TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
Kuna member mmoja humu Jf aliwahi kuandika/kuleta uzi hapa akisema: "Wanawake sio wa kuonea huruma hata mara moja" Hivi ingemchukuwa dk. ngapi kumfungulia geti mwenza wake? Je, Baada ya tukio hili (Matokeo ya kiburi chake) anadhani itamchukua muda gani kumpata tena mwenza mwingine? akina mama tafadhali chukueni tahadhari mnapofanya maamuzi dhidi ya wenza wenu. Asante.
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie

kwa sasa ndugu jamaa na majirani hawaelewi kama shemeji yetu alikuwa amechoka amelala,wanachomuuliza ni kwanini hakumfungulia mwenye nyumba!!!!!

kila maamuzi yana faida na hasara zake,ukipima ukaona faida ni ndogo kuliko hasara usifanye.
 
kwa sasa ndugu jamaa na majirani hawaelewi kama shemeji yetu alikuwa amechoka amelala,wanachomuuliza ni kwanini hakumfungulia mwenye nyumba!!!!!

kila maamuzi yana faida na hasara zake,ukipima ukaona faida ni ndogo kuliko hasara usifanye.
Ndo hivo dunia yote inamlaumu yeye kwa kuwa chanzo cha mauaji kumbe chanzo ni mlevi mwenyewe
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Utakuja kulewa watu wabebe funguo waje kufanya Yao nyumbn.
 
Weka mlinzi getini ili ukifika akufungulie angalau uingie hata ndani ya boma!
Hawa viumbe "wakezetu' akiamua anafunga ,na funguo anaingia Nazo ndani.
Mlinzi anabaki geitini TU. Hapa Cha mhimu kama mtu anamiliki ka IST ni kuhakikisha unatembea na "chan" ukiona hawafunguwi funga chan ,vuta geiti lifunguke lenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chezea wengine mkuu..ulimkubali huyo mtu ukijuwa kabisa ni mlevi, mimi nikuweke wazi tu niko tayari kuuza chochote ili nikupoteze kama ulivyochangia ndugu yangu kupotea ...
Mkuu kifo kitokanacho na ulevi hakijawahi kuwa na kesi. jamaa kaji peleka mwenyewe kuzimu.
 
Kuna jirani yangu hapa yy siku zote ni kurudi saa nane za usiku,huwa najiuliza kazi zake ndo zinamalizika mda huo au ni nn?,najua anatumia pombe lakini si rahisi mtu kuwa kwenye viringe vya pombe siku zote hadi saa nane za usiku.

Mke wake ni mama wa nyumbani ,sijajua kama huwa anarudi kalewa au laa ila huwa nasikia geti tu linafunguliwa pamoja na sauti ya gari ,na nikitazama mda ni saa nane na madakika ,yani hii ni kila siku
Aisee! Una roho mbaya sana hadi saa nane usiku unasubiri tu ujue jirani karudi sa ngapi, nyie ndio mnaweza mkapeleka umbea kwa mke wake ili wavurugane
 
So sad,RIP.Kwa vyovyote vile huyu mama dhambi aloifanya itamtesa milele,sitaki kutoa hukumu Ila apa akinamama Ina bidi wajifunze maana ndoa ni kiapo na pia mapungufu yapo Kila iitwayo ndoa hakuna ndoa yenye amani tu milele hiyo haipo.
 
jamii forum member tuwe na utaratibu wa kufahamiana au kukutana hata kwa mwaka mara moja na kusaidiana inapotokea ishu kama za kifo au maradhi ,
 
Ndio tatizo la kuficha ID zetu, sasa hata rambirambi hatujatuma. All in all, R.I.P Member.
 
Back
Top Bottom