Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya mshtakiwa katika kesi Namba Cc.5866 /2024, Baraka Benedicto anayedaiwa kumlawiti mtoto kushindwa kutoa utetezi wake siku ya Februari 26, 2025 akitoa sababu mbele ya Mahakama kuwa anaumwa, jana Machi 3, 2024 shauri hilo limetajwa, ambapo alipopewa nafasi ya utetezi amesema hana lolote la kueleza, hivyo anaiachia Mahakama.
Kufuatia mshtakiwa kueleza hayo, Mahakama kupitia Hakimu Nabwike Mbaba imeahirisha shauri hilo mpaka Machi 7, 2025.
Ikumbukwe Baraka Benedicto alipandishwa mahakamani baada mdau wa JamiiForums kudai kwamba kulikuwepo na mazingira ya danadana ya kutomfikisha Mahakamani mtuhumiwa (Baraka) ambaye inadaiwa akiwa anatekeleza majukumu ya ulinzi katika Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi-Sinza ambapo ilidaiwa alimfanyia ukatili wa kumlawiti mtoto wa kiume kwenye vyoo Parokia hiyo.
Kesi hiyo inayosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni awali ilianza kutajwa mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira lakini baadae ilihamishiwa kwa Hakimu Nabwike Mbaba ambaye anaiendesha hadi sasa.
Ikumbukwe, kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 2024 siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuomba Mamlaka kuchukua hatua kumsaidia mtoto husika.
Vilevile itakumbukwa mshtakiwa Baraka Benedicto alikana shtaka la ulawiti alilosomewa alipofikishwa mbele ya Mahakama.
Pia soma
~ Mlinzi wa Kanisa (Sinza, Dar) aliyeshtakiwa kwa kumlawiti mtoto kwenye vyoo vya Kanisa, atupwa jela Miaka 30
~ Anayetuhumiwa kulawiti Mtoto kwenye Vyoo vya Kanisa ashindwa kutoa Ushahidi, adai anaumwa, kesi yaahirishwa hadi Machi 3, 2025
~ Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza
~ Dar: Mlinzi wa Kanisa anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto Muimba kwaya kwenye vyoo vya Parokia apandishwa kizimbani
~ Tukio la Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kudaiwa kumlawiti Mwanafunzi, Padri asimulia kilichotokea
~ Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie