Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kama ameamuwa kuzika kazi ya Uwakiki wa vyeti Fake kisa Makonda....awezi kufanya lolote tena akaaminika....
 
YAANI WEWE NDUGU YANGU MUNGU AMEKUSAIDIA UMESOMA HADI CHUO KIKUU,MBAYA ZAIDI UMESOMESHWA KWA KODI YA SERIKALI ,
MBAYA ZAIDI UMEPEWA HADI MKOPO NA PESA ZA KUJIKIMU KIMAISHA LEO HII UNAKUJA KULALAMIKA SERIKALI MBAYA WAKATI KUNA WENZIO HIYO NAFASI ULIYOIPATA WANAITAMANI ANGALAU WAWE KAMA WAWE

Kwani serikali iltowa wapi hizo kodi? Si kwa wazazi wake au?
 
Nakubaliana na mawazo yako hasa pale unapolink mazao ya kilimo kama inputs katika viwanda tunavyotegemea kuvijenga, tatizo linakuja pale unaposema kuuza nchi za nje huku tukishindana na wengine!!! Hapa kuna suala la teknolojia ambayo viongozi wetu wanafikiria viwanda vyetu vitatumia; mara nyingi wao husisitiza na kuamini kuwa viwanda tutakavyojenga vitaajiri watu wengi hivyo kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana, lakini ukweli usiopingika ni kwamba teknolojia ya leo duniani haitegemei tena binadamu[ kuongeza ajira] bali viwanda hutumia ROBOTS na bidhaa zao ni za quality ya juu sana ambayo sisi kushindana nao itakuwa mtihani mkubwa!!

Viongozi wetu wasiwe wanabwabwaja tu bila kufikiria kwa kina hivyo viwanda tunavyotaka kujenga vitatumia teknolojia gani ili tuweze kushindana katika ulimwengu wa leo!!!
Kweli mkuu yaani Jamaa anaota tu wenzao walipanga mipango kwa kuona mbali. Elimu ya watu.nishati.masoko had I wakafika walipo
 
Hujui vipi ? Tunaenda kuishi kama mashetani. Sasa mashetani wanaishi vipi ndo suala la kujiuliza kwani mimi sijui na wrwe hujui wanaishi vipi...
Na huwezi kujua hayo maisha ya kishetani kama hukuyapitia...
Hivo tulieni tunaelekea huko bombadia itakuchukueni
 
Mwenyewe hajui anakotupeleka!
Mtu ambaye anaweza kuasi kauli zake mwenyewe (wenye vyeti hewa waondoke wenyewe) utakuwaje na matumaini naye?
Leo hii watu wanasherehelea mubashara ulaji waliopata kwa kutumia vyeti fake!
 
Jiulize kwanza wewe mwenyewe, hapo ulipo ni wapi, pili unataka kuelekea wapi na tatu utafikajefikaje huko unakotaka kwenda.
Lakini ukisubiri mtu mwingine akupeleke huko unakotaka kwenda ndugu yangu, we utakuwa ni mzigo tena mzigo wa misumari juu ya mgongo wa mwenzio.
 
We end

Endelea na utalii Wako,, hujaelewa , kifupi Ni kwamba nchi inaendeshwa na katiba na sheria za nchi kama zinavunjwa, huduma mbovu hosp., mahakama inashindwa kusimama katika muhimili wake, Polisi wanavunja sheria za nchi kwa kutumia nguvu nyingi ili kuwafurahisha wakubwa unataka uambiwe nini sasa wewe,?? Mfumuko huu WA bei nao huuoni?? Kwendraaa
 
Nimesikitishwa sana na mwelekeo mbaya wa nchi yetu Tanzania na nitaendelea kuisalia na kumuombea Magufuli abadilike kidogo ili hii nchi yetu nzuri iweze kusonga mbele. Wakati Magufuli anaingia madarakani nilifurahi sana sana na kufikiri nchi itabadilika lakini sikujua kwamba serikali itakosa mwelekea na ubunifu kwa kiasi kikubwa hivi. Nina matumaini kwamba bado serikali ina nafasi ya kubadilika na kubadilisha nchi yetu haya ni mambo ambayo sikutegemea lakini ni ushauri wa bure.
1. Serikali inatakiwa kudumisha demokrasia. Ni muhimu serikali kudumisha demokrasia maana kwenye serikali yetu wanacho fanya ndiyo itakuwa standard. Kitendo cha Magufuli kufuatilia wapinzania ni kibaya sana kwani hakihatarishi serikali ya sasa pekee lakini inafanya ukandamizaji kuwa kama utaratibu kwa nchi yetu. Hivyo uongozi ujao hakuna ambaye atawazuia kufanya mabaya zaidi. Cha kujiuliza je tukiwa na serikali na viongozi wabaya hapo mbele na tume minja wapinzani ni nani atakuwepo kurekebisha serikali... ina maana kiongozi mbaya mmoja anaweza kuaribu nchi na progress ya miaka mingi sana.
2. Uchumi: Inaelekea serikali haina plan na hawajui vizuri waanzie wapi kwenye kuimarisha na kukuza uchumi wetu. Hii ni kawaidia lakini serikali inatakiwa kujua waanzie wapi kukuza uchumi. Nawashauri fanyeni hivi ili muwe na process yenye majibu (1) Serikali inatakiwa iweke mandate kwa Bank kuu ya Tanzania ya kwamba kazi mojawapo ya bank hiyo ni kupunguza unemployment. Hii ita lazimisha bank kuu kuhakikisha riba za bank ziko chini na kwa kufanya hivyo wataongeza mikopo kwa small business na kuongeza ajira (2) Ajiri consulting company na kusaidiana na mkaguzi mkuu wa nchi kuangalia tax zote za nchi hadi local na kutoa ushauri wa marekebisho na step by step kwenye kiasi kizuri na endelefu cha tax za nchi na pili kufuta tax zote ambazo hazisaidii kukuza uchumi. Ni lazima tuelewe tax zetu ni sababu mojawapo ya kupunguza ajira na ukuaji wa uchumi. Lakini pamoja na haya mapunguzo ni lazima iwe rahisi kujua kirahisi kodi ya vitu mfano mtu akiingiza gari au vifaa vya ujenzi inatakuwa ajue kwa uhakika ni tax kiasi gani atalipa ili aweze ku calculate cost ya capital hata kama ni mkopo. Utaratibu wa sasa ni kwamba bandarini wanafanya tathimini upya ya gharama ya vitu na mara nyingi wana over estimate vitu hii ina discourage investment mfano mtu ana nunua gari kwenye mtandao anatuma pesa kwa bank lakini bado ni kama serikali haiamini.. uncertain ni sababu kubwa sana ya kupunguza uwekezaji.
3. Punguzeni mlolongo wa vibali vya ujenzi. Mtu akitaka kujenga au kampuni ni tayari wana capital na serikali inatakiwa ipunguze mlolongo wa vibali ambao umejaa rushwa na usumbufu. Ujenzi unasaidia sana unchumi maana unaajiri kwenye kila sekta. magari, madereva, mafuta, mafundi, cement, nondo... na vifaa vya finishing kuna pesa ina inaongezeka na kufanya kazi mara nyingi sana.

Kwenye uchimi Dongote na Bakhresa sio muhimu kama mikopo ya bank na tax kwenye ajira maana mwajiri mkubwa ni small business!!

Kwenye swala la mpangilio wa serikali: Serikali inakimbilia sana kuajiri wasomi lakini wasomi pamoja na akili zao hawatafanya vizuri kama hakuna process nzuri na sera nzuri za utekelezaji. sasa hivi kila waziri anaenda kwa mawazo yake ukali na kukataza lakini si kila msomi ni kiongozi mzuri hasa kwenye ideas hivyo serikali inatakiwa kuwa na process ya utekelezaji . Je wafanyeje toeni siasa na fanya hivi ajiri consulting company tena specific kushughulikia vitu vichache kama ifuatavyo (1) kutoa report ya kuongeza au kupunguza idara zisizo muhimu kwa serikali kiutendaji (2) Kutoa report ya technologia na kupunguza watu wasio muhimu kwenye serikali-watendaji. Leongo kuu ni kutoa plan ya kupunguza matumizi na kuongeza ufanisi serikalini. Lakini vilevile plan ya step by step ambayo itafuatwa na kila mtu ya utekelezaji wa hiyo process. Hii itasaidia kwamba ukiweka viongozi kwenye idara wanafuata process ya utendaji badala ya kutokuwa na process yeyote na kuwaachia mawaziri, makatibu ambao wengine hawana mbinu. vilevile itasaidia ku focus kwenye kutimiza malengo pamoja kama ilivyo kwenye kampuni kubwa. (3) Ajiri watu kutoka kwenye biashara/wafanyabiashara ambao wanaweza kubadilisha culture. Serikali imejaa wasomi ambao hawajui hata kuendesha duka ya nyanya leo unataka wawe ndiyo watendaji na kuamua maswala ya uchumi wakati hawajui hata shida moja ya tax za nchi wengi wao wamekuwa watumiaji wa tax kuliko walipaji. serikali inatakiwa kuajiri walipaji zaidi. (4) Kazi za serikali ziwe kwa muda tu acheni tabia ya kuajiri mfanyakazi kwa milele... ni lazima kuwe na mikataba badala ya kuweka utaratibu wa wananchi kuzoea kutegemea serikali milele...

mawazo mengine kwenye elimu, afya nilishatoa nita copy hapa
 
Hata cjakuelewa. Hebu kabla ya kuandika Fanya research kwanza hata kwa Ku Google hicho unachotaka kukiongelea kujua kwamba wenzio wamekizungumziaje au serikali inaplan gani juu ya hiko unachotaka kukizungumzia. Asante
 
Itakuchukua muda kunielewa maana tumepishana kiwango cha kuelewa na uzoefu. Wengine tuna bahati ya kuona Mengi na kufanya makubwa sana kwenye dunia hii fanya research yako vizuri badala ya ushabiki utaelewa. Mfano kama hujui Finance ni ngumu kukueleza bank kuu inawezaje kusaidia ajira.. je unajua kwanini mikopo ya biashara iko juu TZ, je unajua riba za nchi nyingine kwa sasa za biashara ni rate gani...take your time and study wewe ndiye unahitaji kujifunza hii ni level nyingine kidogo with all respect
 
post nyingine za miaka miwili au mitatu iliyopita:

Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.

Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo

1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%. Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.

Naona hii topic ni muhimu sana kuliko watu wanavyofikiria naomba nitoe some tena!

Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?

1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.

Nimesikia watu wengi kwenye mtandao wakipigia debe elimu ya bure!! tatizo la pesa kweli lipo lakini vilevile hatuna madarasa ya kisasa, walimu wa kutosha na mbinu mpya za ufundishaji.

Tanzania haitaweza kufanya yote haya niliyoyataja kwa Tanzania nzima kwani wananchi wa Tanzania wametapakaa sana nchini na si rahisi kujenga shule kila mahali zenye kila kitu. Sasa badala ya kupiga debe ya elimu bure ni lazima tujiulize je ungekuwa na budget hiyo ungefanya nini tofauti kufundisha watoto wote.

Kwa wenye uwezo wa kulipia shule hawana budi kulipa hakuna sababu ya msingi ya nchi masikini kama Tanzania watoto waliotokea kwenye familia zenye uwezo wasome bure lakini kwa wale wasio na uwezo nakubaliana na wengi kwenye hilo. Mimi nilishatoa mawazo hapa yafuatayo

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanao chukua mikopo na dhamana ya serikali ni lazima wafundishe miezi sita kabla ya kupewa vyeti vyao kama ilivyokuwa JKT. Hii itasaidia kupunguza gharama sana.
2. Kwenye ujenzi wa shule za Primary na Sekondari wakijenga wahusishe wenyeji. Hii itasadia wenyeji kuona ni part ya maendeleo yao na hii tabia wanafanya sana wachagga badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
3. Boarding School- Serikali ianzishe Boarding school kwa wilaya ambazo zina watu wachache hii itasaidia badala ya kuwa na shule nyingi kila mahali ni bora uwe na shule moja kubwa sehemu moja na watoto wa Primary na sekondari waweze kwenda.
4. Serikali isiruhusu shule zinazofelisha zifungwe au wabadilishe uongozi. Kama tatizo ni utamaduni wa jamii kama shule nyingi za Zanzibar wapeleke watoto shule za boarding.
5. Shele binafsi-Serikali ipige mahesabu ya gharama kwa mwanafunzi mmoja na iruhusu watu binafsi kujenga shule za kisasa na kuwapa hizo pesa shule zikifunguliwa kwa mwanafunzi. Kama zinafelisha zinafungwa
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Mkuu , natanguliza salamu , baada ya salamu naomba ruhusa yako kutumia uzi huu ili kutunga kitabu , ambacho natarajia kukisambaza mashuleni kitumike kufundishia , kama alivyofanya NYAMBARI NYANGWINE .

Natanguliza shukrani .
 
post nyingine za miaka miwili au mitatu iliyopita:

Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.

Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo

1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%. Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.

Naona hii topic ni muhimu sana kuliko watu wanavyofikiria naomba nitoe some tena!

Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?

1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.

Nimesikia watu wengi kwenye mtandao wakipigia debe elimu ya bure!! tatizo la pesa kweli lipo lakini vilevile hatuna madarasa ya kisasa, walimu wa kutosha na mbinu mpya za ufundishaji.

Tanzania haitaweza kufanya yote haya niliyoyataja kwa Tanzania nzima kwani wananchi wa Tanzania wametapakaa sana nchini na si rahisi kujenga shule kila mahali zenye kila kitu. Sasa badala ya kupiga debe ya elimu bure ni lazima tujiulize je ungekuwa na budget hiyo ungefanya nini tofauti kufundisha watoto wote.

Kwa wenye uwezo wa kulipia shule hawana budi kulipa hakuna sababu ya msingi ya nchi masikini kama Tanzania watoto waliotokea kwenye familia zenye uwezo wasome bure lakini kwa wale wasio na uwezo nakubaliana na wengi kwenye hilo. Mimi nilishatoa mawazo hapa yafuatayo

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanao chukua mikopo na dhamana ya serikali ni lazima wafundishe miezi sita kabla ya kupewa vyeti vyao kama ilivyokuwa JKT. Hii itasaidia kupunguza gharama sana.
2. Kwenye ujenzi wa shule za Primary na Sekondari wakijenga wahusishe wenyeji. Hii itasadia wenyeji kuona ni part ya maendeleo yao na hii tabia wanafanya sana wachagga badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
3. Boarding School- Serikali ianzishe Boarding school kwa wilaya ambazo zina watu wachache hii itasaidia badala ya kuwa na shule nyingi kila mahali ni bora uwe na shule moja kubwa sehemu moja na watoto wa Primary na sekondari waweze kwenda.
4. Serikali isiruhusu shule zinazofelisha zifungwe au wabadilishe uongozi. Kama tatizo ni utamaduni wa jamii kama shule nyingi za Zanzibar wapeleke watoto shule za boarding.
5. Shele binafsi-Serikali ipige mahesabu ya gharama kwa mwanafunzi mmoja na iruhusu watu binafsi kujenga shule za kisasa na kuwapa hizo pesa shule zikifunguliwa kwa mwanafunzi. Kama zinafelisha zinafungwa
Nikupongeze unamawazo mazuri sana mkuu ila tatizo moja tu unaweka hoja nyingi tofauti tofauti kwa wakati mmoja na kwa kuziunganisha badala ya kueleza hoja moja ikaeleweka. Asante jitahidi utakuja kuwa mwanasiasa mzuri.
 
webmaster ndiyo ameweka topic yangu hapa ilikuwa inajitegemea. Mimi sitakuwa kwenye siasa ni consultant kwenye healthcare na nime specialize kwenye kupunguza cost na kuongeza ufanisi kwenye hospitals
 
Wanajukwaa.
Habari za usiku,naweka mezani juu ya hoja yangu,kua je rais wa nchi yetu huyu wa awamu ya 5 je ni rais wa wanaCCM pekee au ni rais wa WATANZANIA wote?

Huyu ni baba wa familia asiejua alifanyalo au nini tatzo,anzia matamshi yake hayasadifu kutamkwa na mkuu wa nchi,mbaguzi na pengne hajui alitendalo,binafsi sikutarajia rais huyu kua hivi,naichukia October 25 km taifa tumebebeshwa mzigo wa tope.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom