Anayezijua hoja za Mbowe zilizompelekea kugombea tena nafasi ya uwenyekiti wa chama aziweke hapa tuzijue

Anayezijua hoja za Mbowe zilizompelekea kugombea tena nafasi ya uwenyekiti wa chama aziweke hapa tuzijue

Hoja zake ni:
1. Chama hakiko salama hivyo hawezi kukiacha. Ukimuuliza, hakiko salama kwenye mikono ya nani? Hakuna jibu?

2. Wenyeviti waliomtangulia , waliachia kiti wakiwa na miaka 68. Yeye bado miaka 5 afikishe umri huo.

3. Yeye sio mbangaizaji. Hawezi kukiacha chama kwa wa Wabangaizaji kama muuza Bamia wa Mbutu.

Hizo ndizo hoja kuu za mh.
Sasa ZERO atakuwa na Hoja!!
Kazi kweli kweli
 
Kama TAL hatoshi kwanini walimpa fomu za kugombea urais? Ina maana angekua Rais ingekuaje sasa? Kama walijua hatoshinda je ina maana Chadema haipo serious na mageuzi?

Kingine Mbowe kama anaona Lissu hafai kwanini haku mentor viongozi wengi zaidi ili leo awaachie uenyekiti?

Likewise, matumizi ya busara za Mbowe kati ya 2016-24 yalisaidia nini? Mbona hayakuzuia CCM kupora viti vyote chaguzi 3 mfululizo? It's obvious diplomacy imefeli tunahitaji radicalism ili nayo tupime kama inafanya kazi. Hatuwezi tegemea busara milele wakati tunaona wazi kabisa hata mwakani watapora majimbo yote na Mbowe atabaki analilia maridhiano
1: Chadema ilipomteua TAL kugombea urais 2020 walijua wazi hawezi kushinda uchaguzi huo na kua rais dhidi ya utawala uliokuwepo,,walichotazama ni nani anaweza kuipatia Chadema kura nyingi za urais ili zisaidie kupata wabunge wengi wa viti maalum.

2: Chadema inao watu wengi wasomi na wenye uwezo wa kushika uongozi wa nafasi ya mwenyekiti lakini sio wote

3:uchaguzi huru na wa haki hautegemei ni nani mwenyekiti Chadema,,, toka mfumo wa vyama vingi uanze kumeshapita viongozi wenye nguvu kuliko TAL.
 
Chadema ilipomteua TAL kugombea urais 2020 walijua wazi hawezi kushinda uchaguzi huo na kua rais dhidi ya utawala uliokuwepo,,walichotazama ni nani anaweza kuipatia Chadema kura nyingi za urais ili zisaidie kupata wabunge wengi wa viti maalum.
Ingawa unapotosha maana nachojua kura za wagombea ubunge ndio huletq viti maalum. Tanzania tunatumia D'hondt method of proportion kwa threshold ya 5% ya kura zote za ubunge ili uwe eligible kupata viti.maalum. kura za urais zinasaidia walau 30% ya ruzuku kupatikana.

Anyway tukirudi kwenye hoja, Sasa logic hii hii itumike kumuweka Lissu maana ndio mtu pekee ana ushawishi upinzani, so atasaidia tupate wabunge, viti maalum na ruzuku nyingi zaidi!! Pia ana upeo mkubwa ataendesha chadema kitaalamu sana.

2: Chadema inao watu wengi wasomi na wenye uwezo wa kushika uongozi wa nafasi ya mwenyekiti lakini sio wote
Mbona sasa ame endorse Wenje agombee uenyekiti, yaani kweli wenje ndio awe second in command? Hivi mbona ni vituko.

3:uchaguzi huru na wa haki hautegemei ni nani mwenyekiti Chadema,,, toka mfumo wa vyama vingi uanze kumeshapita viongozi wenye nguvu kuliko TAL.
Si kweli, enzi za Dr Slaa mbona CCM tuliheshimiana sana alikua mtu wa kazi sio busara busara. Tunapaswa tumpate Lissu ili awaweke CCM kwenye defensive mode muda wote naamini itarudisha morale ya nguvu ya umma kama ile 2010-2015 hata CCM wakiiba wataiba kistaarabu sio kama huu uhuni unaoendelea maana wanajua Mbowe atacheka cheka tu.

Enough is enough, wakimpa Mbowe chama ndio tumekwisha kabisa.
 
Chama hakipo salama kwenye mikono yake mwenyewe 😂 uzuri anajua kuwa yeye ndio mhusika wa kutokuwa salama
Anaropoka ropoka tu sijui konyagi ndizo zilihutubia? Ati si vema kubadilisha mwenyekiti wakati uchaguzi ni mwakani.

Hivi kwa jinsi ccm walivyomzowea kama nguo zao za ndani mwakani kutakuwa na uchaguzi kweli? Yale yale ya serikali za mitaa yatafanyika.

Jingine anasema yeye ni mfanyabiashara HABANGAIZI. Hivi kweli maneno ya nyodo kama hayo yanaweza kunenwa na mtu mwenye akili timamu?
 
Ingawa unapotosha maana nachojua kura za wagombea ubunge ndio huletq viti maalum. Tanzania tunatumia D'hondt method of proportion kwa threshold ya 5% ya kura zote za ubunge ili uwe eligible kupata viti.maalum. kura za urais zinasaidia walau 30% ya ruzuku kupatikana.

Anyway tukirudi kwenye hoja, Sasa logic hii hii itumike kumuweka Lissu maana ndio mtu pekee ana ushawishi upinzani, so atasaidia tupate wabunge, viti maalum na ruzuku nyingi zaidi!! Pia ana upeo mkubwa ataendesha chadema kitaalamu sana.

Mbona sasa ame endorse Wenje agombee uenyekiti, yaani kweli wenje ndio awe second in command? Hivi mbona ni vituko.

Si kweli, enzi za Dr Slaa mbona CCM tuliheshimiana sana alikua mtu wa kazi sio busara busara. Tunapaswa tumpate Lissu ili awaweke CCM kwenye defensive mode muda wote naamini itarudisha morale ya nguvu ya umma kama ile 2010-2015 hata CCM wakiiba wataiba kistaarabu sio kama huu uhuni unaoendelea maana wanajua Mbowe atacheka cheka tu.

Enough is enough, wakimpa Mbowe chama ndio tumekwisha kabisa.
Ni kweli comrade nilipotoka hapo, nilichotaka kuandika ni ruzuku,,,pengine kichwani nilikua nawaza viti maalum.

Hata Mimi ninapenda Mbowe ang'atuke ili Chadema kisiwe chama cha mtu mmoja.

Hebu jifanye wewe ndio TAL tueleze utafanya nini hadi serikali iliyopo madarakani ikuogope na hivyo ihakikishe uchaguzi unakua huru na haki?

Umetoa mfano wa Dr Slaa,, siamini kama yeye ndio sababu ya uchaguzi angalau kuonesha dalili ya kuwa uchaguzi huru na wa haki, ila ni uongozi uliokua madarakani wakati huo,,,hata mwaka 2015 Chadema ilipata wabunge wengi na kura nyingi za urais, lakini Chadema hiyohiyo ilipoteza viti vingi na sababu kuu ni utawala uliokua madarakani wakati huo.

Ili TAL alete maajabu ni kama ataweza kushawishi kundi kubwa la watu wenye nyadhfa kutoka chama tawala wahamie Chadema tofauti na hapo ataishia kupiga kelele tu.
 
Sera yake ni;
1.Kutaka aiache Chadema salama. Unajiuliza kwani haiko salama chini ya nani?
2. Afikishe miaka 68 kama watangulizi wake. Hoja ya kipuuzi kabisa

Lakini Lissu kaweka mkeka wa hoja, ukiusoma unabaki kuangalia mawinguni labda utamuona Lissu
Hoja yake nyingine ni kwamba:-
Ametumia fedha zake nyingi sana pale chadema
 
Anahitajika sana kwenye siasa za vyama vingi hapa nchini. Huwezi ukakiacha chama mikononi mwa wanaharakati ambao hawatambui mchango wa maridhiano na siasa za maelewano. Lissu na wanachama wengine wanapenda sana nguvu badala ya makubaliano. Sasa hapo unaweza kweli kuachia ngazi ili tu ufurahishe haohao wanaobeza juhudi zako?
Hayo makubaliano ndio yamekufikisha kwenye kutekwa kudhulumiwa uchaguzi na kuumizwa kuuliwa nk. Tumia hata comon sense ulizopewa na Muumba wako
 
Back
Top Bottom