Zaidi ya miaka 2 sasa mambo ya msingi na ya haki kwa watu wanyonge yamesimama huku wengine wakiendelea kutumbua nchi kama kawaida
- Mshahara wa mwalimu 300,000 increment ananyimwa kibabe huku wengine wakilipana posho ya siku tu 400,000
- Ajira kwa vijana zimekuwa za tochi, tena zinatolewa kwa kuviziana na kukomeshana, vijana hawana tumaini
- Si vijana, kinamama, wala yoyote aliye salama sasa maana hata kidogo chako kinaweza kuchukuliwa
- Upinzani nako kila mtu anajitahidi kujenga uchumi wake binafsi, ndugu zake, familia yake na watu wake.
Mimi ni nani, sina ndugu wala baba mbunge wala kiongozi wa chama cha siasa, wala mtu wa kabila langu atakayenibeba hata kwenye interview ya kampuni ya ulinzi licha ya kuwa ninazo sifa zote
Dunia dunia dunia dunia
Anayesononeka,
MoseKing