mjasiliaupeo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2013
- 2,162
- 3,088
Haha! Ngoja ni park ndinga mtaa huu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitatoa million 50 kila kijiji,Million 50 mtazipata katika miradi ya maendeleo
Nitatoa ajira kwa vijana namalizia kutoa wafanyakazi hewa! Nafanya uhakiki wa watumishi
Vijana mjiajiri wafanyakaz waliopo wanatosha walimu wa sekondari mtahamishiwa primary
Mimi rais wa Watanzania wote awe CHadema ,CUF ,Mh spika washugulikie na wakitoka nje ya bunge mimi nitawashughulikia
Kama kuna MTU kajenga katika eneo la serikali bomoa,Hawa wapiga kura wangu wasibomolewe mpaka tathmin na fidia itakapotolewa,
Lishetani lishindwe..ktk jina la Yesu. AminaYaani viongozi tuliowapa dhamna wamekuwa miungu watu. Nimekashangaa kamakonda leo eti anasema amani amani iko wapi zaidi ya kukandamiza watu tu. Leo hii hamna hata platform ya kuexpress kero yaani nchi nzima imepigqa ganzi.
Dhana ya maandamano ni kuelezea hisia na matitozo mbalimbali ya kijamii. Leo hii hamna ajira, unataka tuzungumzie wapi badala ya maandamano au kuna vitu mnaficha visijulikane.
Nashangaa sana nguvu kubwa inayotumika kuzima maandamano. Mbona jk aliruhusu maandano na nchi ilikuwa inakwwnda vizuri.
Nani kakwambia maendeleo ni ukimya wa woga au mabarabara pekee.
Maendeleo ni kuwa huru ilimrdi huvunji taratibu.
Amani haiwezi kuwa kutishiwa bali itoke rohoni. Mtu unawwza kuwa na billions lakini bado huna maendeleo kwa maana ya amani moyoni.
Hivi huyu shetwani jpm tulimtoa wapi. Mbona ni ****** sana kiasi hiki
Inauma sana mkuuHaiwezekani kabisa usikosolewe wewe malaika?
Wewe ni adui namba moja wa taifa kiuchumi, kisiasa na kijamii
Umeua uchumi, umeua demokrasia, umeharibu huduma za jamii kwanini usiwe adui wa taifa??
Halafu ati kukosolewa hutaki
, Mara nyingi ujasiri huongezeka mtu anapokumbana na majaribu ya hatari na kuogofya.
Ben Saanane ambaye alikuwa mkosoaji mkuu wa rais kuhusu PhD yake alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha tukajua watu wataogopa, lakini bado wanakosoa tena bila woga. Nilitegemea baada ya Lema kukaa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne ataacha kukosoa bado anaendelea kukosoa.
Kila siku tunashuhudia viroba vya maiti vikitolewa baharini labda kwa makusudi ya kuwatisha wakosoaji, instead wakosoaji kwenye mitandao na hadharani ndio wanaongezeka.
Kila siku tunasikia wabunge hasa wa upinzani wakikamatwa lakini kadri wanavyokamatwa ndivyo wanavyojawa na ujasiri, sikutegemea mbunge asiyekuwa na makuu Joseph Selasini kupata ujasiri wa kuwaongoza Warombo kuishinikiza serikali iwaambie alipo mpiga kura wake Ben Saanane.
Kuna matukio mengine mengi yamefanyika kwa nia ya kutisha na kunyamazisha wakosoaji, tukio kama la Ulimboka, Mvungi, Mawazo, mabomu ya Arusha, tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu ni mbinu ya kuwatisha watu wasiseme waliyonayo moyoni.
Nina uhakika wa 100% kuwa mbinu hii kamwe haitafanikiwa kuwazuia watu kusema labda kama wameamua kuwamaliza wakosoaji wote kwa kuwatandika risasi na kwamba wameamua kujipambanua hivyo na dunia ujue. Maana hakuna nchi yeyote duniani iliyowahi kufanikiwa kuwanyamazisha wakosoaji wake kwa mbinu hii. Makaburu wa Afrika Kusini waliokuwa na silaha zote walitumia mbinu hii bila mafanikio, na kila walipozidi kuwaua wakosoaji ndivyo sauti zilivyozidi kuongezeka.
Kama matukio haya ya mauaji na manyanyaso watu kuwekwa mahabusu na baadae kuachiwa kwa kukosekana ushahidi yana lengo la kuwanyamazisha na kuwatisha wakosoaji wa rais na serikali, naomba waelewe kuwa ukimtoa Lissu mmoja utazalisha Lissu 100 walio na ujasiri zaidi ya Lissu original.
Wewe ni adui namba moja wa taifa letu ukweli ndo huo
Utanufaika na nini endapo rais atajiuzulu?Ni ushauri wa bure na wakiungwana kabisa kabisa,
Tokea uingie madarakani nchi imekumbwa na mambo ya kutisha sana,hali ambayo haijawahi kutokea katika hostoria ya Taifa hili la Tanzania.
Nia na madhumuni yako wengi tunayaona na hayana shaka kuwa unataka kuijenga Tanzania yenye maendeleo na faida kwa kila mmoja wetu.
Huenda matukio yanayoikumba nchi hii ni ya kupangwa ili kusabotage utawala au tuseme uongozi wako. Inawezekana polisi,vyombo vya usalama na wengine hata waliokaribu nawe kichama wanakuzunguuka na kupanga mipango na mikakati ya kuiletea sura mbaya Serikali yako kwa uangalifu mkubwa sana,kwani matukio yanatokea hadharani mchana kweupe ,ila hujawahi wewe wala sisi kusikia wahusika wamekamatwa,kwa kisingizio cha wachunguzi kukuweka na kutuweka kwenye mabano ya mazingira ya matendo hayo kutokea katika mazingira ya kutatanisha na pia kutendwa na watu wasiojulikana.
Ni dhahiri kuwa vyombo vya kiintelejensia vimeshindwa kazi na kauli mbiu yao nj uchunguzi unafanyika au haujakamilika na kukuweka katika wakati mgumu sana,kwani wewe na wananchi mngependa kusikia wahusika wa matukio wanakamatwa na kutiwa hatiani,mbadala tunasikia vyombo hivyo vikijilabu tupo makini na nchi ipo salama,kauli amabayo inamuudhi kila Mtz.
Ikiwa Mtz mmoja tu atapotea au kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha basi nionavyo mimi nchi haipo salama ,itakuwa tumevamiwa na snipers ,tutamalizwa sote mmoja baada ya mwingine.
Ndio nikaona ni bora ukajiuzulu ila kabla ya hio waekee waTz tume huru ya uchaguzi ili ile kumbukumbu utakayoiwacha kwa Taifa hili iwe ni ya kukumbukwa na vizazi vijavyo,wananchi wamechoka na mapambano ya wabunge na sasa madiwani na mameya ni aibu .