TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Kule Njombe kuna jamaa alimua Mke wake kwa kiss kama hicho cha Mke kutofungua mlango.Jamaa akavunja mlango Mke alipokea kipigo mpaka mauti.

Badaye Jamaa aliachiliwa baada ya miezi 6 kwa kuua pasipo kukusudia.
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Kwa mtazamo wa haraka haraka hii nyumba tayari ilikuwa haina amani,shetani alikuwa ameshafanya yake,upendo ulikuwa umeshatoweka,ni dakika chache tu ambazo angefungua mlango na mume angeingia, na yeye angerudi kulala,lakini hizo dakika chache alizo dharau ameruhusu kifo kwa mume wa maisha yake,najua saa hizi anajutia lakini it's too late...
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Zamani wakati nakunywa mwanamke alikataa kunifungulia nikapiga ngumi mlangoni na kuna vioo,ilikua nife.Hawa viumbe wako kama nyuki,Asali yao tamu ila ukin'gatwa maumivu
 
shida inaanziaga pale manapokutana na kukubaliana kuoana.

usioea wala kuoelewa kwa bahati mbaya.
ndoa zasasa nyingi ni za bahati mbaya aka kuviziana.

Unakuta mmoja kaviziwa kakubalia kuoa au kuolewa lakini kiuhalisia hakuwa tayari au mhusika sio chaguo lake hapo sasa ndio balaa linapoanzia.
 
[emoji16] si kweli mkuu

Hao watu walishafikia either kuchokana, au kudharauliana.

Me napenda usuluhishi, sidhani kama naweza fikia mfungia mtu nje aisee.. huko ni mbali sana.
Sasa we unakuta daily ni ukifungua geti ni unakumbana na harufu Kali ya nyagi na Shah.wa + plus lipstick kwenye shati

Hizo nguvu za kufungua geti unazipata wapi?
 
Kwenye dini zote kuoa/kuolewa ni ibada lakini hizo hizo dini zinatutaka tuwe makini kwenye kuoa/kuolewa.

Kwa tafsiri ni kuoa au kuolewa na mtu sahihi, kwa mtu sahihi hata shida ikitokea inaweza kutatuliwa kiakili na wote mkawa salama.
 
Sasa we unakuta daily ni ukifungua geti ni unakumbana na harufu Kali ya nyagi na Shah.wa + plus lipstick kwenye shati

Hizo nguvu za kufungua geti unazipata wapi?

Wakati anakuoa hukujua kama anatabia hizo? kama ulijua na ukakubali kuolewa nawe hilo ni tatizo lako na ni either ukubaliane naye au muachane haraka.

Kama hakuwa na tabia hizo, kwanini amezianza ghafla ?
 
Yeye alipokataa kufungua wala hakuwaza hayo. Lakini pia huwezi jua ndoa yao ilikuwaje...ukute marehemu alikuwa aina ya wanaume ambao hawajali hisia za mke bali kujifurahisha yeye mwenyewe kwenye hizo pombe zake jambo ambalo mkewe alikuwa halimfurahishi
Haijalishi, usitetee ukatili hapa. Hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha alichokifanya huyo mama zaidi ya ubinafsi. Halafu ninyi wanawake acheni hulka ya kujifanya victims wa kila sintofahamu inayotokea katika ndoa/mahusiano. Ninyi huweza kuwa chanzo/villains wa mambo mengi tu.
 
Kuishi na mwanamke unatumika akili ya ziada, angejiongeza atoke na funguo zake baada ya kusoma tabia za mwanamke. RIP.
 
Tayari amekufa, Mimi mke ninapochoka na tabia za mume mama ake alikuwa bado anamhitaji.

Tayari amekufa.....okay,ni bahati mbaya ngoja awe huru sasa
Una busara sana aisee. Hakika mumeo ana bahati kukuoa.
 
Back
Top Bottom