Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Akili zetu watanzania ni '' shake well before'' yani nahisi we have a big problem in our mindsets kuliko tunavodhani. Alipita Mwinyi akasemwa alikua rais alieshikwa maskio na kupoteza thamani ya pesa sababu ya ''kila kitu ruksa'' kila mtu akawa na pesa hatimae ikapoteza thamani..Akaja Mkapa, akaambiwa yeye ndo kafilisisha viwanda vyote Tanzania. Akaja Kikwete yani hapo ndo sisemi, oh rais anaweka watu anaowajua, hana decision, analea mafisadi, oh tunahitaji rahisi mkali atakae simamia nchi..sasa Mungu akasikia maombi..akaja Tingatinga..he!

Mkali, hataki upuzi, kodi utalipa, hakuna uhuru to that extent mana tushazoea kutumia mindao hovyo, kazini utaenda mana hakuna dili tena, wafanyakazi hewa ondoa, watoto wanakaa chini hawana madawati, changia dawati kama unachangia harusi kwanini sio dawati, hakuna kusafiri hovyo, hiyo pesa kanunueni magodoro wamama wajawazito mwimbili wanalala chini,

wapeni magodoro, mikataba ya madini irudiwe tena, alie na uwezo wa kuinvest kwenye kiwanda aje mazingira yapo, jam zimezidi, tafuta wakandarasi by 2018 tz iwe na flyovers. Elimu bure, watoto wasome, walimu walipwe madai yao, maaskari walipwe madai yao, wazee walipwe madai yao,, mtaala wa elimu uangaliwe upya etc etc .na vitu viko kwenye progress....

lakini hata mika 3 haijapita..watanzania,, huyu rais dictator, taifa linapotea. Pesa zinakusanywa hazionekani..hivi unadhani hizo flyovers hao wakandarasi wanalipwa na pesa za misaada, au hayo madeni ya walimu etc yalilipwa na pesa za misaada? Watu wanataka walale waamke wakute tz iko marekani. We should take time kujifunza hayo mataifa yaliyoendelea how long did it took them to be where they are now!!!

And what did they go through... Kufunga mkanda lazima katika early stages..hao walioendelea tu wenyewe they workd day and night, taifa uchumi mzuri lakini people take hata 3 jobs na bado ni developed country. Sasa sembuse sisi. Tumeambiwa hapa kazi tu tung'aka... Sasa unataka ulale uamke ndo ukute maisha mazuri??

Do not ask what does the country do to you, ask what are you doing for the country!!!! Mwe! Mi sijui labda tunahitaji malaika. Mana nadhani tumekua wale wana wa israel, tutakaa jangwani miaka 40 mpaka akili zikae sawa.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Labda umepotea wewe na familia yako. Mlizoe Upigaji, Sasa Kila Kona Kumebana Mnalalamika, Na bado. Piga Kazi Rais JPM
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
WEWE NI MHAINI
 
Kama wahenga walivyosema Ngoma ikivuma sana hupasuka. Hiki ndicho tunachokishuhudia.

Pogba ni wewe ulikuwa unatoa kauli za kibabe na utumbuaji usiofuata sheria.

Ulifikia hatua ya kuzima mikutano ya kisiasa na uhuru wa bunge.
Umenyanyasa sana viongozi wa vyama vya upinzani.

Pogba tulikuacha ufanye yako, kwa jeuri ya Vyombo vyako vya dola ukatumia kunyanyasa watu.

Pogba ni wewe uliyekuwa ukitoa tamko na kutikisa nchi nzima. Chama chako kilikuonya hukusikia.

Pogba ile jeuri ya kuwakebehi waathirika wa tetemeko la ardhi kule Kagera na kutafuna pesa zao sasa inakutokea puani.

Hii ngoma mliyoicheza juzi wewe na kijana wako mwenye ushawishi kuliko Wadhili Mkuu sasa inakutokea puani.

Baraza zima la mawaziri limeshakuchoka, huna ushawishi tena.

Nchi imesha kuchoka, kila ukiongeacho hakipewi uzito, unaonekana una bwabwaja tu.

Umefikia hatua za kudharau bunge, kuiendesha mahakama unavyotaka wewe, sasa basi, mwisho umefika.

Zile amri zako na jeuri zako zimefikia mwisho, NGONA INAKARIBIA KUPASUKA, IKIPASUKA NI SHANGWE KWA TAIFA.

Pole sana Pogba, tambua kuwa "Action and reaction are equal, have the same frequency and rate.

Haramu ya uchaguzi Mkuu ndio inakutafuna.

Karma!!!
Dahh......siku zote dhambi ya dhulma itakubamba tu
 
Tusipokuwa wavumilivu tutatukana sana,tutakamatwa sana,tutafungwa mno.
Hizi kauli za sipangiwi cha kufanya,sijaribiwi zinachefua kiasi cha kulazimisha watu.kusema vibaya.

Kanuni za utumishi wa umma zimepindishwa,watumishi hawapandishwi mishahara,hawapandishwi vyeo,waliopandishwa hawarekebishiwi mishahara,uhakiki hewa hauishi,hakuna mrejesho wa uhakiki wa vyeti,vyama vya wafanyakazi vimeduwaa tu.

Maamuzi yamekuwa ya mtu mmoja,huyu mmoja atatibu wagonjwa hospitali zote,atafunfisha,atachunga wafungwa magerezani na kazi nyingine nyimgi.
Elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi darasani,hakuna ajira za walimu wapya,walimu waliopo wamelemewa,wamekata tamaa kwa haya mazingaombwe yasiyoisha.

Niwaombe wabunge katika vikao vya bunge linaloanza april wapaze sauti zao kutetea watumishi wa umma waachane na Makonda.

Tutakukumbuka sana Kikwete.
 
Bila shaka wanajamvi mko wazima, hii mada niliwai kuizungumzia mara mbili kupitia vituo vya redio mbali mbali .Mh.Rais wetu sio mtu wa kuamini katika maamuzi yake ambayo amekua akiyafanya ata kabla ajawa Rais wetu. Ukifuatilia madhara ya maamuzi yake bila shaka utaona ni jinsi gani anavyorigharim ili Taifa. Nitajaribu kulikumbusha Taifa ili huko nyuma huyu mtu amefanya nini

1. Akiwa waziri wa mifugo na uvuvi tunakumbuka hasara ya kukamatwa bila kufuata taratibu ile Meli ya Wachina

2. Akiwa ujenzi tunajua nini kilitokea kwenye Ujenzi wa bara bara mfano zilizo chini ya kiwango,utapeli kwenye fidia, n.a. upotevu wa pesa mfano 284million

3. Ununuzi wa meli/kivuko kilichotumika na kibovu Mv Dar Es Salaam

4. Akiwa waziri wa nyumba na ardhi bila shaka mengi mabovu yalitendeka wakati wizara ikiwa chini yake

5. Akiwa kama mbunge na waziri ameshiriki kama mwanaccm mwenzangu kupitisha sera na sheria mbovu kwenye madini tena kwa kusifia sana sasa leo eti amekuja na nyimbo mpya.

6. Lakini pia akiwa waziri na mbunge leo tena ni mkuu ameshiriki katika mambo ambayo yamefanywa na wanaccm mfano sakata la LUGUMI,Escrow,EPA nk
Sasa leo anafanya maamuzi kama haya huku tukijua huko nyuma alivyoligharim Taifa alafu bado watu wanakua n.a. imani n.a. huyu mtu.

Tusubiri tena hasara ndo labda tutatoka kwenye usingizi mzito
 
-POMBE ni kinywaji kinacholevya

-Toka lini POMBE ikaleta maendeleo kwa jamii?

-Lakini kuna wajinga kwa maksudi au kutojua wakaichagua POMBE eti ilete maendeleo.

-POMBE hulevya na kufanya vitu kwa sifa tena vya kipumbavu na kilofa(in BM's voice).

-POMBE imeacha majuto mtaani, kwani imekuwa kero kwa wengi hata ambao ambao "hawakuichagua" kuinywa.

-POMBE ina kawaida ya hunena manena maneno ya kipuuzi mithili ya mtu kichaa tena kwa KUKURUPUKA.

-nadhani ni busara tukaachana na POMBE ili tufanye maendeleo, kuacha pombe ni kazi ngumu, ila taratibu tu, kidogo kidogo hadi 2020 utakuta umeiacha na umeitoa moyoni mwako.

SIIPENDI POMBE NA NAWACHUKIA WOTE WALIOICHAGUA POMBE
 
Bila shaka wanajamvi mko wazima, hii mada niliwai kuizungumzia mara mbili kupitia vituo vya redio mbali mbali .Mh.Rais wetu sio mtu wa kuamini katika maamuzi yake ambayo amekua akiyafanya ata kabla ajawa Rais wetu. Ukifuatilia madhara ya maamuzi yake bila shaka utaona ni jinsi gani anavyorigharim ili Taifa. Nitajaribu kulikumbusha Taifa ili huko nyuma huyu mtu amefanya nini
1.Akiwa waziri wa mifugo na uvuvi tunakumbuka hasara ya kukamatwa bila kufuata taratibu ile Meli ya Wachina
2.Akiwa ujenzi tunajua nini kilitokea kwenye Ujenzi wa bara bara mfano zilizo chini ya kiwango,utapeli kwenye fidia, n.a. upotevu wa pesa mfano 284million
3.Ununuzi wa meli/kivuko kilichotumika na kibovu Mv Dar Es Salaam
4.Akiwa waziri wa nyumba na ardhi bila shaka mengi mabovu yalitendeka wakati wizara ikiwa chini yake
5.Akiwa kama mbunge na waziri ameshiriki kama mwanaccm mwenzangu kupitisha sera na sheria mbovu kwenye madini tena kwa kusifia sana sasa leo eti amekuja na nyimbo mpya.
6.Lakini pia akiwa waziri na mbunge leo tena ni mkuu ameshiriki katika mambo ambayo yamefanywa na wanaccm mfano sakata la LUGUMI,Escrow,EPA nk
Sasa leo anafanya maamuzi kama haya huku tukijua huko nyuma alivyoligharim Taifa alafu bado watu wanakua n.a. imani n.a. huyu mtu..
Tusubiri tena hasara ndo labda tutatoka kwenye usingizi mzito
Wewe ulitaka afanye maamzi gani? Aamue kuwa "Haya mbowe, Gwajima, Uzeni madawa ya kulevya hakuna shida"? Hayo ndiyo unayotaka?
 
Alafu akiwa kama Rais kuna Bashite, dah! hii imefunika yote ya nyuma.
 
Tatizo watanzania yale yanayoliokoa taifa ndo tunayaita yanaangamiza taifa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom