Kazi za ujenzi anafanya sana tu ila kurugenzi ya mawasaliano ya Shaban Kisu ilikuwa hopeless
Kukaa kimya kutosema kilichofanyika watu wanadhani labda hakuna kinachoendelea na yeye Mama Samia kujieleza mafanikio yake au anachofanya midomo mizito tofauti na Magufuli
Kinywa cha Mama Samia kizito
Mimi binafsi nilikuwa najua huyu mama hamna kitu lakini baada ya kupata taarifa zenye takwimu nikaamini kafanya makubwa mengi ila watendaji wake na yeye hawayasemi utasikia tu ohhh mama anafanya kimya kimya tofauti na mtangulizi wake Magufuli mpiga yowe kila kitu anaita press!!! Sera gani hiyo ya kimya ?eleza tu kodi za watu nini umefanya usiogope au kuona aibu .
Zuhura Yunus nadhani hili aliangalie akutane mara kwa mara na waandishi wa habari kuwaeleza what is going on so far aliyofanya Mama Samia
Mama Samia anasifiwa tu kwa madarasa tu si kweli na yenyewe anasifiwa sababu ya Ummy Mwalimu alikuwa ndiye aongea mara kwa mara kuwa mama kajenga madarasa nchi nzimav public ndio ikapata information
Mawaziri wengine igeni Ummy Mwalimu pia kueleza nini kinafanyika kwa sasa wizara zenu kwenye public vinginevyo Hamtetendei haki mama Samia anaonekana hana alifanyalo