Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mkuu shuka ukapande usafiri mwingine uelekee unakokujua ww maana hakuna namna sasa
 
wana Jf
Naomba mnisaidie na huu ugonjwa wa hewa kwa nini unawapata na ambao hawahusiki nao, katika swala hili la ajira mpya imegeuka kuwa hata matamko ya viongozi wetu nayo ni hewa!!!

Nauliza, kila kitu hapa Tanzania kimekuwa hewa??! tuelewe!!?
 
Kwa kuwa hewa ni kitu cha bure hakilipiwi kodi wala hakinunuliwi ndio maana hewa hewa hewa na kila mtu anaitumia haiishi
 
Hiyo ni kete tu ya kisiasa kusaidia watu kuficha ukweli kuwa wana miezi 10 madarakani lakini hali ni ngumu bora hata utawala uliotangulia
 
HAYA MANENO ALIYASEMA MH.RAIS MAGUFURI AKIWA KWENYE ZIARA YAKE KANDA YA ZIWA JE?UKWELI UPO AWAMU HII WAKULIMA WANALALAMIKA JUU YA MAZAO YAO KUKOSWA SOKO VIJANA WANALALAMIKA AJIRA HAKUNA WATUMISHI WA UMMA HAWANA STAHIKI ZAO ZA MSINGI MFANO UHAMISHO KUPANDA MADARAJA
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

I wish clip hiyo ya JKN,RAIS wangu angekaa nayo siku moja nzima usiku na Mchana akaisikiliza labda angetoka na kitu akafuata anachozungumza JKN.
 
Wanaoporomosha matusi hawajui hali za ofisi zetu wao hushinda kwenye mitandao tu

Watanzania tumekuwa watu wa Ndiyo tu tukisubiria ukuu wa wilaya au Ukuu wa mikoa.Tunaenda kama vipofu
 
Takribani miezi kumi sasa tangu watz wachague wabunge madiwani na rais wao mnamo October 25 2015

Raisi aliaanza vizuri sana, na akasisitiza raia waungane kumwombea ili uongozi wake ulete tija kwa haraka.

Mpaka sasa kuna sintofahamu juu ya haya mambo yafuatayo

1-Sukari na bei elekezi bado ni tatizo

2-Waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi huku wakiendelea kulipwa mishahara

3-Wafanyakazi hewa mpaka sa hii bado tatizo

4-Madawati mashuleni tayari, kashindwa kuajiri walimu wapya

5-Wahudumu wa afya bado hajaajiri

6-Bunge + mikutano ya kisiasa

7-nasikia noti yapotea kwa mtaa, nani kaficha? sababu ni nini

Au mungu hapokei maombi tena.... poleeni majirani
 
Asante. Tushapoa. Tutafanya nn sasa? Ukiongea kidogo tu utaitwa mchochezi
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
Wale Kijani watakwambia tumpe mda wakati siku njema huonekana asubuhi,,, Hii imeshafikisha miezi kumi hamna hata dalili,😛😛😛😛😛😛😛
 
Wadau wa JamiiForums mimi ni kada wa CCM wa mda mrefu ila kuanzia leo naachana na CCM na sitajihusisha na chama chochote cha siasa nimeona siasa ni mchezo mchafu sana kwa sababu zifatazo.

01.Wanasiasa kusema waongo kwa sababu ya ahadi wanazozitoa kwa wananchi bila kutekeleza mfano.zoezi la uhakiki wa watumishi hewa halitazidi miezi miwili huu tayari ni mwezi wa tatu

02. Wanasiasa kutojari wananchi wao kwa kutoa kauli tata mfano.wanaolalamika hakuna hela ni wapiga dili
 
WADAU WA JAMII FORUM MIMI NI KADA WA CCM WA MDA MREFU ILA KUANZIA LEO NAACHANA NA CCM NA SITAJIHUSISHA NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NIMEONA SIASA NI MCHEZO MCHAFU SANA KWA SABABU ZIFATAZO.

01.WANASIASA KUSEMA WAONGO KWA SABABU YA AHADI WANAZOZITOA KWA WANANCHI BILA KUTEKELEZA MFANO.ZOEZI LA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA HALITAZIDI MIEZI MIWILI HUU TAYARI NI MWEZI WA TATU

02. WANASIASA KUTOJARI WANANCHI WAO KWA KUTOA KAULI TATA MFANO.WANAOLALAMIKA HAKUNA HELA NI WAPIGA DILI.
wewe hukuwa mwana ccm kama tunavyowafahamu nduguzo.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Labda tutakapofika ndio tutajua tulikua tukielekea wapi??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom