na sio utumishi kwa chama chake cha CCM pekee?
Kwa mapungufu hayo ya serikali ya awamu ya 5 na utawala wa kibabe anaouendeleza Mkulu ambao unafanya hali ya uchumi kwa mwananchi kuzidi kuwa ngumu mitaani kunaendelea kufanya wananchi wengi waendelee kupoteza imani kwa serikali hii ya awamu ya 5 kutokana na serikali hiyo kuwafanya wananchi waishi kama mashetani........