Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kiburi anakipata kutoka jwtz,hawana huruma na wananchi! Wangekuwa na huruma wangesha mwadabisha ndio maaana Mkuu wa majeshi alimteua mtu wa kabila lake ili wamlinde na ngaz karib zote kateua watu wa kabila lake au ukanda wa ziwa ili wasimsalit cc anaetuita wanyonge tuzid kunyongwa
 
Nafikiri wewe ndio una kiburi,nchi haiongozwi kama unavyofikiri wewe, nchi si saccos,mlizoea kumpinduapindua Kikwete mtakavyo, hiyo miruzi yenu pelekeni kwenye kuimarisha.saccos zenu zenye wenyeviti wa maisha
Ondoa taarabu zako we mataga!
 
Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
umeongea vzr lakini hapo kwenye wanawake una ugomvi nao?
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Hili bandiko litadumu sana
 
Kiongozi wa namna hii wala hafiki mbali hata wananchi tusipochukua hatua ya "Kumlenga Mawe" kama alivyopata kusema Baba wa Taifa

Mfano ni Ali Bongo wa Gambia alivyopigwa na stroke..

Imagine watu wanalalamika Halmashauri ziko hoi kifedha baada ya kuzinyang'anya vyanzo vyao vya mapato lakini bado mtu anazibebesha mzigo wa kugharamia posho za Watendaji wa Kata 4,700 kwenda kuona naye Ikulu, na hapo hapeleki hela kwenye hizo Halmashauri zaidi ya kujenga kijijini kwake, huyu mtu ni makini kweli? Hivi ina maana Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, MaRAS, MaDAS, hawana uwezo wa kuwapa maelekezo hayo ya "kuvuruga uchaguzi" na kuiingiza nchi kwenye migogoro ya kijinga na umwagaji hadi awape yeye mwenyewe?

Imagine watu wanalalamika ubadhirifu mbalimbali unaofanywa na serikali yake lakini bado anapeleka Mawakili "incompetent" 15 kwenye kesi ya kumdhulumu Lissu haki zake, gharama zote hizo za haja gani?

Hapo bado kila siku anazunguka mtaani akigawa hela za Umma Cash hovyo hovyo kwa watu wanaoimba sifa zake kana kwamba hizo hela ni za kwake...

Imagine mtu anaelekezwa ni gharama kununua madege ya mabilioni ya fedha bila kwanza kushughulikia changamoto za uendeshaji za shirika la ndege la ATCL, lakini bado mtu anakwenda mwenyewe kufanya manunuzi pasipo mtu mwingine kufahamu, kisa tu tamaa ya 10%, unajiuliza utimamu wa akili wa ndugu yetu ukoje!

Hapo anahangaika kumsumbua Ramaphosa ndege iachiliwe, bila kujua kuwa kwa South Africa Judiciary hawafanyi kazi kwa amri za Ikulu tofauti na alivyozoea yeye hapa...

Mungu akikuinua ukapata nafasi ya kuongoza Taifa ni heri uendelee kumtegemea na si kujawa na kiburi...KIBURI WILL LEAD YOU TOWARD A CAR CRASH, HEAD ON COLLISION.

Ni vema mtu ukajisahihisha tu, EVERYBODY IS BLESSED WITH A CAPACITY TO CHANGE!

Mungu Ibariki Tanzania!

Ali bongo ni wa Gabon.Dikteta Yahya Jameih ni wa gambia alikuwa gwiji wa ndumba na ulozi aliyewafadhili wasiojulikana wa kuwateka na kuwauwa wenye mawazo tofauti na yake ambao wengi wa wasiojulikana Baro kawasweka ndani wanaoza jela juu ya matendo yao na Jameh hana uwezo wa kuwasaidia sababu hana mamlaka amri wa dola zaidi ya kumuamuru Mke wake tu.Kama alipigwa stroke ni jambo jema sana linaponya taifa pale wakala wa shetani anapopata dhamana sisi ni Furaha kwetu tunaongeza idadi ya bia cheers Kwa sana mezani.Copy na paste zaidi anajifikiria binafsi Kwa maslai yake ya kisiasa kulidhisha nafsi yake kujifichia kwenye kichaka cha utetezi wa wanyonge kimaneno kivitendo akiwanyongelea mbali.Too much inner selfishness like mobutu, Mugabe, yayha Jameh.Madikteta wote duniani mama yao huwa mmoja tabia zao ufanana.
 
Tanzania ni nchi yenye historia ya kuheshimika mno ktk nchi zote za kusini mwa Africa.
Tanzania ni taifa pekee Africa lililoshiriki kwa nguvu zake zote ktk ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa.
Tanzania kwa miaka yote ndo imekuwa kimbilio la wananchi wa mataifa ya jirani kila wanapopata matatizo .
Lakini heshima na hadhi ya Tanzania imekuwa ikishuka kila siku kwa sababu ya kundi la watu wachache wanaopenda vyama vya siasa kuliko nchi yao.
Watu wanapenda chama kuliko nchi, huu uendawazimu hautavumilika kwa gharama yoyote.
Wakati Mungu anaiumba Dunia na Tanzania ilikuwemo ndani ya Dunia hii, na hapakuwepo CCM, CHADEMA, CUF wala dude lolote lile la kuwatesa watanzania wa Mungu zaidi ya Tanzania yenyewe tu na Raslimali zake zote za kutukuka Kama Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Gesi, maziwa, Bahari, ardhi safi kwa kilimo, wanyama na mito mizuri ya kutumia kwenye kilimo cha irrigation.
Mungu wa mbinguni kila leo anashangaa kuona watu aliowapatia Raslimali za kujikomboa na umasikini bado wanaishi maisha magumu kupindukia eti kwa sababu ya dude linaloitwa siasa.
Ndo maisha wanayoishi wananchi wa North Korea ,wana maisha magumu kupindukia, hawaruhusiwi kuhoji wala kulalamika popote.
Kila mwananchi wa North Korea ni lazima awe mfuasi wa chama tawala kinyume chake kifo ni haki yake.
Wenzao wa South Korea wana maisha bora, haki na Demokrasia imetamalaki.
Hatutakubali Tanzania yetu iwe ya familia ya kundi flani la watu kwa sababu ya manufao yao wakitulaghai ni manufaa ya nchi huku tukipigwa risasi kila tunapohoji juu ya mwenendo wa nchi, huku watesi hawakamatiki.
Nasema hatutakubali kwa gharama yoyote ile.
Tanzania ni bora kuliko hizo siasa zenu za kishamba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom