Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hebu sema mkuu, wewe binafsi JPM kafanya decision gani mbaya ambayo imeletelea kuharibu maisha yako?Kwa upande wangu mimi, mzunguuko mdogo wa fedha umeniathiri,lakini nimefurahishwa sana na uboreshaji wa miundombinu,kudhibiti wizi wa mali zetu za asili;kupiga vita ufisadi,wizi wa mali za uma,matumizi ya vyeti fake,uzembe sehemu za kazi,rushwa,ukwepaji kodi,matumizi na uuzwaji wa madawa ya kulevya na kuongeza uwajibikaji sehemu za kazi.

Hata hivyo harakati hizo ambazo nimezitaja kwa kiasi kikubwa, naamini ndizo zilizofanya mzunguuko wa hela uwe mdogo.Kwa sababu hiyo sichukii, kwa kuwa najua nia ni njema kwetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.Najua kwamba kila jambo lina "pro and cons."
Mkuu nimesema kulitia Taifa hasara kwa maamuz yake ya gafla unaweza uone ni kitu kidogo lakin kina athari kubwa sana kwenye uchumi wa nchi ni sawa na kuwa fisadi tu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Hiyo takwimu ya kila mtu ananalamika umeitoa wapi? Labda kama ya mtaani unakoishi ndio wanalalamika pasi kujua tatizo wanalo wao.

Takwimu kaitoa JF. Huku ndipo anashinda akilalamika kila kukicha. Ameshakuita hopeless sijui kati ya wewe na yeye nani ni hopeless tupa kule anayelalamika humu. ...eti kuonyesha hisia? ?

Mwache aendelee kuonyesha hisia atakapo shtuka Magu anaondoka ye ye uzee ushamvaa!

Usipate shida kujibishana naye. Yeye ni kati ya wale -waliotumbuliwa au waliokuwa wanawaweka mjini kutumbuliwa

-waliozibiwa mianya ya madili

-waliopunguziwa mishahara

-waliozibiwa safari za nje na posho. In fact wamechanganyikiwa ni watu was kuwaonea huruma. Kwanza mavivu halafu Wanachuki matusi kejeli. Mimi wala hawanitishi wala siwezi kuwajibu au kubishana nao wasije niondolea mood yangu nzuri bure
 
Jamani hata Israeli walipotolewa Misri walisafiri miaka 40 kabla ya kufika kwenye nchi iliyojaa maziwa, na asali. Walipokuwa njiani wengine walimlaumu Musa sana kwa kuwatoa Misri ambako hata hivyo walikuwa utumwani. Ningesema watakaofaidi makundi ya juhudi za sasa za uongozi wa serikali hii ya awamu ya tano ni wale walio watoto na vijana wadogo sasa. Dominica Republic ina hali nzuri angalau kuliko baadhi ya jirani zake kwa sababu ya juhudi za Rafael Trujillo, Rais wao miaka ya sitini. Singapore imefika hapo kutokana Na maongozi thabiti ya Lee Kuan Yew miaka ya sabini.
Mkuu kwa maamuzi yake sidhani km kuna kitu kipya tutagain labda abadilike

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Sisi soteni wapitaji hapa duniani...kiburi cha mtu na damu ya utakayewaua itabaki ikilia
 
You people are hopelesses of the kind! Hivi mtu akiwa kiongozi anapaswa kufanya maisha ya watu yawe mazuri au aharibu? Kwani hakuna njia bora zaidi ya kuwatesa watu? Kwa mawazo yenu ni kwamba ili aonekane yu sahihi ni lazima watu wawe fukara? Hizo akili makinikia huwa mnagawiwa wapi wakati wengine wanazo zenye fikra yakinifu? Kwendeni zenu huko!!

Sasa wewe JPM kakutesaje. Bundle lako la hapa badala ya kusave ufanye shughuli. Unamsingizia JPM.

Wengine wanahonga laki tatu kwa wiki. Ila Maendeleo tu akupe JPM. Wajibu wa Rais ni kusaidiana na System kuweka mazingira ya wewe kuishi kwa amani.

Kupata Muda kama huu wa kuropoka hapa kila siku bila tija bila mtutu wa bunduki nk nk. Mengine ni yetu. Wewe
 
Kwani kuna sehemu nimesema nimefika hata hiyo secondary? Mbona mnapenda kutunyanyapaa ambao hatujasoma? Inamaana tanzania wanaostahili kutoa maoni au mawazo ni waliosoma tuu? Acha ubaguzi, tanzania ni yetu sote regardless kiwango cha elimu, na yawezekana wewe hata kuandika umejifunzia kwenye smartphone
Uyo kashiba hamkumbuki mwenye njaa

Alafu elimu ya bongo ni vyeti tu asikutishe

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Mimi kipato changu kwa muda sasa ni Tsh 1.5m kwa mwezi. Unga niliokua nanunu kwa tsh. 11,000 sasahivi ni tsh. 8,000. Gas ya tsh. 52,000 sasa hivi ni 42,000. Toka tegeta hadi kivukoni ni tsh 600 badala ya 1400. Nimmpeleka mgonjwa wangu muhimbili, tumepokelewa vizuri alilazwa kwa wiki moja na kufanyiwa operation ya jicho na tulichangia tsh. 120,000 tu, tena kwenye wodi safi na madaktari na manesi wanao nyenyekea wagonjwa. Binafsi naipongeza sana sana serikali ya JPM kwa sababu imenipunguzia makali ya maisha. Ila mimi ni mfanyakazi na nafanya kazi kwa bidii na kazi yangu ainaga magendo.
Hongera mkuu km kweli

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Huu ni ushauri mzuri kabisa

Bila hata nchi kugawanywa kwenye zone kwa wakati huu angeweza kutumia hata wati wanaomzunguka ana washauri,mawaziri, makam rais, majasusi ya kiuchumi nk

Nchi ingeweza kuwa stable tu kuliko saiv tunapiga maktaim

Mh asiamin katika kile kilichopo kichwani mwake tu kuna watu very intelgence and patriotic awatumie

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?

Mkuu zones ni muhimu,

kutatoa balance katika sehemu mbali mbali,

itatoa manung'uniko kwa nini watu wa Chato wanapendelewa,
 
Umeshindwa kujua wajibu wako kama binadamu , unataka kuanza kuhamishia wenzako matatizo yako. Timiza wajibu wako kwanza.
 
You people are hopelesses of the kind! Hivi mtu akiwa kiongozi anapaswa kufanya maisha ya watu yawe mazuri au aharibu? Kwani hakuna njia bora zaidi ya kuwatesa watu? Kwa mawazo yenu ni kwamba ili aonekane yu sahihi ni lazima watu wawe fukara? Hizo akili makinikia huwa mnagawiwa wapi wakati wengine wanazo zenye fikra yakinifu? Kwendeni zenu huko!!
Wa kuharibu au kutengeneza maisha yako ni wewe acha kuhamisha goli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You people are hopelesses of the kind! Hivi mtu akiwa kiongozi anapaswa kufanya maisha ya watu yawe mazuri au aharibu? Kwani hakuna njia bora zaidi ya kuwatesa watu? Kwa mawazo yenu ni kwamba ili aonekane yu sahihi ni lazima watu wawe fukara? Hizo akili makinikia huwa mnagawiwa wapi wakati wengine wanazo zenye fikra yakinifu? Kwendeni zenu huko!!


Pambana na hali yako ndugu, acha kulialia
 
Anafuata falsafa ya maandiko matakatifu, mbegu nzuri huoza kwanza ndipo humea. Labda ameamua kuharibu kwanza ili vimee umpya! Sasa visipoota sijui tutafanyaje!!!
 
Sasa wewe JPM kakutesaje.
Nimesoma kanibania ajira, Nimekuwa machinga polisi wake wanavurumisha kama jambazi kila siku.
Bundle lako la hapa badala ya kusave ufanye shughuli.
Mtu anaekula kwa shida, atapata wapi pesa ya bundle. Anatumia www.freebasics.com
Unamsingizia JPM.
Hakuna anayemsingizia, yeye ndie anaeua ndoto za vijana wa taifa hili.
- Usajili wa makampuni na trademarks gharama kubwa
- Machinga unapigwa na polisi
- Watumishi hawapati hata increment yeye watu wake wanalipana LAKI 4 per day
- Kakwamisha ajira, vyeo na nafasi mpaka jeshini

.Ila Maendeleo tu akupe JPM. Wajibu wa Rais ni kusaidiana na System kuweka mazingira ya wewe kuishi kwa amani.
Hayo mazingira yako wapi wakati MALIPO ya PAYPAL yamewashinda
mijitu na PhD zao wakati Kenya ipo. In short anaua NDOTO za vijana wa Taifa hili kwa KASI Kubwa sana
 
Usi
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.

Usituchonganishe raia na Rais, alitwambia Nchi hii siyo masikini kwani tuliibiwa sana, na waliotuibia watazitoa kupitia tundu lolote...ashakum! Tunasubiri Noah, mimi nimesha tengeneza na parking chini ya muti nasubiri ikija tu, hakuna kuombana lift!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom