Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Labda huna MACHO
 
Mi naomba watulegezee wakulima , zao kama mbaazi hali ni mbaya wafanyabiashara wakubwa wanasema tatizo ni vat bandari, mwaka Jana tuliuza kilo kwa 3500 mwaka huu ni 1000 kwa kilo. Mi naamini magu anania nzuri sana na nchi ytu .
 
Wakati wa Kikwete, ufisadi ulikuwa juu, wafanya kazi hewa kwa wingi, wanafunzi hewa usiombe, misafari ya nje, makusanyo kiduchu LAKINI maisha yalikuwa nafuu sana.. Wakati huu hayo yote yamedhibitiwa yote, makusanyo yameongezeka HALI NI NGUMU KULIKO MAELEZO. Mshahara ya wafanyakazi kupandi hawaoni hata dalili, ajira zoye zilishasimama! Pesa zinaenda wapi?? Je jamaa anatimiza adhima ya watu kuish kama mashetani!!?
 
Amekwisha sema kuwa malipo (siyo pesa) ni kwa wale wanaofanya kazi tu. Fanyeni mtapata malipo nanyi mtabadilisha kuwa pesa. No kazi no money. Enzi za Kikwete mlikuwa namzitumia huko huko juu kwa juu. Sasa makusanyo yote yanalipwa ndani kwa ndani. Mwenye masikio na macho....
 
Tusipotoshwe na kauli maisha ya shetani hapa duniani ni ya starehe sana na ndio maana hata kule jangwani alimwambia Kristo amsujudie ili ampe milki ya ulimwengu wote
 
Sijui tutakua katika hali gani wakati tukitathmini miezi 12 ya hapa kazi. Hata hivyo tungepaswa kuwa na rundo la ahadi mbalimbali katika hotuba maeneo tofauti alikopita mwenyekiti wa sasa wa CCMna mh rais J,pombe.Katika ahadi hizo nyingi ni barabara za lami ktk maeneo alikopita kwa barabara. Ombi langu tuanze kujikumbusha ahadi na kutiki kiwango cha utekelezaji mikoa yote tz
 
Nikiwa mwana CCM aliyeshiriki kwenye kampeni kwa hali na mali, mwisho wa siku niliona mbali na kumpa kura yangu Ndg. Dovutwa.

Wenzangu, tena vigogo wanajilaumu sana Kwa kufanya maamuzi Mabaya. Hasa baada ya kuzisikia kauli Tata za Rais Magufuli kule Zanzibar. Kwa kifupi bora nilimpa Dovutwa kura yangu.
 
Ulichokosea ni kuwahadaa watanzania kwenye majukwaa ya kampeni ilihali unaujua ukweli. Hii dhambi itakutafuna usipotubu
 
Uwa naandika matukio yote yanayoendelea Tanzania kuanzia mwanzo mwa Utawala wa hawamu ya 5...Kikwete pamoja na udhaifu wake aliweza kosovu mambo mazito ya taifa Kwa kutoa hotuba za kiwango cha hali ya juu na kuwalizisha wananchi.

Kila ulipokuwa ukimsikiliza unapata matumaini ya kesho .
Kumbuka alivyosovu mgogoro wa Wakulima na Wafugaji!!
Kumbuka alivyosovu mgogoro wa Madactari.
Kumbuka alivyosovu mgomo wa walimu .
Kumbuka alivyosovu mgogoro wa Malawi.

Na kumbuka alivyosovu mgogoro wa Rwanda.
Hivi kama unashindwa kukabiliana na insu Ndogo kama Sukari unaweza pambana na Mgogoro wa wakulima na wafugaji, Migomo ya walimu na Madactari?

Aliwatisha watu wakaficha sukari tukaanza kumtafuta mchawi mpaka sasa hatujampata ilo likamsinda.

Likaja swala la mchanga wa kule Kahama akawatisha lakini yakamsinda na atimaye mchanga umeanza kusafirishwa tena .
Tukaja kwenye swala la bandari akawatisha wafanya biashara mwisho wake ameanza kuwabebereza.

Sasa hivi tunakaribia kumuona akitoa tamko la kuondoa VAT kwenye utalii na kuwaomba watalii waje Tanzania.
Stay turned continue to watch this movie!!
 
Mi naona ungejuta kumpa kura yako Dovutwa mtu ambae hana ndoto za kuwa kiongozi katika nchi hi zaidi ya kupiga ramli tu
 
Naona jana viongozi wa ukawa walikutana na mzee kupatania bei ya cuf.
Mzee anataka kuinunua aiunganishe na chagadema
 
Mbona ameshaanza kunyosha mikono mapema..ni sawa na baunsa kumtisha bwana mdogo wa mtaani alieshika KY...utasikia tu sauti "ameninaliii lakini kwa tabu sana"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom