TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

dah RIP.

qkigoma kukufungulia mlango usijitese kalale tu ulikotoka tena kwa wajuba hiyo ni game of chance, unaenda zako kujilalia na kamchepuko kako tu.... asubuhi unarudi mwepesiiii.
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia[emoji24]
 
Kwahiyo kuepusha gubu ndio unaona ukwende kushinda bar? Hapo unasuluhisha nini sasa?

Hivi mtu mnapendana na kuheshimiana vizuri hizo gubu zinatoka wapi? Ingawa najua kuna watu wapo both me & ke wana lawama sana
Kama wewe hauna gubu ubarikiwe ,mimi mke wangu ukifika muda wa kulala tu utasema vikao vya mahakama ndio vimeanza...naamua kushinda bar nikirudi niwe nimependeza
 
Kuna wakati wanawake wanahitaji ukatili kidogo ili mambo yaende sawa, ukijifanya mtu wa love love sana kwa hawa viumbe utakufa faster, inabidi uwe mhuni na mkatili kidogo kwa hawa viumbe ili uwe salama.

Naona sana ndugu zetu wanaojifanya watakatifu na waungwana kwa watoto wa kike mateso wanayoyapata hadi wengine kufa kabisa.
 
Hapo ungeshauri wanawake wenzio kuwa waache viburi visivyokuwa na maàna. Sasa aligoma kufungua alitaka akalale wapi wakati hapo ndipo nyumbani kwake!!!!
Kwani mwanamke wa watu ni Gate man... yani kwakuwa tu umeoa basi uwe mlevi kila siku unarudi mda umeenda jalafu eti lazima ufunguliwe kwa kuwa ni kwako...
Starehe zako zisiwakwaze wengine. Baba funguo yako uwe huru na usiwakwaze wengine
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.

Si kweli mkuu ,huyo alifumaniwa na mke wa mtu taarifa zake tunazo hapa Kituo cha kati na muhusika wa mauaji anatafutwa,na sio nondo ya geti ,alienda kumtafuna mke wa mtu kwenye nyumba anayoishi huyo mchepuko ndipo mwanamme akamfumania na kumchoma kisu.
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Upendo huvumilia yote, upendo hauhesabu mabaya
 
Angerudi bar kuagiza mbili anakunywa taratibu mpaka asubuhi
 
Pole kwa wafiwa..

Mi nilikuwa na mazoea hayo ya kulewa na kurudi usiku naruka hizo nondo asubuhi najikuta nimekwaruzika mwili mzima kisa cha kuacha mchezo huo sitasahau.

Nilirudi siku hiyo kilevi kimezidi kuliko kawaida nikapiga simu na kugonga sikufunguliwa nikachukua maamuzi ya kuruka. Niliacha kila kitu juu ya nondo surwali shati hadi boksa. Nikaingia ndani nikalala na viatu tuu. Asubuhi kidogo mama angu afe kwa presha akajua nimeuliwa nikatupwa juu ya nondo kumbe nguo. Akaingia ndani nimelala uchi akanikagua mzima zaidi ya michubuko tuu. Sitasahau
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] haki ni kichekesho
 
Ulevi mbwa na umasikini ndio unasumbua familia nyingi.
Kama una pesa geti la nyumbani kwako lazima uwe na fully access kama funguo au finger print au gari yako iwe connected na geti,huna haja ya kupiga honi au kugonga na kusumbua watu waliolala kisa ulevi wako wa kingese.
 
Ifikie hatua MTU kama hupendi tabia za mume urudi tu kwenu,kuliko unajua mume ni mlevi umekomalia kwenye Nyumba yake na mlango unamfungia.

Nao ni watoto wa wanawake wenzenu walipata uchungu kama muupatao. Pumzika Mkuu,pumzika Kamanda!
Umejuaje hiyo nyumba imejengwa na mwanamke?...mlevi alale nje full stoop
 
Kuna jirani yangu hapa yy siku zote ni kurudi saa nane za usiku,huwa najiuliza kazi zake ndo zinamalizika mda huo au ni nn?,najua anatumia pombe lakini si rahisi mtu kuwa kwenye viringe vya pombe siku zote hadi saa nane za usiku.

Mke wake ni mama wa nyumbani ,sijajua kama huwa anarudi kalewa au laa ila huwa nasikia geti tu linafunguliwa pamoja na sauti ya gari ,na nikitazama mda ni saa nane na madakika ,yani hii ni kila siku
 
Back
Top Bottom