Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Nashuhudia kura za CCM uchaguzi ujao kuvunja historia kwa kuwa chache zaidi ya miaka yote
Natamani uchaguzi uwe hata leo. Nakuapia, huyo rais wa mioyo yenu, atabaki humo humo na hatathubutu kutoka tena!
 
Nakumbuka watu tulikuwa na imani na kikwete na kumshangilia kwa miaka miwili, lakini huyu hata mwezi tayari tushamchokaa

Mmeshachoka kwani mliwahi kumhitaji lini?Kura mlimpa Lowassa kwa hio tuliempa Magufuli sisi tunamuunga Mkono.jipangine 2020
 
Ninashuhudia mafisadi yakisakwa; Ninashudia mafisadi yakitumia vyama vya siasa kumdhoofisha; Ninamshuhudia akipambana NATO bila kuchoka; Ninamshuhudia wazalendo wa nchi hii wakiwa nyuma yake katika mapambano ya kuijenga Tanzania mpya; Ninamshuhudia watu wa mataifa mbalimbali wakitamani angelikuwa rais wao; Ninamshuhudia akiendelea kufanywa 'SI UNIT' ya uongozi bora Africa; Ninamshuhudia, Ninamshuhudia ...!
Ungeyasema haya mtaani kwetu, ninauhakika ungetemewa makohozi, jamaa yako watu hawataki kumsikia hata kwa jinsi alivyoharibu uchumi! Mtaani hakukaliki
 
Wabongo walikuwa wamezoea mafisadi yao sasa yeye kayafurusha wapi na wapi? Nimeanza kukata tamaa na nchi hii na hata aje Yesu mwenyewe atutawale mijitu italalamika tu.

Kupigana na mafisadi na wakwepa kodi siyo kazi lelemama. Ni kazi ya hatari. Ni kazi ya kujijengea maadui. Ndiyo maana wengi huwa wanaikwepa. Huyu yeye angalau amejaribu na kusema kweli nidhamu yetu kama taifa imerudi na pengo hatarishi lililokuwa linakua kwa kasi kati ya mafisadi na watu masikini limeanza kupungua.

Kama unatafuta uongozi ili upendwe au usiwe na maadui hasa katika nchi iliyooza kama yetu wewe hufai. Mungu Amsaidie angalau afikie nusu ya malengo yake.
 
Nimeshuhudia vijana Wengi kukosa ajira Na wakati hapa kazi tu. Au kazi ya kuiba
 
Wabongo walikuwa wamezoea mafisadi yao sasa yeye kayafurusha wapi na wapi? Nimeanza kukata tamaa na nchi hii na hata aje Yesu mwenyewe atutawale mijitu italalamika tu.

Kupigana na mafisadi na wa wakwepa kodi siyo kazi lelemama. Ni kazi ya hatari. Ni kazi ya kujijengea maadui. Ndiyo maana wengi huwa wanaikwepa. Huyu yeye angalau amejaribu na kusema kweli nidhamu yetu kama taifa imerudi na pengo hatarishi lililokuwa linakua kwa kasi kati ya mafisadi na watu masikini limeanza kupungua.

Kama unatafuta uongozi ili upendwe au usiwe na maadui hasa katika nchi iliyooza kama yetu wewe hufai. Mungu Amsaidie angalau afikie nusu ya malengo yake.
Mbona unaandika kama hii nchi Dikteta ameipokea toka utawala wa mafisadi wa chama cha CUF au TLP .... ?![emoji15]
 
Ninashuhudia upigaji ukipungua

Ninashuhudia hela chafu ikipungua mtaani

Ninashuhudia watanzania wakianza kuthamini kufanya kazi kwa bidii maana hakuna hela ya fast fasta ya wizi wizi

Ninashuhudia bei za vitu zikianza kuwa halisi badala ya kurushwa rushwa kutokana na kuwepo hela bwerere kwenye mzunguko

Ninashuhudia Elimu inaanza kuthaminiwa

Ninashuhudia upinzani ukikosa mwelekeo maana wanakosa madhaifu katika kuikosoa serikali

Ninashuhudia wapinzani wakianza kutumiwa Na watumbuliwa kuihujumu serikali

Nashuhudia magenge ya kifisadi kutoka nje yakianza kutumia wapinzani kuiharibia serikali
 
Mbona unaandika kama hii nchi Dikteta ameipokea toka utawala wa mafisadi wa chama cha CUF au TLP .... ?![emoji15]
Ulitaka niandikeje? Mimi nimeandika kama Mtanzania mzalendo na simo katika ushabiki wa kisiasa kama wewe. Ndo maana umeshindwa kunielewa!
 
Nakumbuka watu tulikuwa na imani na kikwete na kumshangilia kwa miaka miwili, lakini huyu hata mwezi tayari tushamchokaa
Kachokwa kama tulivyo mchoka Lipumba CUF.Tatizo kukamia sana. Mkamia maji mata zote hayanywi.Tutajikuta miaka imeisha hakuna kiwanda hata kimoja.
 
Wabongo walikuwa wamezoea mafisadi yao sasa yeye kayafurusha wapi na wapi? Nimeanza kukata tamaa na nchi hii na hata aje Yesu mwenyewe atutawale mijitu italalamika tu.

Kupigana na mafisadi na wakwepa kodi siyo kazi lelemama. Ni kazi ya hatari. Ni kazi ya kujijengea maadui. Ndiyo maana wengi huwa wanaikwepa. Huyu yeye angalau amejaribu na kusema kweli nidhamu yetu kama taifa imerudi na pengo hatarishi lililokuwa linakua kwa kasi kati ya mafisadi na watu masikini limeanza kupungua.

Kama unatafuta uongozi ili upendwe au usiwe na maadui hasa katika nchi iliyooza kama yetu wewe hufai. Mungu Amsaidie angalau afikie nusu ya malengo yake.
Nashindwa kuelewa kwa nini ukabila umetamalaki ndani ya miezi kumi tu ya utawala wake!? Mmebakia wasukuma tu mnaoamini kuwa anapambana na mafisadi wakati wazee WA escrow wako mtaani wanatumia zile hela na IPTL inaendelea kulipwa.
 
Wabongo walikuwa wamezoea mafisadi yao sasa yeye kayafurusha wapi na wapi? Nimeanza kukata tamaa na nchi hii na hata aje Yesu mwenyewe atutawale mijitu italalamika tu.

Kupigana na mafisadi na wakwepa kodi siyo kazi lelemama. Ni kazi ya hatari. Ni kazi ya kujijengea maadui. Ndiyo maana wengi huwa wanaikwepa. Huyu yeye angalau amejaribu na kusema kweli nidhamu yetu kama taifa imerudi na pengo hatarishi lililokuwa linakua kwa kasi kati ya mafisadi na watu masikini limeanza kupungua.

Kama unatafuta uongozi ili upendwe au usiwe na maadui hasa katika nchi iliyooza kama yetu wewe hufai. Mungu Amsaidie angalau afikie nusu ya malengo yake.
mafisad
Kachokwa kama tulivyo mchoka Lipumba CUF.Tatizo kukamia sana. Mkamia maji mata zote hayanywi.Tutajikuta miaka imeisha hakuna kiwanda hata kimoja.
ni nilichogundua uongozi ni kipaji na sio elimu
 
Yaaaani huyu tushamchoka kwa kweli.
Lakini si mnaendelea kumwombea kwa Mungu? Hilo msisisite, siku mkiacha kumwombea mtegemee moja kati ya haya, atawapatia maburungutu ya fedha au atawatumbua.
Mbona honeymoon yake imeisha so fast?
Huyu honemoon imeisha vipi? Si aliwaambia wadanganyika kwamba akiwa yeye watu watalimia kwa meno na walimtaka akachukue fomu? Baada ya kusimikwa na Tume huru aliwaambia wadanganyika atawatumbua na wenyewe hawakufurahi na kumpigia makofi? Sasa honeymoon inaishaje hapo?

Mwenyewe anajua honeymoon yake inaisha baada ya miaka 10 atakapomkabidhi mtu ingine ya chama dola kijiti. Honeymoon ya kupokezana, kupokezana "baton". Mwenyewe ana honeymoon na vyombo vya ulinzi na usalama. Hiyo inamtosha, wadanganyika waisome namba tu na wamwombee kwa Mungu.

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom