Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Sasa tunatoka koromije tunaelekea chato
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HtlMwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?
Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Kweli kabisa. Wa mjini wanaopewa ma T shirt Ndio wanaotuharibia maisha kila siku,wanachagua watu hovyo kabisaMnatumia nguvu kulalamika badala ya kuwaelimisha ndugu zenu vijijini,mana wao ndo mtaji wa chama chakavu
Hata sasa hivi niko huku vijijini najitolea kufanya kazi hiyo bila malipo.Mnatumia nguvu kulalamika badala ya kuwaelimisha ndugu zenu vijijini,mana wao ndo mtaji wa chama chakavu
Nakweli tena kwa kuanzia sasa hivi ndugu ,baba .mama unawakatia misaada .mpaka walalamike .wakiuliza kulikoni unawaambia mmechagua ccm .[emoji23] [emoji23] [emoji23]Mnatumia nguvu kulalamika badala ya kuwaelimisha ndugu zenu vijijini,mana wao ndo mtaji wa chama chakavu
[emoji106] [emoji106] [emoji106]Kwa kweli kuna umuhimu wa kuungana na yeyote yule aliye madhubuti na tayari kuwaondoa huyu mkoloni mweusi Tanzania.
Tukutane 2020 tukinia mamoja.
Together we can.
Wanunulieni ndugu zenu smartphone ziko mpaka za alfu 60,wawe wanaingia mitandaoni kutoa tongotongoNakweli tena kwa kuanzia sasa hivi ndugu ,baba .mama unawakatia misaada .mpaka walalamike .wakiuliza kulikoni unawaambia mmechagua ccm .[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kwa akili yako ndogo unadhani ccm haina watu?Huwezi kuitoa ccm madarakani kwa kukutana jamii forumsWengi tunaumizwa na serikali hii ya awamu ya tano. Tunakatishwa tamaa na serikali hii ya awamu ya tano. Tunapuuzwa. Tunaonewa. Tunadhalilishwa. Tunadhihakiwa. Ndugu zetu wanapotea. Ndugu zetu wanaumizwa. Ndugu zetu wananyanyaswa. Ndugu zetu wanatishwa. Hakuna wa kuwatetea. Hakuna anayejali.
Tupeanae faraja. Tujengane kisaikolojia. Tuungane kwa maumivu yetu. Tutafute majibu kwa pamoja. Tutafute adhabu inayostahili kwa serikali ya awamu ya tano.
Wafanyabiashara. Mama ntilie. Wafanyakaz/watumishi. Wakulima. Wafugaji. Wavuvi. Madereva. Wakandarasi. Vijana. Akina mama. Wazee. Wasomi. Wanaolala njaa. Tuungane, tuiadhibu CCM na serikali yake.
Hatuwezi kukombolewa na vyama vya upinzani. Hatuwezi kukombolewa na wazungu. Hatuwezi kukombolewa na Mbowe ,Maalim ,Lipumba wala Zitto. Hatuwezi kukombolewa na CHADEMA, CCM, CUF. Hatuwezi kukombolewa na Rais Magufuli.
Njia pekee ya kujikomboa ni kuungana. Ni kupambana na kila fikra hasi bila kujali imetolewa na nani. Njia pekee ni kuamua leo ni namna gani tuendeshwe sio wao watuamulie namna gani watuendeshe. Muda ni sasa. Tuchukue hatua. Tujikomboe.
Kila kundi tuna wajibu wa kujikomboa kwa kuweka tofauti zetu pembeni na kuungana.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa.