Anayeshtakiwa kumuua Mkewe adai haogopi Kunyongwa

Anayeshtakiwa kumuua Mkewe adai haogopi Kunyongwa

Sio wote wana bond kiasi hicho. Ebu soma hapa
• Rukilwa alisema kuwa hakudhamiria kumuua mume wake, kwani wakikuwa wanang'ang'ania shoka na mumewe akajikata kichwa kwa shoka hilo.

• Hata baada ya kutoka jela baada ya miaka 24, watoto wake wote walimkataa wakiaminishwa kuwa alimuua baba yao kwa kupenda.

Haina tofaut mzazi yeyeto akimuua mwenza wake ameshatengeneza uadui na wanae.
Ni Kama kaiingizia familia laana
 
Mfanyabiashara Hamis Luwonga mwenye umri wa miaka 38 anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, amedai haogopi kunyongwa hadi kufa wala adhabu nyingine yoyote.

"Kitu ambacho ninakikataa Mhe. Hakimu, ni kuwa niliua kwa makusudi, mimi sikuua kwa makusudi hata ninyongwe leo hadi kufa kwa kile cha kweli, nitaangamia kimwili lakini siyo kiroho, siogopi kunyongwa wala siogopi adhabu yoyote ile lakini ninataka kama nikinyongwa basi ninyongwe kwa haki kwamba niliua bila kukusudia kwasababu ni ajali tu ilitokea"

"Kama shetani angeendelea kunishikilia hadi leo hii, hakuna mtu angejua kitu gani nimefanya lakini roho mtakatifu alinishukia na nilikuwa nasukumwa kusema ukweli kwasababu nilikaa miezi miwili na siku moja bila ukweli kujulikana, hadi sasa Naomi asingejulikana yuko wapi, kutokana na hofu ya Mungu niliamua kusema ukweli siyo kwasababu nilipata mateso kutoka kwa Askari polisi, hapana, ni mimi mwenyewe niliamua"- amejitetea Luwonga kisha akaendelea kujieleza kuwa

"Mhe. Naomba utambue jambo moja, Mawakili wangu ninawaomba wanitetee kwa haki na siyo kupindisha-pindisha mambo kwasababu mimi mwenyewe ndiye niliyeamua kuzungumza ukweli"

Luwonga amemalizia kwa kuiomba Mahakama wamalize kesi yeke kwani Rais na Watanzania wanatamani kujua nini hatima kesi yake kwasababu ilitika nchini mwaka 2019 lilipozuka sakata hilo la kutisha la Luwonga kumuua mkewe kisha kumchoma na magunia mawili ya mkaa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es salaam.
Screenshot_20230704-130636_Facebook.jpg
 
Mfanyabiashara Hamis Luwonga mwenye umri wa miaka 38 anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, amedai haogopi kunyongwa hadi kufa wala adhabu nyingine yoyote.

"Kitu ambacho ninakikataa Mhe. Hakimu, ni kuwa niliua kwa makusudi, mimi sikuua kwa makusudi hata ninyongwe leo hadi kufa kwa kile cha kweli, nitaangamia kimwili lakini siyo kiroho, siogopi kunyongwa wala siogopi adhabu yoyote ile lakini ninataka kama nikinyongwa basi ninyongwe kwa haki kwamba niliua bila kukusudia kwasababu ni ajali tu ilitokea"

"Kama shetani angeendelea kunishikilia hadi leo hii, hakuna mtu angejua kitu gani nimefanya lakini roho mtakatifu alinishukia na nilikuwa nasukumwa kusema ukweli kwasababu nilikaa miezi miwili na siku moja bila ukweli kujulikana, hadi sasa Naomi asingejulikana yuko wapi, kutokana na hofu ya Mungu niliamua kusema ukweli siyo kwasababu nilipata mateso kutoka kwa Askari polisi, hapana, ni mimi mwenyewe niliamua"- amejitetea Luwonga kisha akaendelea kujieleza kuwa

"Mhe. Naomba utambue jambo moja, Mawakili wangu ninawaomba wanitetee kwa haki na siyo kupindisha-pindisha mambo kwasababu mimi mwenyewe ndiye niliyeamua kuzungumza ukweli"

Luwonga amemalizia kwa kuiomba Mahakama wamalize kesi yeke kwani Rais na Watanzania wanatamani kujua nini hatima kesi yake kwasababu ilitika nchini mwaka 2019 lilipozuka sakata hilo la kutisha la Luwonga kumuua mkewe kisha kumchoma na magunia mawili ya mkaa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es salaam.View attachment 2678246
Wanaumme tunapashwa kua na uvumilivu sana ukiamua kuoa wanawake ni mitihani mkubwa.
 
Wakati LULU kwa kosa lile lile yupokitaa maisha yakiendelea
Yule aliyemuua kwa kuchoma moto nyumba aliyomo mchumba ake, ambaye ni kinyozi wa salon? Kule mbezi?? Nikajua kafungwaa tayari jela. Lol
 
Wabongo Tunajifanya tuna hasira za kipumbavu sana, ona sasa anaenda kula tanzi, angelimuacha akatafuta pisi nyengne pengine angekua anakula raha mda huu
 
Kitendo cha kua tayari kwa hukumu yeyote hata kunyongwa hadi kufa,kinaashiria kua mtuhumiwa amekubali kosa lake,na anaona kabisa kua ni haki kuhukumiwa kwa alichokifanya,

Sometimes majuto huja baada ya kitendo but hua ni too little too late.
Sad
 
Ila namsifu jamaa kwa alichoeleza mbele ya mahakama. Naomi alikuwa msumbufu sana hata majirani zake Kigamboni wanakili hilo wazi baada ya hilo sekeseke kutokea 2019.

Duh maskini angejua angehama nyumba angejiepusha na shari wanawake sisi tuna midomo sanaaa huwa tunasukuma wanaume kufanya vitu vya ajabu
 
Duh maskini angejua angehama nyumba angejiepusha na shari wanawake sisi tuna midomo sanaaa huwa tunasukuma wanaume kufanya vitu vya ajabu
Ndio mbadirike sasa Mary, wengine wanatoa machozi kilasiku kwenye maombi wakitafuta ndoa na mwanaume yeyote wengine wanaanzisha vitimbi ndani ya ndoa ili zivunjike.😀
 
Ndio mbadirike sasa Mary, wengine wanatoa machozi kilasiku kwenye maombi wakitafuta ndoa na mwanaume yeyote wengine wanaanzisha vitimbi ndani ya ndoa ili zivunjike.[emoji3]

[emoji3][emoji3]sio rahisi acha tu ni kama shetani anakuvaa mdomo hauwezi kufunga unaongea hatariiii,mtujulie tu hakuna namna
 
[emoji3][emoji3]sio rahisi acha tu ni kama shetani anakuvaa mdomo hauwezi kufunga unaongea hatariiii,mtujulie tu hakuna namna
Kwa midomo yenu hiyo ndiomana wengine hawaishi vizuri bila kulambwa makofi na wanaume zao.🤣🤣
Unakuta unanichokoza kwa maneno makusudi ili mradi tu ninyanyue mkono juu yako kha!😂
 
"Ninataka kesi hii iwe fundisho kwa watu wengi, kwa sababu tulifanya uzembe mkubwa sana sisi wanandoa na jamii pia ilifanya uzembe hadi mauaji yakatokea, alidai Luwonga.
In maana walipopeleka malalamiko kwa ndugu na jamaa waliwadharau au hawakuwapa ushikiano katika kutatua Hilo tatizo, na kweli hili litakuwa fundisho kwa wengi
 
Hakuna kiumbe kipumbavu kama hiki kinachowakilisha hapa. Eti for a man to cheat is okay.. nyie wauaji wakubwa chanzo cha ndoa nyingi kuwa na purukushani ni hamtaki kuona wake zenu wana hela kuwazidi. Mnaskia raha wakishinda wanawaomba kutwa. Mnaanza kuwataftia visa, mna cheat makusudi ili muwakomoe wakiongea mnapata sababu. Huyo kaka apewe adhabu anayostahili
 
Attachments

  • E3646DC7-9ECB-441C-9CA8-AB9533746D26.jpeg
    E3646DC7-9ECB-441C-9CA8-AB9533746D26.jpeg
    136.9 KB · Views: 8
Wana jamii ni wazembe sanaaa !!!watu wa dini ni wapuuzi inshu ikishakua ya uzinzi hakuna Amani tena apo inatakiwa kua mbali mbali tu hawezekani mwanamke alale nje week nzima af anarud ndan same as mwanaume..... tunajamii ya wapumbavu sana wazungu ikifikia ivo hamtakiw kukaribiana kabisa
 
Maisha haya duuuh mtu kapambana kashakua na nyumba zake halafu maisha ya tabu yanafuata kisa mwanamke mtoto wa watu asie damu yenu
 
View attachment 2677118

MFANYABIASHARA Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, amedai haogopi kunyongwa hadi kufa wala adhabu nyingine yoyote.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amedai kuwa anataka "anyongwe kwa haki" kwamba aliua bila kukusudia.

Katika kesi hiyo ya mauaji Na. 4 ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam, anadaiwa kuwa Mei 15, 2019, akiwa Gezaulole, Kigamboni, alimuua Naomi Marijani.

Luwonga alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalira wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dares Salaam baada ya kusomewa maelezo ya mashihidi 28 na vielelezo 14 na upande wa mashitaka.

"Kitu ambacho ninakikataa mheshimiwa hakimu, ni kuwa niliua kwa makusudi. Mimi sikuua kwa makusudi. Hata ninyongwe leo hadi kufa kwa kile cha kweli, nitaangamia kimwili lakini siyo kiroho.

"Siogopi kunyongwa wala siogopi adhabu yoyote ile, lakini ninataka kama nikinyongwa, basi ninyongwe kwa haki kwamba niliua bila kukusudia, kwa sababu ni ajali tu ilitokea," alidai Luwonga.

Hapo Hakim Rugemalira akaingilia akisema: "Unaanza kuhubiri sasa, wewe zungumza unachotaka kuzungumza ili nikiandike kwenye rekodi za mahakama."

Luwonga aliendelea kudai kuwa msingi wa kesi hiyo ni maelezo yake, baada ya kuwaambia polisi kwamba yeye ndiye aliyeua na ndiye aliyekuwa anajitumia ujumbe mfupi kutoka simu ya mkewe kwenda katika simu yake.

"Kama shetani angeendelea kunishikilia hadi leo hi, hakuna mtu angejua kitu nimefanya, lakini roho mtakatifu alinishukia na nilikuwa na sukumwa kusema ukweli. Kwa sababu nilikaa miezi miwili na siku moja bila ukweli kujulikana, hadi sasa Naomi asingejulikana yuko wapi.

"Kutokana na hofu ya Mungu, niliamua kusema ukwell sio kwa sababu nilipata mateso kutoka kwa askari polisi, hapana! Ni mimi mwenyewe niliamua," alidai Luwonga.

Mshtakiwa huyo pia aliiomba mahakama kuwa pindi kesi itakapoanza kusikilizwa, Mahakama Kuu ihamie sehemu ya tukio nyumbani kwake, ili wane mashimo sita aliyoyachimba katika nyumba zake sita na nyumba ya kulala wageni kwa ajili ya maji taka. Alidai kuwa lengo la mahakama kwenda eneo hilo ni ili ione mashimo yaliyochimbwa yalikuwa ni ya maji taka na sio kwa ajili ya kumzika mkewe, kwa sababu yeye ndiye alitaka kwa ajili ya maji machafu.

Ni madai yaliyomfanya hakimu aingilie, akisema: "Sasa mshitakiwa huko unapokwenda ni kwenye ushahidi. Hayo utayazungumza huko Mahakama Kuu katika ushahidi wako."

Mshitakiwa Luwonga alidai: "Mheshimiwa ninaomba ufahamu jambo moja; hawa mawakili wangu nimewaomba wanitetee kwa haki na siyo kupindishapindisha mambo kwa sababu mimi ndiye niliamua mwenyewe kuzungumza ukweli," alidai Luwonga.

Alidai hayo baada ya wakili wake, Mohamed Majaliwa kumtaka aache kuzungumza. Wakili huyo alimtaka wazungumze kwanza wao kabla ya yeye kuendelea kuzungumza mbele ya hakimu.

"Ninawaomba mawakili wa serikali, mnipelekee taarifa zangu kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwamba aharakishe kesi hi lishe haraka kwa sababu hata Rais na jamii kwa ujumla wanataka kujua mwisho wake kwa sababu kesi yangu hii ilitikisa chi.

"Ninataka kesi hii iwe fundisho kwa watu wengi, kwa sababu tulifanya uzembe mkubwa sana sisi wanandoa na jamii pia ilifanya uzembe hadi mauaji yakatokea, alidai Luwonga.

Baada ya mshitakiwa kudai hivyo, Hakimu Rugemalira alimweleza kwamba hakuna kesi kubwa. Zote zinalingana na hakuna kesi inayotikisa chi, hivyo hata kesi inayomkabili "sio konki" kama alivyodai. Mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi 20 na atakuwa na vielelezo wakati shahidi unaendelea. Atavitoa mwenyewe au mashahidi wake watakuja navyo mahakamani.

"Una haki zako za msingi za kupewa wakili na kupewa orodha ya mashahidi, kama utahitaji na mawakili wako hawa wawapo, hilo ni jukumu lako wewe. Kwa hiyo, unahamishiwa kwenda Mahakama Kuu," alisema Hakimu Rugemalira.

Luwonga anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na baadaye alichukua majivu ya mwili wa marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga mkoani Pwani.

===

Kwanza nianze kuwapongeza wanandoa mliopo mkoa wa Da resalaam. Maana Kwa mujibu wa msajili wa taraka kutoka Nida mkoa unao ongoza Kwa taraka nyingi ni mkoa wa dare salaam.

Ndugu zangu GAZETI la nipashe la Tarehe 3/07/2023 limeandika habari ya Mauaji ya Naomi vizur sana Kona ya habari za mahakamani. GAZETI limeripoti yakuwa Mwanaume aliyemuua Naomi Kisha kumchoma moto alimchoma Kwa magunja mawili ya mkaa.

Pili kichwa Cha mkewe kiliwai sana kuungua maana alikuwa anakigeuza. Tatu amedai Tako lilikuwa na mafuta mengi. Nne sehemu za Siri za Naomi zlikuwa na mafuta. Tano matiti pia yalikuwa na mafuta.

Sehemu zote zilizokuwa na mafuta zilichelewa kuungua ila zilisaidia moto kukolea.

Zingatio;
Mshitakiwa anadai alikuwa na mgogoro wa ndoa na mke wake takribani miaka miwili hawakushirki tendo la ndoa,na Kila mmoja alikuwa analala chumba chake.

Ilifikia hatua Kila mmoja akawa anatoka na kulala nje ya ndoa PASIPO kuulizana au kuagana.

Naomi aliwai kumkata mmewe Kwa kisu na mme alishafika polisi mara kadhaa KULALAMIKA lakini polisi walimfukuza Kwa kumwambia atoke hapo huyo ni mkewe wao hawaingilii ndoa za watu.

Naomi aliwai mvuta mmewe sehemu Siri Tena Kwa nguvu mbele ya mama yake na mwanaume.

Naomi aliwai mpiga mmewe na ndoo ya chooni.

Mara ya mwisho jamaa akirudi kwake asubuhi na kukuta Naomi anamwandaa mtoto aende shule, jamaa aliweka simu yake mezani ilipoita Naomi akaishika na kumpelekea mmewe ukubakimwambia pokea simu za Malaya wako.

Mwishowe wakaanza kugombana Naomi akakimbilia kushika uboo na PUMBU zake Kwa nguvu,mume nae kujiami akampushi, puuuuuu! Laalura! Naomi akadondokea ukuta wa bafu na kudodondekea kichwa na kufa pale pale baada ya damu nyingi kuvujia kichwani.

Baada ya kifo mume akawaza akazike apo apo?itakuwa shida,apeleke Mwili shambani akazike, akaogopa Trafiki, mwishowe akaamua kuuchoma Mwili Ili akazike majibu ya Mwili huo shambank kwake.

ujumbe ndoa kama za Naomi na mwenzake ziko ngapi Kwa Sasa?

Je, kama polisi wetu wangeingilia kati haya yote yangetokea?

Ndoa sio msaafu shekhe!.
Pili kichwa Cha mkewe kiliwai sana kuungua maana alikuwa anakigeuza. Tatu amedai Tako lilikuwa na mafuta mengi. Nne sehemu za Siri za Naomi zlikuwa na mafuta. Tano matiti pia yalikuwa na mafuta.

Sehemu zote zilizokuwa na mafuta zilichelewa kuungua ila zilisaidia moto kukolea.[emoji848][emoji2827][emoji1544]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom