Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Weweee uko wapi? East afrika yote kwa sasa inatawaliwa kwa mfumo mmoja! Kaka zake Rwanda,Uganda,Burundi nk hujawaonaaa! Ni hiviii marufuku kutoka ikulu! Unatokaje ikulu kirahisi! Kalaga baho!
Wengine wanajiita KOTA PINI
 
kwa bahati mbaya sana ninashangazwa na watu ambao huchukua maneno ya utani katika hotuba na kujaribu kujenga hoja. Hizi ni dalili za kufikisika. Nilitegemea tungejadili mikatika JPM anayoeleza kufufua na kujenga viwanda hapa nchini. Lakini uzi nyingi zinazoletwa humu zinzkwepa hoja za msingi kwa makusudi na kujikita katika mambo ya utani ndani ya hotuba zake.
Kwani hayo maneno hakuyatamka?
 
Kuna kila dalili kuwa huyu jamaa anaweza akafanya 'attempt' ya kuliconvince Bunge ili liweze kuondoa kile kipengele kinachoweka ukomo wa vipindi vya kutawala.......
Hii naamini kwa 95% Ndio ukweli
 
Hao wasukuma si ndio wamemweka hapo kwa kura nyingi? Au haujui maana ya tyranny of numbers? Wanaoamua Rais awe nani ni kanda ya ziwa, dar, moshi, arusha, mbeya mlimnyima kura ilisaidia nini kanda ya ziwa waliposema sema ndio? So endeleeni, 2020 tunamjazia tena atuletee maendeleo, nyie endeleeni kuzungusha mikono mpaka 2025.
Una cha kupoteza Shemeji ameshaemea ukiamka unakwenda kupanga folen ya msosi ujui hata bei ya chumvi wanaume wanaposema maisha magumu wewe kaa kimya
 
Sijpui kuhusu huko kwenu...lakini huku kwetu sasa shuga ni 1500...sukari sio agenda tena, mpo hapo wazee wa matukio?
Rudia ulicho kiandika ndio utajua sukari ina kazi yake mwilini na kwa afya ya akili
 
Umemsahau mzee wa pushapu?
Kila ninapo msikliza naona amenogewa na kazi hii ya Urais ingawa bado hajajuwa namna ya Ku bahave na kuwa kiongozi Mwenye tija.Jambo moja is too ambitious kiasi kwamba kama malengo take hayatafikiwa atatamani abaki milele. Ukitaka kuja undani Wa mtu angalia marafiki zake.Rafiki take Mkubwa Ni Kagame ! Naam, president Wa muyaya Wa Rwanda!!!
 
Huyu atakuja kuifanya tz kuwa kama Zimbabwe, atavuruga uchumi wote na Kila kitu subirini tu
 
Kuruka ruka kwa maharagwe ndo kuiva kwake JPM kaza kamba mpaka tunyooke baba
 
Kila ninapo msikliza naona amenogewa na kazi hii ya Urais ingawa bado hajajuwa namna ya Ku bahave na kuwa kiongozi Mwenye tija.Jambo moja is too ambitious kiasi kwamba kama malengo take hayatafikiwa atatamani abaki milele. Ukitaka kuja undani Wa mtu angalia marafiki zake.Rafiki take Mkubwa Ni Kagame ! Naam, president Wa muyaya Wa Rwanda!!!

Rwanda nchi ndogo kila mwanafunzi wa shule za msingi anatumia kompyuta mpakato (Laptop), hivi sasa Rwanda wataalamu wa IT wa Rwanda wanatengeneza software za kiswahili.

Kama huo ndio udikteta, basi udikteta huo ni mzuri mara 100 kuliko demokrasi ya watoto kukaa chini, kukosa madarasa, madawa kukosekana hospitalini n.k
 
UKAWA MNATAPATAPA kazi mnayo, jiandaeni kuchukua Ikulu ya Dsm maana lengo lenu ni kujihisi mko Ikulu. Chukuweni Edo akae muwe mnaenda kumsalimia pale.
Maguguli anafaa na anaenda vizuri tutafika tu.
 
kwa bahati mbaya sana ninashangazwa na watu ambao huchukua maneno ya utani katika hotuba na kujaribu kujenga hoja. Hizi ni dalili za kufikisika. Nilitegemea tungejadili mikatika JPM anayoeleza kufufua na kujenga viwanda hapa nchini. Lakini uzi nyingi zinazoletwa humu zinzkwepa hoja za msingi kwa makusudi na kujikita katika mambo ya utani ndani ya hotuba zake.
Kuhamasisha uzazi bila mpango ni suala la utani?
Kugeuza ikulu kuwa jumba la maonyesho ni utani?
Kusema buku 5 kwa trafik police in ya kung'arishia viatu ni utani?
kusema utawalinda wastaafu hata kama walifisidi nchi ni utani?
kuwaita watoto wa wapiga kura maskini Vil.aza ni utani.
Kuchagua majipu ya kutumbua ni utani?
Kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano na maandamano kwa mujibu wa sheria ni utani?
Kusema mambo ya zanzibar hayamhusu raisi wa JMT isipokuwa tushughulikia wanaoleta fyokofuoko ni utani?
Kusema kuwa unaweza "kuwapoteza" wanaoimba sifa za fulani ni utani?

Kauli za vitisho, kejeli na dharau zinapotolewa na kiongozi yeyote makini haziwezi siku zote kutafsiriwa kuwa ni utani. Kiongozi mkuu anatakiwa kuweka akiba ya maneno huku matendo yakishamiri.
 
Basi kimponzacho samaki ni mdomo wake

HIVI HAYA HAPA CHINI TOKA MDOMONI MWAKE HUKUYASIKIA?

Rais Magufuli alisema alipoingia alikuta makusanyo ya mapato ni Sh bilioni 850, lakini baada ya kubana mapato yaliongezeka hadi Sh trilioni 1.5, akisema makusanyo hayo yalikuwa yakiliwa na wachache wachache walioko ngazi ya juu.

Aliongeza kuwa spidi yake ya kufanya kazi ni kubwa hivyo hataki kuona mtu anamkwamisha kwa kuwa amepanga kufanya mambo mazuri. Alisema ndio maana wameamua kujenga reli ya kisasa ili kubeba mizigo ya kutosha, kununua ndege tatu na mbili zitaingia mwezi ujao na kwamba serikali imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya kuboresha viwanja vya ndege vya Iringa, Songea na Musoma.

Alizitaja huduma nyingine ambazo serikali imeamua kuboresha ni umeme ambapo mradi wa Kinyerezi II una megawati 240 na Kinyerezi I utaongezewa megawati 185 na pia Kinyerezi III na IV inakuja ili kuongeza usambazaji wa umeme nchini uwe mkubwa.

Alisema bajeti ya maji mwaka huu imeongezwa na pia kwa Dar es Salaam kuna mradi wa maji unakuja, na pia wamepata mkopo wa dola za Marekani milioni 500 (sh trilioni 1.05) kutoka Serikali ya India.

Kwenye sekta ya afya, alisema wametenga Sh trilioni 1.99 na kwamba wametenga Sh bilioni 200 kwa ajili ya kununulia dawa hospitalini tofauti na mwaka uliopita ambapo ilitengwa Sh bilioni 25.

Chanzo: Habari Leo
 
Huna uwezo wa kunichagulia cha kusikiliza maana mimi siyo mpiga marimba kama wewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom