Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
1.Uchumi wa nchi upo hoi
2.Hataki kuajiri,yeye ni kufukuza tu
3.Ameua uhuru wa Habari(kwa kuthibitisha hilo huu uzi hautadumu)
4.Ameua Demokrasia
5.Anatumia pesa za umma kulaghai wapinzani (kuwanunua) na kurudia uchaguzi ,je? Hivyo ndo viwanda?
6.Wanaomkosoa anawatisha
7.Manunuzi ya ndege hayakuwa na baraka za wananchi (bunge)
8.Hakuna anayejua nchi hadi Sasa hivi ina mwelekeo gani,kila kukicha mambo ya ajabu yanaibuka,samaki wa ziwa Victoria wamegeuka kuwa Bange, watu wanajiuliza kwa nini isiwe samaki wa ziwa Nyasa,ziwa Tanganyika au wa Baharini? Kuna tetesi kuwa anajenga kiwanda cha samaki kwa ubia na wachina Sasa anaona samaki wa ziwa Victoria wataisha.
9.Ana chuki za wazi na wapinzani, moyoni mwake huwaona Kama wahaini.
10.Hakuna mtu ambaye hajalia chini ya uongozi wake, wafanyabiashara wamelia, wakulima wamelia, wafanyakazi wamelia, wafungwa wamelia.
Sasa tukupende kwa lipi Baba? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hatukupendi.
 
Huyu ndiye Tuliyekua tunamtaka kwa muda mrefu ili aje atuletee mabadiliko ya kweli.

Amekuja kunyoosha mabondo na vilima ili ajaye atembee pazuri kwa uhakika.

Nchi ilikua imepoteza uelekeo mpaka vyama vya siasa vilikua vinaongozwa na wahalifu. Watu wanaoigiza michezo ya hatari kwa kushughulikia watu kama alivyokua Mbowe na kugeuza chama kuwa SACCOS binafsi.
Tumeona mbivu na mbichi sasa Chadema inapukutika na Mbowe anangangana kwa kusema kuwa hawezi kumwachia mtanzania wa Kabila lingine uenyekiti wa Chama.

Wanyooshe baba.
Usirudi Nyuma.
 
Screenshot_2018-08-16-22-15-11.jpg

Naomba kuwasilisha
 
Anatupeleka kwenye ulimwengu usiokuwa na blaablaa , uchakachuaji , ufisadi nk . Hakika ni uchumi wa kati
 
Anatupeleka kuzimu! Kasi ya kuharibu umoja wa taifa letu na kuua democrasia.Atakumbukwa kwa madhambi haya.Nilimtumainiavsana awali kama mtendaji makini ,lakini kwa ushamba wa siasa juu ni aibu na balaa kwa taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya miaka kumi baadae tutakuwa tunatembea kifua mbele na Tanzania [emoji1241] itakuwa mfano kwa nchi jirani kwa maendeleo
 
Watanzania tumekuwa watu wa kuyumbishwa mara Dr Shika mpaka GPA ya 32.
Ni wakati turudi kuuliza maswali ya msingi.
1.Yako wapi makontena ya makinikia?Ziko wapi hela za tulizoahidiwa?
2.Zile range rover ndani ya makontena bandarini zimepelekwa wapi?
3.Yale mabasi mapya ya mwendo kasi vipi?
4.Vile vichwa vibovu vya treni vimeanza kazi?
5.Matengenezo ya viwanda vya saruji yatakwisha lini?
6.Kusimamishwa kwa ajira kupita ukaguzi wa watumishi hewa kutaisha lini?
7.Millioni 50 kwa kila kijiji zimeshaanza kutumwa vijijini?
8.Madawati ya elimu kwanza na tenda walizopewa magereza mbona zimesimama?
9.wizi wa mpaka uniform za polisi kwenye jeshi la polisi wahusika walikatwa?
10.Lugumi kashaanza kufunga mitambo?
11.Mahakama ya mafisadi ina kesi ngapi?
12. Wifi ya dreamliner iko poa tayari?na lini itaanza route za "bombay"
13.Ukaguzi wa vyeti feki umekwisha?
14.List ya wauza madawa ya kulevya wangapi wako ndani?
15.Shisha bado hairuhusiwi?Boda boda mwisho saa sita vipi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom