Nadhani unakumbuka uliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania huku mkono wako wa kulia ukiwa umeshika Biblia takatifu ambayo ni neno la Mungu.
Hii inamaanisha kwamba uliapa mbele ya Mungu na si mbele ya wanadamu,ni kwa sababu binadamu Unaweza kumfanya lolote lakini Mungu si mwanadamu na hana utani na binadamu.
Taifa lilijua limepata kiongozi mwenye uchungu na nchi yake na mwenye huruma na watu wake.
Kinyume chake ukaanza na chuki za wazi kwa wapinzani, badala ya ahadi ulizotuahidi.
Katiba inatambua Uwepo wa vyama vingi vya siasa na shughuli zao zote za kisiasa.
Wewe hutaki kusikia habari za watu wanaoitwa "wapinzani ".
Wapinzani kwako ni adui namba moja na siyo umaskini na ujinga.
Neno la Mungu ktk kitabu cha Isaya 43:26 linasema ,"Unikumbushe, na tuhojiane, eleza mambo yako, upate kupewa haki yako ".
Hapa Mungu ametueleza wote bila kujali tabia zetu endapo tunamwabudu au lah!
Wewe hutaki watanzania wakueleze shida zao kwa njia ya maandamano ya amani, huwezi kuonana na mtanzania mmoja mmoja, njia pekee ni maandamano tu.
Sijui maandamano yanazuia viwanda kujengwa?
Sasa kama Mungu ameruhusu tumhoji kwa nini wewe hutaki kuhojiana na wananchi wako? Na ndo maana nataka kujua kama wewe upo juu ya Mungu, sasa kama utaendelea kukataa kuongea nasi, basi siye tutakushtakia kwa Mungu ili atueleze kama wewe upo juu yake, iweje yeye akubali maongezi na Sisi na wewe hutaki?
Tafsiri yetu ni kwamba wewe upo juu zaidi yake na itabidi sasa na Mungu athibitishe hili ,na tumeanza kumwomba leo ni siku ya 10,bado siku 110,tutapata majibu sahihi.