Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hebu sema mkuu, wewe binafsi JPM kafanya decision gani mbaya ambayo imeletelea kuharibu maisha yako?Kwa upande wangu mimi, mzunguuko mdogo wa fedha umeniathiri,lakini nimefurahishwa sana na uboreshaji wa miundombinu,kudhibiti wizi wa mali zetu za asili;kupiga vita ufisadi,wizi wa mali za uma,matumizi ya vyeti fake,uzembe sehemu za kazi,rushwa,ukwepaji kodi,matumizi na uuzwaji wa madawa ya kulevya na kuongeza uwajibikaji sehemu za kazi.

Hata hivyo harakati hizo ambazo nimezitaja kwa kiasi kikubwa naamini ndizo zilizofanya mzunguuko wa hela uwe mdogo.Kwa sababu hiyo sichukii, kwa kuwa nia ni njema kwetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Unauliza swali halafu unajijibu, hivi nyie watu mnatumia kichwa gani kuwaza, hivi Magu kamaliza rushwa ipi? Uwajibikaji upi sehemu za kazi maeneo mengi bado yapo vilevile nenda polisi, nenda mahakamani uone kama kuna mabadiliko, madawa hospitali hakuna, mnasifia kana kwamba nyie tu ndio mnaishi Tanzania.
 
Acha ujinga,hujui kuwa maamuzi mabovu ya kiongozi,na kutofuata sera pamoja na ukiukwaji wa katiba ndio umaskini wa mtu?

Acha mahaba kwa huyo kiazi wenu.
Chonde chonde utaitwa mchochezi. Jaribu kumuita mtetezi wa wanyonge. Japo napata wakati mgumu kujua wanyonge anaowataja ni watu wa aina gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha hayajirudii Mara mbili tunahitaji kupiga hatua, tunataka maamuzi yenye tija kwa nchi sio maamuzi yenye hasara kila kukicha.

Magufuli wewe ni mkuu wa nchi, tumekupa kila kitu ili uwe dereva wa nchi yetu.

Sasa kwanini unakosea kila maamuzi unayofanya? Ni kweli watanzania tulikosea kukuchagua?

Magufuli kuwa fisadi sio kuiba Mali ya umma tu hata kulitia Taifa hasara kutokana na maamuzi ya hasira na yasiyofuata sheria ni ufisadi.


Tulikuamini, tukasema Tanzania imepata Nyerere mpya lakini imekuwa tofauti.

Tupo njia panda mkuu Magu hatujui jahazi laenda kus au kas.

Tuliza kichwa Fanya maamuzi sahihi usituharibie nchi.

We live once, miaka mitano au kumi inatosha kabisa kuharibu maisha ya watu kutokana na Sera zako.

This is a wake up call

02 : 35
Sep.05.2017

Usiku mwema

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?

Kwa kweli natambua 'Concern' yako. Unayo nia njema lakn kama wengi wetu una wasiwasi na hali ya mambo yanavyokwenda. Umekatiza usingizi na kutoa dukuduku. Ni wachache sana wanaweza kutii dhamira zao kama ulivyofanya.
BARIKIWA SANA
 
Hii ni sawa tu na watoto kumlalamikia baba au mama yao kuwa ni mnoko anawapa wakati mgumu. Sawa, kwa uelewa wao mdogo wanakuwa sahihi, lakini kwa aliyepevuka kiakili atagundua kuwa wakifanyacho wazazi kwa watoto ni sahihi. Mwisho wa siku hao hao watoto, wakishafikia umri wa utu uzima, watajirudi na kuanza kuwasifia wazazi wao kwa kuwapa malezi safi kabisa yaliyowajenga kimaadili.
Hakuna mzazi mwenye nia mbaya na makuzi ya mwanae. Vilevile mzazi akifuata maelekezo au malalamiko ya watoto kuhusu malezi kwa hakika ataharibu tu mfumo mzima wa malezi bora.

Ni kujitoa akili kufikiri kwamba Rais wa nchi ndo anajua kila kitu na wengine wote wanatakiwa kufuata bila kuhoji au kukosoa. NI KUKOSA AKILI NA UFAHAMU WA MASUALA
 
.
Wengi wanaamini maisha bora yanakuja pasi kufanya kazi. Unakuta vijana wanashinda kijiwani halafu ndio wanaongoza kwa kuilalamikia serikali. Wangine wanataka kuishi maisha ya ghali kuliko vipato vyao, na ndio hao walalamikaji wa kila kukicha. badala ya kufikiri kuongeza kipato chao fikira zao zimelenga kukosoa tu kila kifanywacho na mamlaka.
Kwahiyo watanzania hawafanyi kazi? Wewe na huyo rais wako ndio unawalisha? Acheni kukaririshwa maneno na wanasiasa, kuna watu wanafanya kazi tena kwa kujituma sana lakini ndio hivyo mfumo wa maisha ni mbaya wanaishia kuwa masikini.
 
Maisha hayajirudii Mara mbili tunahitaji kupiga hatua, tunataka maamuzi yenye tija kwa nchi sio maamuzi yenye hasara kila kukicha.

Magufuli wewe ni mkuu wa nchi, tumekupa kila kitu ili uwe dereva wa nchi yetu.

Sasa kwanini unakosea kila maamuzi unayofanya? Ni kweli watanzania tulikosea kukuchagua?

Magufuli kuwa fisadi sio kuiba Mali ya umma tu hata kulitia Taifa hasara kutokana na maamuzi ya hasira na yasiyofuata sheria ni ufisadi.


Tulikuamini, tukasema Tanzania imepata Nyerere mpya lakini imekuwa tofauti.

Tupo njia panda mkuu Magu hatujui jahazi laenda kus au kas.

Tuliza kichwa Fanya maamuzi sahihi usituharibie nchi.

We live once, miaka mitano au kumi inatosha kabisa kuharibu maisha ya watu kutokana na Sera zako.

This is a wake up call

02 : 35
Sep.05.2017

Usiku mwema

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?

Jamani hata Israeli walipotolewa Misri walisafiri miaka 40 kabla ya kufika kwenye nchi iliyojaa maziwa, na asali. Walipokuwa njiani wengine walimlaumu Musa sana kwa kuwatoa Misri ambako hata hivyo walikuwa utumwani. Ningesema watakaofaidi makundi ya juhudi za sasa za uongozi wa serikali hii ya awamu ya tano ni wale walio watoto na vijana wadogo sasa. Dominica Republic ina hali nzuri angalau kuliko baadhi ya jirani zake kwa sababu ya juhudi za Rafael Trujillo, Rais wao miaka ya sitini. Singapore imefika hapo kutokana Na maongozi thabiti ya Lee Kuan Yew miaka ya sabini.
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.

Kinachowasumbua ni selfishness mpo tayar kutetea amewapa mavyeo yenye mshahara mnono tu.

Ndivyo miafrika tulivyo,umeona wapi harakat za mapinduzi zimefanywa na watu wanaoenjoy national cake???Hata IDD Amin alikua na watu km ww
 
Nilitegemea kuona sehem alipokosea sana hadi ukaamua kuandika uzi huu... Usiwe kama asilimia kubwa ya waandishi wa tanzania kuchukua habari kwenye mitandao na kuandika bila uchunguzi wa kina. Toa ufafanuzi wapi amekosea sana ili ajue ajirekebishe wapi mana kila mtu hukosea...

Sent using Jamii Forums mobile app
- Ajira hakuna mwaka wa tatu sasa ( Wao wanateuana kula kila leo )
- Mikopo vyuoni kupata kwa tochi
- Increments hakuna ( Wengine wanalipana posho ya laki 4 kwa siku )
- Machinga, Bodaboda na Waosha Magari wanasulubiwa kila leo
- JKT nafasi hazitoki, Jeshini vyeo havipandi
- Mbaazi kwa sasa hata 100 kwa kilo hazinunuliwi
- Pesa zote anataka ale yeye, kundi lake na kulipa wazungu anaowatia hasara

Na Ndo mwaka wa pili sasa na Ndoto za vijana zinakufa kwa KASI !
 
This absolutely non sense,gari limepoteza mwelekeo linayumba alafu unawambia abiria vumilie tu itafka.Unatoa huu ushuzi kwa sababu amekushibisha, kwa hali ya kawaida huwezi kumtetea mtu huyo kama sio jamii yake,hii haiwezekani ni common sense tu
 
.
Mkuu, tafadhali ainisha hapa hayo maisha mabaya wanayoishi watu. Pia tuwekee hapa ni kwa namna gani kiongozi anawatesa watu.

ANGALIA HAPA:

1. Watu wanabomolewa nyumba zao bila fidia yyte huku wakiwa na vibali halali vya ujenzi mikononi mwao na hata zuio la mahakama linadharauliwa

2. Kodi za ajabu ajabu katika Biashara ndogo ndogo. Kiduka cha mtaani tulichokuwa tunalipa sh elf70 sasa hivi tunatakiwa kulipa taki 3, nikishindwa kupata hiza lak3 unaniambia funga acha biashara..?? Kweli???? Nina watoto

3. Ninatakiwa kufanya siasa ndo kula yangu, unapiga marufuku siasa, ninaishi jee?? Hii ni kazi yangu. Kwa nini uniweke mahabusu kwa kuhudhuria mkutano wa kisiasa jimbo la jirani yangu?? Hiyo ni kazi yangu. Nimekosa wapi kwa sheria zetu??

4.Nimekosaoa Serikali kwa kutoa maoni yangu, kwa nini nikamatwe na vyombo vya dola?? Kukosoa ni dhambi?? Kwa nini nikae mahabusu
 
Hivi wengi naona munapingana na mtoa mada na kumuambia kua sjui anataka rais agawe pesa kwa wananchi , sjui mara life style , sjui watu wanaishi maisha nje na uwezo wao

Hivi nyinyi wote mnao ongea hivi munaishi tz kwel ??
Nina mashaka sna kua wote mnaongea mkiwa out of tz

Mtoa mada kazungumzia kuhusu maamuz mambov ya hasira anayochkua kiongoz ambayo mwisho yanatugharimu kama taifa

Hivi ww nchi ikiingia hasara unajua nn kinafata ?? Kodi zitaongezwa yaan utakamuliwa ww raia to to infinity ili serikal ilipe maden hata km ulikua na biashara zko bas somehow zitayumba hadi unakuja ku adapt isha take time ,

Hivi unajua ni wawekezaj wangap ambao wameondoka tz baada ya hii hali ya hapa kuwa moto ajira za watu weng sna zimetoweka , na opportunity ngap za ajira kwa vijana zimekua hazipo tena ktk awamu ya sasa

Je hivi si kutufanya tuwe maskini ?

In short we live once , maguful acha kuharibu future zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.
Ati nini? hakuna raisi anaegawa pesa ? Mbona hata vyombo vya habari hurushwa wkt ngawira zikigawiwa ? na hawasemi ni msaada.
 
kwa hiyo mifano yako uliyotoa hapo sijaribu kuamini kama umefika hata kidato cha nne na kupata walau divisheni 4 ya 31.

Sent using Jamii Forums mobile app


Kwani kuna sehemu nimesema nimefika hata hiyo secondary? Mbona mnapenda kutunyanyapaa ambao hatujasoma? Inamaana tanzania wanaostahili kutoa maoni au mawazo ni waliosoma tuu? Acha ubaguzi, tanzania ni yetu sote regardless kiwango cha elimu, na yawezekana wewe hata kuandika umejifunzia kwenye smartphone
 
Raisi au kiongozi wa nchi akifuata hayo maneno ya mtaani ya we only live once,sijui maisha ni mafupi,tumia ela ikuzoee,ponda mali kufa kwaja..... etc,nchi itageuka kichaka cha walanguzi.Huo waweza kuwa ukweli lakini usiotakiwa kutiiliwa maanani hata dakika moja na kiongozi yoyote.

Acha kuwa na mawazo ya kifukara kiasi hicho wewe, kwanini uko hopeless kiasi hiki?
 
.
Mkuu, tafadhali ainisha hapa hayo maisha mabaya wanayoishi watu. Pia tuwekee hapa ni kwa namna gani kiongozi anawatesa watu.

Pia kumbuka hakuna mtu aliyekatazwa kuwa tajiri. Ufukara wa watu ni kutokana na lifestyle yao mkuu, hakuna kiongozi atakuja awe anagawa pesa kwa watu ili kuwakwamua kiuchumi. Kama mnategemea hicho sahauni, hata mitume wakishuka hawataweza kuwaridhisha.

Mara nyingine watu kama nyie ndio mnapalilia umaskini hapa nchini kwa kuamini na kuhubiri kuwa umaskini unasababishwa na serikali. Tumieni raslimali na nguvu zenu kujikwamua, msingoje serikali iwawekee mabomba ya maziwa na asali.
Hivi kwani na wewe ni mgeni wa nchi hii!?
 
Kuwa na double standard pia ni ufisadi,kuajiri watoto wa ndugu katika nafasi muhim kwa upendeleo ni ufisadi,kutumia pesa za serikali bila kufuata utaratibu ni ufisadi.,kuikanyaga katiba ni ufisadi uliopindukia.wewe ufai kuwa kiongoz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom