Anayenufaika zaidi kwenye mahusiano ni nani, mwanamke au mwanaume?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Mwanaume atapambana kwa kila njia, iwe vibarua, kazi ngumu, kukopa, ufisadi ilimradi tu aweze kumuhudumia mpenzi wake, iwe kwenye kumlisha, kumvisha, kulipa kodi, kusomesha, pamoja na gharama nyingi zilizojificha; hapo mwanaume ananufaikaje?

Mwanaume atajitahidi kujinyima na kusomesha, baada ya miaka kadhaa kupita watoto wakiwa wakubwa watamchukua mama yao na kwenda kuishi naye, huku mzee/baba akitelekezwa; mbaya zaidi mtoto anaanza kukuimbia ''nanii kama mamaaaa..aaa'' bila kujua ya kuwa baba yao ndio aliyekuwa mpambanaji mpaka wao kufikia pale; hapo mwanaume ananufaikaje?

Baada ya kuligundua hilo, kwa sasa najipa raha mwenyewe.

 
Mwanaume atapambana kwa kila njia, iwe vibarua, kazi ngumu, kukopa, ufisadi ilimradi tu aweze kumuhudumia mpenzi wake, iwe kwenye kumlisha, kumvisha, kulipa kodi, kusomesha, pamoja na gharama nyingi zilizojificha; hapo mwanaume ananufaikaje....​
Wewe wape tu haki yao ya mavazi,malazi na chakula. Hayo mengine tutayajadili mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…