Masai wa Town
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 7,009
- 25,406
Naona hivi karibuni, Kila kiongozi wa serikali au wa kidini anayesimama anasema vyama vya siasa vinapaswa kuilinda amani ya nchi.
Lakini katika maelezo ya Kila mmoja kwa kina, utagundua anazungumia agenda za CHADEMA ikiwemo Ile ya "no reforms, no election". Yaani kwa tafsiri nyepesi wanamaanisha CHADEMA ndiyo wapaswa kulinda amani ya nchi hii.
Miaka yote CCM imekuwa ikiiba kura na KUPORA UCHAGUZI kwani katika Kila uchaguzi tangu 2015 Kuna watu walikamatwa mbele ya camera wakibeba mabegi ya kura zilizopigwa tayari wakizipeleka kwenye mabox ya kura, jambo linalohatarisha amani ya nchi. Lakini CHADEMA wakijitokeza na kuitisha mabadiliko wanaonekana wanahamasisha uvunjifu wa amani.
CCM mjitafakari na mfahamu kuwa Wizi wa kura na KUPORA UCHAGUZI ni uvunjifu wa amani lakini KUKEMEA wizi wa kura na KUPORA UCHAGUZI siyo uvunjifu wa amani. Pia siyo CHADEMA na vyama vya upinzani pekee wa kuhusishwa katika utunzaji wa amani ya nchi bali CCM pia na wadau wote wanapaswa kuwajibika.
#No_Reforms_No_Election
You can take me to jail on that.