Kiongozi wa namna hii wala hafiki mbali hata wananchi tusipochukua hatua ya "Kumlenga Mawe" kama alivyopata kusema Baba wa Taifa
Mfano ni Ali Bongo wa Gambia alivyopigwa na stroke..
Imagine watu wanalalamika Halmashauri ziko hoi kifedha baada ya kuzinyang'anya vyanzo vyao vya mapato lakini bado mtu anazibebesha mzigo wa kugharamia posho za Watendaji wa Kata 4,700 kwenda kuona naye Ikulu, na hapo hapeleki hela kwenye hizo Halmashauri zaidi ya kujenga kijijini kwake, huyu mtu ni makini kweli? Hivi ina maana Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, MaRAS, MaDAS, hawana uwezo wa kuwapa maelekezo hayo ya "kuvuruga uchaguzi" na kuiingiza nchi kwenye migogoro ya kijinga na umwagaji hadi awape yeye mwenyewe?
Imagine watu wanalalamika ubadhirifu mbalimbali unaofanywa na serikali yake lakini bado anapeleka Mawakili "incompetent" 15 kwenye kesi ya kumdhulumu Lissu haki zake, gharama zote hizo za haja gani?
Hapo bado kila siku anazunguka mtaani akigawa hela za Umma Cash hovyo hovyo kwa watu wanaoimba sifa zake kana kwamba hizo hela ni za kwake...
Imagine mtu anaelekezwa ni gharama kununua madege ya mabilioni ya fedha bila kwanza kushughulikia changamoto za uendeshaji za shirika la ndege la ATCL, lakini bado mtu anakwenda mwenyewe kufanya manunuzi pasipo mtu mwingine kufahamu, kisa tu tamaa ya 10%, unajiuliza utimamu wa akili wa ndugu yetu ukoje!
Hapo anahangaika kumsumbua Ramaphosa ndege iachiliwe, bila kujua kuwa kwa South Africa Judiciary hawafanyi kazi kwa amri za Ikulu tofauti na alivyozoea yeye hapa...
Mungu akikuinua ukapata nafasi ya kuongoza Taifa ni heri uendelee kumtegemea na si kujawa na kiburi...KIBURI WILL LEAD YOU TOWARD A CAR CRASH, HEAD ON COLLISION.
Ni vema mtu ukajisahihisha tu, EVERYBODY IS BLESSED WITH A CAPACITY TO CHANGE!
Mungu Ibariki Tanzania!