Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huwezi kuwa CCM alafu ukapinga yanayofanywa na mwenyekiti na chama kwa ujumla.kwani uozo na mauzauza yameanza na magufuli?.kuwapo kwenu madarakani kwa miaka takriban 50 ndiko kumetufikisha hapa tulipo.Falsafa nzima ya CCM imeegemea katika kubebana,unafiki na hadaa.kubebana kumekuwepo tangu kipindi cha nyerere ndio maana viwanda vingi vilivyoanzishwa kipindi kile vilikufa sababu ya kuwekwa makada wa chama wasio na elimu wala weledi.Ni unafiki kujinasibisha na haki ilhali uko kwenye chama kinachosifika kwa uminyaji wa haki.
Kwa hili nimeamini kweli huyu Bashite ana vyeti feki na wengi wapo kwenye huu utumishi wa umma wasio na sifa sitahiki wanalindana ila hakuna marefu yasio na mwisho sheria zipo wazi kiswahili chetu kiatupa uwezo wa kudadisi zaidi.
 
Narudia tena na ntasema tena.. Tanzania wapiga kura tunadharaulika sana hasa awamu hii
 
Huwezi kuwa CCM alafu ukapinga yanayofanywa na mwenyekiti na chama kwa ujumla.kwani uozo na mauzauza yameanza na magufuli?.kuwapo kwenu madarakani kwa miaka takriban 50 ndiko kumetufikisha hapa tulipo.Falsafa nzima ya CCM imeegemea katika kubebana,unafiki na hadaa.kubebana kumekuwepo tangu kipindi cha nyerere ndio maana viwanda vingi vilivyoanzishwa kipindi kile vilikufa sababu ya kuwekwa makada wa chama wasio na elimu wala weledi.Ni unafiki kujinasibisha na haki ilhali uko kwenye chama kinachosifika kwa uminyaji wa haki.
Sio kweli kuwa nikiwa ccm nakubaliana na kubalianana kila jambo.ndio mana nikasema kwa hili japo mim ni ccm sikubaliani nalo na wala si kosa kwa mwanaccm kutoa mawazo yake..
 
Watz mtakoma na serikali yenu si wengine tumejikataaa tupo bondeni huku tunatibu watswana endeleeni kusema hapa kazi tuuuu fyuuuu
nadhani umebeba ukoo wako wote upo uko ulipo, vinginevyo tunakoma wote mpaka ndugu zako kasoro wewe tu wa bondeni.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Kikawaida unapotea kama unajua unapoelekea. Kwa hali ilivyo sasa. Kwa kuwa hatujui tunapoelekea for sure hatujapotea na nnachoweza kusema tupo kwenye roli na roli linachanja buga kuelekea tusipokujua.
Labda umepotea wewe na familia yako. Mlizoe Upigaji, Sasa Kila Kona Kumebana Mnalalamika, Na bado. Piga Kazi Rais JPM

Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo tu.
 
Na kwa kuwa hata sisi wenyewe hatujui tunataka kwenda wapi, wacha tu lori liende linapoenda, labda huko mbeleni tutajua tunaenda wapi then tutaamua.
 
Eti sifa ya mteule wa Rais ni kusoma na kuandika kweli? Historia itamuhukumu Kairuki
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Kwa hotuba za Rais za hivi karibuni na kabisa za wiki hii nahisi kama tumefika mahala pameandikwa "Hakuna Njia" na hatuna maarifa mengine!🙁😵😱
 
Magufuli anatupeleka kule tulikotakiwa kwenda au kuwepo miaka mingi iliyopita. Kutokana na vitendo vya ufisadi tumechelewa mpaka sasa tupo hapa tulipo.
Kwa anatutoa hapa tulipo na kutupeleka mbele kimaendeleo.
 
KWA sababu we mwenyewe hujui maisha yako utatoka vipi ndivyo hivyo hivyo magu anataka watu mjue mnatoka vipi labda nikufundishe njia bora ya kujua jukumu lako kama mwananchi selikari yoyote duniani husimamia usalam,amani na kuelekeza selikari njinsi ya kufanya ili maisha ya wananchi yaendelee kwahiyo kama unasubili magu akusaidie kutoka zero to higher ni ngumu sana HAKUNA raisi anayependwa duniani kama magu angalia aljazera world asubuhi wameonyesha.
 
Sio kweli kuwa nikiwa ccm nakubaliana na kubalianana kila jambo.ndio mana nikasema kwa hili japo mim ni ccm sikubaliani nalo na wala si kosa kwa mwanaccm kutoa mawazo yake..
Hahah mkuu bwana sasa unawezaje kuwa kwenye chama cha wakulima then ukawa huna interest na kilimo,ama chama cha kutetea haki za mashoga then ukawa huusapoti ushoga.Hivi unafahamu maana ya chama kweli mkuu?
 
Ni wasiwasi wako tu; umepofuliwa na chuki za kushindwa ya kura nyingi za Watanzania kukataa ukabila na ukanda. Huoni wafanyakazi hewa kufutwa? Na wanafunzi hewa? Na miradi hewa? Na madawa ya kulevya? Na ufisadi? Na uzembe? Huoni Shirika la Ndege kufufuka sisi Taifa kubwa pande hii ya dunia hatuna airline? Huoni treni za standard gauge? Huoni bomba la mafuta kupitia Tanga? Umeme Vijijini huuoni, siku hizi unaenda hadi Rorya na Tandahimba na Nzega, huko zamani ilikuwa ni migombani tu. Huoni shule ziko nchi nzima, si Kaskazini tu? Huoni uchumi kukua, huoni inflation kupungua? Toa mawani meusi ya ukabila na udini na ukanda, utaona tunaenda wapi. WM.
Unaupeo mdogo wakufikiri yani umezidiwa hata na kuku
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom