Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kujiajiri ni kufanyaje ?

- Maana kuna waliojiajiri kama machinga ila kila wakati wanapigwa na polisi na kuna waliojiajiri kama Bodaboda na wanachukuliwa kama majambazi vilevile!
Unapojiajiri mkuu zingatia kufuata kanuni za nchi ingawa zinaumiza. Unadhani kwa mfano ni fair kulipa kodi? Lakini tunalipa tu ili kupunguza matatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Be your own leader amigo,usiwekeze sana kwa hao watu huwa ni waongo kuliko shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni pale unapokuwa YOUR OWN LEADER halafu unaletewa watu wanakupiga NGWALA ( Kupigwa na machinga, kukamatiwa bodaboda yako, kukadiriwa kodi kubwa, kupandishiwa RIBA YA MKOPO, Kubomolewa nyumba, kufungiwa ofisi na TRA, TFDA, NEMC, OSHA, Kunyimwa kibali cha kusafiri, Kukataliwa mazao yako kuyauza sehemu fulani, Kudhulumiwa na fedha na NFRA nk )
 
ACt ya zitto inaweza kuyafanya haya

Si hao watafuta kiki na wachumia tumbo
 
Tunaelekea zimbwabwe, kama mbunge tu anashambuliwa kwa mtutu je sie pangu pakavu?tz si sehemu salama ya kuishi
 
Wana jf kuna swali ambalo Rais Magufuli huwa anatuuliza watanzania kila wakati kuhusu nani aliyeturoga na kusababisha watanzania tusiwe na uchungu na mali zetu hata zinapoporwa mchana kweupe. Sijasikia watu wakimpa majibu Rais wao kuhusu "Nani ameturoga" Je, wewe unalo jibu la kumpa Rais Magufuli kuhusu hili swali lake?

Nijuavyo mimi mtindo huu wa kutothamini mali zetu za taifa ulianziaga kipindi cha Ujamaa na Mashirika ya umma (SU) wakati wa Mwl. Nyerere. Kipindi kile watu walikuwa hawathamini mali ya umma hata kidogo wakidhani kuwa ilikuwa ni mali isiyokuwa na mwenyewe hadi wakatoa tafsiri ya "SU" ni Soma Ule. Mali za mashirika kama RTC, NMC, UDA, kaMAta, NAFCO na bodi za mazao kama KNCU n.k zilikuwa zinaliwa na wasomi wachache waliopewa dhamana za kuyaongoza. Na wananchi hatukuwa na uchungu nayo hata pale tulipokuwa tunawaona waliopewa dhamana za kuyaongoza wakiyafuja, maana tulikuwa tunadhani wanafuja mali isiyokuwa ya kwetu bali mali ya "umma". Hakujua wala kuwahi kuambiwa kuwa umma ni sisi na sisi ni umma.

Hatukuwahi kuambiwa kuwa elimu, afya, barabara, maji, umeme na huduma nyingine ambazo tulikuwa tukipatiwa bure zilikuwa zikitokana na mali hizo zilizokuwa zinafujwa na watanzania wenzetu waliokuwa wakiziiba na kuzitumia kwa manufaa yao, badala yake tulikuwa tukiwasifu na kuwaona kama watu "waliopata kazi nzuri". Hivyo kila mzazi alitamani mwanawe asome ili aajiliwe kwenye mashirika hayo ya umma (SU) kwakuwa wataleta nyumbani kwa wingi hela, sukari, unga, mifugo, bia, nguo, sabuni na bidhaa zilizokuwa zikizalishwa na SU hizo. Hatukujua kuwa kumbe mashirikia yale yalikuwa pia ni yetu hivyo walikuwa wakituibia sisi.

Dhana hiyo ya mali ya umma ilichagizwa pia na kitendo cha serikali kuzitumia mali zetu hizo (umma) na kuzitumia kwa harakati za ukombozi wa bara la Afrika bila idhini yetu yetu umma. Hivyo hadi leo umma hauna habari kuhusu ni mali ya umma kiasi gani tuliitumia katika zoezi zima kulikomboa bara la Afrika na itarejeshwaje au umma utafaidikaje za kwa kuzikomboa nchi nyingine. Watawala wetu waliitumia mali ya umma kama mali yao ya mfukoni bila kutushirikisha kikamilifu katika matumizi yake. Walikuwa wanafanya kwa niaba yetu, hivyo ikawa sawa na kumfunika blanket mtu anaejisikia joto na kumfunika shuka mtu anayejisikia baridi kali.

Hivi ndivyo vilivyoutafuna uzalendo wa wananchi wetu kwa mtizamo wangu.
 
Kuna maswali huwa najiuliza ila bado majibu hayajafika kwenye halmashauri ya ubongo wangu.

1. Kwenye huu utawala mnyama mwenye jina la mt Yohana amepewa thamani kubwa kuliko binadamu mwenye jina la muda (WAS NANE). Hakuna kosa kubwa binadamu anaweza kulifanya kama kutokuthamini muda naye Magufuli amelifanya je atapona???

2. Ni katika utawala huu wananchi masikini wameanza kulia Kwa viitikio tofautitofauti wakililia njaa na ugumu wa Maisha ambapo Kwa tawala zilizopita ugumu wa Maisha ulikua unatokea kipindi cha majanga tu mfano ukame au mafuriko. Najiuliza 2020 huyu bwana atapona???

3. Elimu ambayo Kwa karine hii ndo ufunguo wa maisha Kwa utawala huu imekua kinyume chake, wao elimu Ni mtu kuweza kuingia darasani na kurudi nyumbani huku akiwa hana tofauti ya kabla na baada ya kuingia darasani......Mikopo ya elimu ya juu nalo Ni bomu ambalo najiluliza je! 2020 litamuacha huyu bwana kileo salama???

4. Huyu bwana ana jipiga kifua akiamini kwamba 2020 hata asipopiga kampeni atashinda! Je, Paulo zake za mzalendo Ni yule anayemshambulia msaliti hata ikiwezekana kumuua, au Ile ya watoe waropokaji wakija mtaani nitawashughulikia kisawasawa..... hajui zinawaumiza wananchi wenye imani na hao anaowatafsiri kama waropokaji????

Watu wametekwa awamu ya tano, watu wametishwa awamu ya tano, Ma DC na Ma RC watukutu wametokea awamu ya tano, mtu anamiminiwa risasi 35 mbele ya makazi ya serikali na watu wasiojulikana hii imetokea awamu ya tano pekee. Je bado anajipiga kifua akidhani 2020 Ni nyepesi???

5. Wananchi wameinua mabango kumweleza shida zao anawaambia katindikieni mlale na wake zenu hivi 2020 anadani watakua wamesahau????

6. Kuna binadamu anaitwa Jerry Muro naye anasaka u DC Kwa kutoa kejeli na kashfa Kwa wakosoaji wa Mkulu, na muuliza je hao wanaokosoa wanadanganya????? Na je amesahau ndo walimpigania alipokua korokoroni???? 2020 naitazama kama chungu cha moto kichwani Kwa mtu....mnaonizidi upeo semeni mnaionaje.

[HASHTAG]#Tuiombee[/HASHTAG] Tanzania#
 
- Umefanya maisha yamekuwa magumu kupindukia
- Watanzania wameamua tu kukaa kimya na kupambana tu na maisha yao
- Umewakaba kila kona hawapumui bado huridhiki, ukiongea tu inabidi mtu atafute panadol ameze
- Tushakubali kwamba tumepoteza, tunavumilia tunajua yatapita lakini bado huridhiki unawarushia vijembe kwanini lakini ?

............
........
- Wamewekewa mchakato mzito na wa gharama kubwa kupata mikopo ya elimu ya juu. Wametulia
- Waliohitimu vyuo umezuia wasipate kazi, Wametulia
- Wakulima wa mbaazi wanatafuta mnunuzi hata wa kg 1 kwa Tsh 200 hawapati, wametulia
- Wafanyabiashara wanapelekewa mikodi ya ajabu, wengine wanafungwa. Wametulia
- Machinga wanapigwa na polisi. Wametulia
- Watumishi wanajuta na kuminywa haki zao. Wanasoma tu magazetini kuna watu WANALIPANA POSHO LAKI 4 PER DAY. Wametulia
- Watu wamezuiwa kusafiri kwa amri yako. Hela zote za MAKUSANYO, WATUMISHI HEWA, Unagawa kama njugu kwa uwatako. Tumetulia
- Unapiga wapinzani. Tumetulia
- TUNAHANGAIKA. Tafadhali heshimu hisia zao,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom