Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwa maoni yangu na matwakwa yangu ambayo kila Siku namwomba Mwenyezi Mungu ayakubali ni kwamba Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli aiongoze Tanzania hata kwa miaka 50 ijayo kwani namkubali, nina uhakika nae na namuamini kwa 100% kuwa ndiye Rais ambaye Tanzania ya sasa tulikuwa tunamtaka na kumlilia siku nyingi ukiachia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Burito Kambarage Nyerere.
Hizi ni akili za Ngamia
 
Watu tupo ktk maombolezo ya watanzania wenzetu waliofariki,
Wengine ndio wanachkulia Advantage ktk hili tukio ili kutafa kiki ktk SIASA
 
Mke wa mtu kwangu siwezi yumba kwa hilo labda hayo mengine muhimu ni kufarijiana katika kipindi kigumu kama hiki R I P
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!


Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Nani atamuelekeza wakati hapendi kusikia ya mtu? CCM haina ramani?
 
Kama mtu alishasema yeye ni kichaa unategemea atatupeleka wapi zaidi ya Milembe?
 
Yaani badala ya kudhibiti RUSHWA Jitu linadhibiti VYOMBO VYOTE vinavyoibua RUSHWA !!
 
Katika hali ya kawaida, kuna kauli au maneno ambayo mtu huwezi kuyatamka hadharani unless una mapungufu kichwani mapungufu yanayoweza kuashiria tatizo la afya ya akili.

Kwa mfano, kumuambia mtu vipande thelathini alivyojichotea atavitoa kupitia sehemu fulani za mwili wake(niliwahi sikia kuwa aliitoa hii kauli. Kama haipo mnikosoe).

Maneno kama haya mtu unaweza kuyatamka mbele za watu ukiwa ama ni mlevi au mko katika ugomvi huku hasira zimekupanda kupitiliza lakini sio hivi hivi.

Ukiacha kauli hii, kuna matamshi mengine ambayo ni ya kuji-contradict kiasi kwamba mtu unajiuliza hivi huyu mtu anakumbuka jana au juzi aliongea nini na leo anaongea nini.

Kwa mfano ile kauli kuwa wakati anaingia ofisini, alikuta teyari bei ya kikombe cha chai imepanda wakati si kweli bali bei ilipanda baada ya yeye kuingia ofisini na kufanya aliyoyafanya na kisha bei ya kikombe cha chai ndio ikapanda ghafla.

Kauli nyingine ambayo mpaka leo huwa naishanga ni ile ya kuwadhalilisha wanaomsaidia majukumu kuwa ni wapu...avu (hii iliniacha hoi kabisa).

Iko mifano mingi tu ambayo mtu ukiitafakari, utagundua ndugu yetu huyu sio kama hana mshipa wa noma, bali huenda hayuko fit mentally(tutapata tabu sana).

I hope iko siku atafanya kituko kikubwa (kwa kauli au matendo) kuthibitisha mtazamo huu ambao kwa sasa umeanza kuwa ni mtazamo wa wengi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom