TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Ametoa ushauri muwe na funguo zenu, hujaona? Umeona tu roho mbaya ya huyo alogoma kufungua mlango?

Yan mtu umejizoelea kulala saa 4, mumeo mlevi anakaa bar mpaka saa7/8/9, kuashwa kila wakati hivyo inaboa sana.
Bora na ww umejionea.
Na akirudi vurugu. Lipo lipare limoja la makanya linafanya bandari nalo lina tabia za kula starehe huko na madanga halafu likirudi limelewa chakarii linampiga maza angu mdogo.... linanikera natamani hata lipate majanga Leo kesho.

We libaba kama unasoma hapa jua tu kwa matendo yako sikupendi kama m****avi
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima .
Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Hiyo sio salama pia. Imagine kama kuna vibaka nearby. Kuwa gate la remote au kulala hotel usiku ukiwa mrefu sana.
 
Ifikie hatua MTU kama hupendi tabia za mume urudi tu kwenu,kuliko unajua mume ni mlevi umekomalia kwenye Nyumba yake na mlango unamfungia.Nao ni watoto wa wanawake wenzenu walipata uchungu kama muupatao.Pumzika Mkuu,pumzika Kamanda!
Kamanda gani analewa hadi mke anachoka kumfungulia.

Hadi mke anakataa basi alishakuwa kero. Mwanamke ukute alibaki kwa sababu ya wanae ....akiwaza baba ni mlevi wanae wangeteseka kama akiondoka
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast foward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
apumzike kwa amani
 
Bora na ww umejionea.
Na akirudi vurugu. Lipo lipare limoja la makanya linafanya bandari nalo lina tabia za kula starehe huko na madanga halafu likirudi limelewa chakarii linampiga maza angu mdogo.... linanikera natamani hata lipate majanga Leo kesho.

We libaba kama unasoma hapa jua tu kwa matendo yako sikupendi kama m****avi
Hahahahaha, unamsema Mshana Jr sio. Yupo humu anakuangalia tu mchawi mstaafu. Atakufanyia kazi muda si mrefu.
 
Kamanda gani analewa hadi mke anachoka kumfungulia...
Hadi mke anakataa basi alishakuwa kero.
Mwanamke ukute alibaki kwa sababu ya wanae ....akiwaza baba ni mlevi wanae wangeteseka kama akiondoka
usihukumu kabla hujajua ukweli. kuna wanawake wengine ni controlling na wana gubu sana. pengine jamaa aliamua kuwa anapita bar kuepusha balaa la gubu la wife
 
Kamanda gani analewa hadi mke anachoka kumfungulia...
Hadi mke anakataa basi alishakuwa kero.
Mwanamke ukute alibaki kwa sababu ya wanae ....akiwaza baba ni mlevi wanae wangeteseka kama akiondoka
Tayari amekufa, Mimi mke ninapochoka na tabia za mume mama ake alikuwa bado anamhitaji.

Tayari amekufa.....okay,ni bahati mbaya ngoja awe huru sasa
 
Back
Top Bottom