Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Kwa mtazamo wa haraka haraka hii nyumba tayari ilikuwa haina amani,shetani alikuwa ameshafanya yake,upendo ulikuwa umeshatoweka,ni dakika chache tu ambazo angefungua mlango na mume angeingia, na yeye angerudi kulala,lakini hizo dakika chache alizo dharau ameruhusu kifo kwa mume wa maisha yake,najua saa hizi anajutia lakini it's too late...Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Yaani sijui atakua na hali gani maskiniDuh, uyo mke wake atakua kwenye majuto Sana,kitendo Cha kufungua geti asingechukua ata dakika moja, Sasa ameshapoteza mume
Hamna watu wananiboa kama walevi wa kurudi majumbani usiku wa manane.
Kila mtu Ana misimamo yake kuhusu maisha... .. kuliko kukomoana bora kuachanaNyie WanWake wa siku hizi heshima ni zero kabisa,yani ingekuwa mie ningeenda zangu Lodge kesho huyo Mke angerudi tu kwao.
Zamani wakati nakunywa mwanamke alikataa kunifungulia nikapiga ngumi mlangoni na kuna vioo,ilikua nife.Hawa viumbe wako kama nyuki,Asali yao tamu ila ukin'gatwa maumivuMemba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.
Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Ku mind your own business ni vizuri ila kumjua jirani yako ni vizuri zaidiJitahidi kumaindi bizinezi zako mkuu, unaonekana unapenda kufuatilia mambo ya jirani yako, achana nae kila mtu ana maisha yake ili mradi hakusumbui au kukukwaza.
Kwamba hataolewa na mwanamume mwengine?Duh, uyo mke wake atakua kwenye majuto Sana,kitendo Cha kufungua geti asingechukua ata dakika moja, Sasa ameshapoteza mume
Sasa we unakuta daily ni ukifungua geti ni unakumbana na harufu Kali ya nyagi na Shah.wa + plus lipstick kwenye shati[emoji16] si kweli mkuu
Hao watu walishafikia either kuchokana, au kudharauliana.
Me napenda usuluhishi, sidhani kama naweza fikia mfungia mtu nje aisee.. huko ni mbali sana.
Sasa we unakuta daily ni ukifungua geti ni unakumbana na harufu Kali ya nyagi na Shah.wa + plus lipstick kwenye shati
Hizo nguvu za kufungua geti unazipata wapi?
Haijalishi, usitetee ukatili hapa. Hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha alichokifanya huyo mama zaidi ya ubinafsi. Halafu ninyi wanawake acheni hulka ya kujifanya victims wa kila sintofahamu inayotokea katika ndoa/mahusiano. Ninyi huweza kuwa chanzo/villains wa mambo mengi tu.Yeye alipokataa kufungua wala hakuwaza hayo. Lakini pia huwezi jua ndoa yao ilikuwaje...ukute marehemu alikuwa aina ya wanaume ambao hawajali hisia za mke bali kujifurahisha yeye mwenyewe kwenye hizo pombe zake jambo ambalo mkewe alikuwa halimfurahishi
Una busara sana aisee. Hakika mumeo ana bahati kukuoa.Tayari amekufa, Mimi mke ninapochoka na tabia za mume mama ake alikuwa bado anamhitaji.
Tayari amekufa.....okay,ni bahati mbaya ngoja awe huru sasa