mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 96,490
- 138,365
Solo ana vina ni muandishi mzuri,ila kwa wakati ule mziki,message sele alikuwa juuSolo namkubali kiasi chake, lakini ukifuatilia sana ngoma zake, utaona ni mtu mjivuni alafu ana lugha ya matusi japo anatumia tafsida.
"vidato sita nilivopitia ndo vinavonisaidia hata kama wakinibania"
"Kuna kupara miwa na kupara samaki'
"Huku Mombasa ukiwa punga watu wanatwanga"
"Dume zima shanga kiunoni"-
"Kama inabana leta tuitanue"
"Tamaa ikizidi sana watu watakupakata"
Hiyo ni baadhi ya mistari katika nyimbo zake. Japo nikimsikiliza kwenye "Homa ya dunia" naona ilikuwa na ujumbe kwa hadhira.
Lakini Sele nyimbo zake hazina lugha chafu. Yaani zina ujumbe mzuri.
Sisemi Sele ni mkali kuliko Solo.
Ova