Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ni bora kujitia uchizi..ili kulinda ajira mana..kichaa kapewa rungu..usijaribu kupita mbele yake..[emoji445] [emoji445] [emoji445]
 
wataalaamu ndio wametuibia sana na kusababisha nchi isiendeleeee

hatutaki ushauri wao..

wataalamu wameshawai kugundua nini?

hata kujenga barabara hadi tuwatafute wazungu strabag halafu unasema tuna wataaalamu...

hata ningekuwa mimi rais hao wajinga wanaojiita wataaalamu ningewatia viboko wote
 
Mjomba amezidisha ubabe hata kwenye vitu vya maana.Washauri wa mjomba nao wameamua kuwa wanafiki uku wengine wakijitoa ufahamu.Anataka nchi anayoifikiria kichwani mwake bila ushauri wa mtu.Maji yatakapozidi unga wakati unga umeisha ndo atajua Watanzania siyo watu wa spoti spoti.
 
Ni bora kujitia uchizi..ili kulinda ajira mana..kichaa kapewa rungu..usijaribu kupita mbele yake..[emoji445] [emoji445] [emoji445]
Huo ndio upuuzi wa kichaa,muda wote rungu analizungusha hewani hata haujui litatua kwa nani na saa ngapi !!!? Sasa ni mwendo wa kujihami tu
 
Kuna kitu kimoja tu Shetani hutenda vyema; ni kwa Shetani kukiri moyoni kwamba Mungu ni Mungu; japo ataeneza uzushi kwa viumbe wengine kuwadanganya vinginevyo lakini moyoni mwake daima anakiri, na hana namna nyingine, isipokuwa Mungu kweli ni Mungu japo kukiri huko hakuna msaada wowote kwake.
 
well inawezekana hatumuelewi lakin ajuwa kule anatupeleka maana anaijuwa njia vizuri hivyo kuingia kwake vichochoron ambako mimi na wewe hatujuwi njia isiwe ndio sababu yakusema hajuwi kule anatupeleka. Tumpe muda na kwa kuwa uchochoro anapita sisi hatuujuwi ila bila shaka tutafika na tusipo fika tutakuwa na nguvu kumwambia umetupoteza achia uskani.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
well inawezekana hatumuelewi lakin ajuwa kule anatupeleka maana anaijuwa njia vizuri hivyo kuingia kwake vichochoron ambako mimi na wewe hatujuwi njia isiwe ndio sababu yakusema hajuwi kule anatupeleka. Tumpe muda na kwa kuwa uchochoro anapita sisi hatuujuwi ila bila shaka tutafika na tusipo fika tutakuwa na nguvu kumwambia umetupoteza achia uskani
 
well inawezekana hatumuelewi lakin ajuwa kule anatupeleka maana anaijuwa njia vizuri hivyo kuingia kwake vichochoron ambako mimi na wewe hatujuwi njia isiwe ndio sababu yakusema hajuwi kule anatupeleka. Tumpe muda na kwa kuwa uchochoro anapita sisi hatuujuwi ila bila shaka tutafika na tusipo fika tutakuwa na nguvu kumwambia umetupoteza achia uskani
Hata kama ss njia hatuijui, lakini kwa mwenye akili timamu unaweza tu ukapata idea kutokana na mandhari ya njiani, hapa dalili zinakatisha tamaa. Halafu mwengine kweli anapokupeleka panaweza kuwa pazuri na zipo njia nzuri zakufika huko lakini anaamua tu kukupitisha kwenye njia za ajabu ajabu ili uteseke tu. Unapo lia lia na kupiga kelele yeye ndio anasikia raha eti ili mwisho akupe surprise, ss ndio nn? Hata tukifika, kwa njia hizi na majeraha tutakayo yapata, mara nyengine akitangaza safari tunaweza goma kwenda.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tuna bahati mbaya kwamba kwa nchi yetu ya Tanzania tunaishi kwenye ndoto za mchana za viongozi wetu,matamko,makaripio,kauli mbinu na sio mipango madhubuti ya maendeleo.Tujiulize tangu uongozi wa awamu ya tano uingie tumejenga viwanda vingapi?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ki ujumla viongozi wetu ni wapumbavu.
no watanzania ndio mataahira kwa kuaminishwa vitu visivyoingia akilini,nchi haina maji haina umeme,hakuna elimu kwa ufupi wananchi wanapigania basic needs kila siku kisha anasimama mtu anaongea uchumi wa viwanda,nchi zenye uchumi wa viwanda basic needs wamesolve miaka 100 iliyopita
 
Serikali ya sasa haina watu ambao wanajua utekelezaji imekuwa serikali ya matukio tu na ushabiki. Hakuna plan nzuri ya elimu zaidi ya elimu ya bure!, plan nzuri ya makazi na nyumba, plan nzuri ya afya, plan nzuri kwa wafanyabiashara . Plan za umeme ni zilezile ndiyo pekee zipo. Tatizo kubwa ni kwa uongozi wa juu kutaka ku control kila kitu wakati hawana ujuzi na kama tulivyosema hakuna watu wabaya kama wasomi ambao hawana uzoefu na proven record .. hawa ma professor watatuletea umasikini tu wakati mwingine muuza duka anaweza kufanya kazi zaidi ya professor maana anajua results
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom