Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Unazi unakufanya uamini deni kuongezeka ni maendeleo pia.

Unazi unakufanya uamini vitu Kupanda bei ni maendeleo.

Unazi wako unakufanya uamini watu wanaokukosoa hawakupendi na hawakutakii mema.

Unazi wako unakufanya uamini biashara kufa na Maduka kufungwa ni maendeleo.

Unazi unakufanya uamini soko la hisa kuporomoka ni maendeleo.

Unazi unakufanya kuamini mtu hawezi kukuunga mkono akiwa upande mwingine.

Unazi unakufanya uamini watu wengine kuuliwa,kutishwa, kutekwa na kupotea ni haki yao.

Unazi unakufanya uamini mawazo ya mtu mmoja tu ndio sahihi

Unazi unakufanya uamini mtu mmoja anaweza kuongoza wengine milele.

Unazi unakufanya uamini wafanyakazi na wanafunzi kulazimishwa kumkubali na kushiriki mikutano ya mtu mwingine uzalendo.

Unazi unakufanya uamini watu wanaozungumzia mambo yao katika ardhi yao ni dhambi.

Unazi unakufanya uamini kuwa na marafiki wenye sifa mbaya ni ndio kuwa salama.

Unazi unakufanya uamini wengine kubomolewa na wengine kutobolewa ilhali wote wamejenga kimakosa ni sawa.

Unazi unakufanya usifie tu na usipende kuambiwa ukweli kuhusu kasoro zilizopo.

Unazi unakufanya uwe ujione upo salama hata kama umezungukwa na hatari kubwa na nyingi.

Uwe wa huko au wa kule...

Acha unazi uyaone mambo katika uhalisia.
 
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje

hatuwezi kuruhusu sukari toka nje ya nchi kuingia kienyeji. tunahitaji kulinda viwanda vyetu vya ndani na ajira ya Watanzania ambao wameajiriwa katika viwanda hivo. Pia kuna wakulima wengi sana wa miwa kando kando ya mashamba makubwa ya miwa. hivyo pia tunahitaji kulinda soko la miwa yao. Tukiruhusu kienyeji sukari ya nje athari yake kiuchumi ni kubwa sana kuliko tunavyoshabikia humu jukwaani. Tutaua viwanda vyetu vya ndani, tutakosa mapato ya serikali na opia ajira za watanzania walioajiriwa moja kwa moja katika viwanda hivyo na waliojiajiri katika kilimo cha miwa kitakuwa hatarini.
 
Nchi ilikofikia kwa sasa sijui hatma yake,watu wanatekwa,watu wanateswa,watu wanauawa,watu wanapotezwa na magufuli kama Rais yupo tu hajatoa kauli yoyote ya kukemea jambo hili,je nchi inakuwa mahala gani???
 
Nadhani unakumbuka uliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania huku mkono wako wa kulia ukiwa umeshika Biblia takatifu ambayo ni neno la Mungu.

Hii inamaanisha kwamba uliapa mbele ya Mungu na si mbele ya wanadamu, ni kwa sababu binadamu unaweza kumfanya lolote lakini Mungu si mwanadamu na hana utani na binadamu.

Taifa lilijua limepata kiongozi mwenye uchungu na nchi yake na mwenye huruma na watu wake.

Kinyume chake ukaanza na chuki za wazi kwa wapinzani, badala ya ahadi ulizotuahidi.

Katiba inatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa na shughuli zao zote za kisiasa.

Wewe hutaki kusikia habari za watu wanaoitwa "wapinzani ".

Wapinzani kwako ni adui namba moja na siyo umaskini na ujinga.

Neno la Mungu katika kitabu cha Isaya 43:26 linasema ,"Unikumbushe, na tuhojiane, eleza mambo yako, upate kupewa haki yako ".

Hapa Mungu ametueleza wote bila kujali tabia zetu endapo tunamwabudu au lah!

Wewe hutaki watanzania wakueleze shida zao kwa njia ya maandamano ya amani, huwezi kuonana na mtanzania mmoja mmoja, njia pekee ni maandamano tu.

Sijui maandamano yanazuia viwanda kujengwa?

Sasa kama Mungu ameruhusu tumhoji kwa nini wewe hutaki kuhojiana na wananchi wako? Na ndo maana nataka kujua kama wewe upo juu ya Mungu, sasa kama utaendelea kukataa kuongea nasi, basi siye tutakushtakia kwa Mungu ili atueleze kama wewe upo juu yake, iweje yeye akubali maongezi na sisi na wewe hutaki?

Tafsiri yetu ni kwamba wewe upo juu zaidi yake na itabidi sasa na Mungu athibitishe hili na tumeanza kumwomba leo ni siku ya 10, bado siku 110, tutapata majibu sahihi.
 
Inamaana ROMA alipoimba nakwenda ZIMBABWE hamkumuelewa anamaanisha nini...!? Usikilize tena na tena ule wimbo kisha tuliza akili yako kuutafakari utaelewa maana mule FASIHI imetumika zaidi
 
Siku hizi tunaogopa hata kutoa mawazo yetu popote pale..wasiojulikana wapo kona zote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom