TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast foward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Mke kawa mjane ghafla
Dah

Mara nyingi tafakari jambo kabla ya kutenda
 
Kwanza poleni wanajamii forams kwakuondokewa na mwenzetu.

Kuhusu ushauli wako huu ,ebu wambie wifi zako mama zako wadogo, waache adhabu zakikatiri. Unaanzaje Kugoma kumfungulia mwezio? Ona Sasa amekua mjane .

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati unakunywa mipombe huku ulimwita mjumuike pamoja wanaume tuache ubabe tembea na funguo zako utadhibiti hayo yote
 
Pole kwa wafiwa..

Mi nilikuwa na mazoea hayo ya kulewa na kurudi usiku naruka hizo nondo asubuhi najikuta nimekwaruzika mwili mzima kisa cha kuacha mchezo huo sitasahau.

Nilirudi siku hiyo kilevi kimezidi kuliko kawaida nikapiga simu na kugonga sikufunguliwa nikachukua maamuzi ya kuruka. Niliacha kila kitu juu ya nondo surwali shati hadi boksa. Nikaingia ndani nikalala na viatu tuu. Asubuhi kidogo mama angu afe kwa presha akajua nimeuliwa nikatupwa juu ya nondo kumbe nguo. Akaingia ndani nimelala uchi akanikagua mzima zaidi ya michubuko tuu. Sitasahau
Hama kwenu

Kapange
 
Eti kwa sababu ni baba mwenye nyumba a.k.a mume ukaleweeee weee hadi night kali halafu unikatishie usingizi wangu nikufungulie.... hapana kwa kweli. Kuwa na funguo za ziada... kama geti sio la kitasa basi kitengenezwe.
Ukute mke wa watu hata outing hajawahi kutolewa yeye Ana kazi ya kufungua mageti tuu....
Tuweni wakweli asee.
 
Ametoa ushauri muwe na funguo zenu, hujaona? Umeona tu roho mbaya ya huyo alogoma kufungua mlango?

Yan mtu umejizoelea kulala saa 4, mumeo mlevi anakaa bar mpaka saa7/8/9, kuamshwa kila wakati hivyo inaboa sana.
Ushauli wake wa kumiliki funguo, nimeiona sijaubedha Wala sijaupuuza.

Shida inakuja pale ambako mwenza ameamua kumunyosha huyo unae muita mlevi. Mageiti mengi hunguliwa kwa vitasa ukiwa nje.
Alieko ndani akiamua kukomoa anafunga makomeo kwa ndani , au kama Kuna asikali anatia na makufuri kabisa.

Je hapo funguo Yako itasaidia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora na ww umejionea.
Na akirudi vurugu. Lipo lipare limoja la makanya linafanya bandari nalo lina tabia za kula starehe huko na madanga halafu likirudi limelewa chakarii linampiga maza angu mdogo.... linanikera natamani hata lipate majanga Leo kesho.

We libaba kama unasoma hapa jua tu kwa matendo yako sikupendi kama m****avi
Lina hela? Kama lina hela usijemtibulia mazako mdogo
 
Tupige kura kumbaini huyo mwenzetu mi naanza na..............maana siju ya pili hii hajacomment humu wala kupost
Mkuu soma uzi vizuri. Jamaa kasema week mbili zilizopita ndo alipata hiyo taarifa ya msiba.
 
Eti kwa sababu ni baba mwenye nyumba a.k.a mume ukaleweeee weee hadi night kali halafu unikatishie usingizi wangu nikufungulie.... hapana kwa kweli. Kuwa na funguo za ziada... kama geti sio la kitasa basi kitengenezwe.
Ukute mke wa watu hata outing hajawahi kutolewa yeye Ana kazi ya kufungua mageti tuu....
Tuweni wakweli asee.
Nina uhakika kwa hizi comment zako haujaolewa, Nimekosea? Inaonekana una kiburi
 
Back
Top Bottom