Anayosema Kigwangalla kuhusu uaminifu wa Watanzania kuna tatizo?

Ndio ukweli huo halisi nakuambia. Either uufuate ufanikiwe ama ubaki kulalamika.
Eg: crdb,nmb,tbl,tcc,nk kampuni hizo wanaofanya kazi ni vijana wazungu ama wajapani? No ni watanzania, ishu ni system hakuwa nayo. Kwa capital yake hakutakiwa kuwa mchuuzi. 100% blaming ni juu yake
Haya basi Sawa mtaalam
 
Leo asb Hamisi Kigwangalla ameliamsha tena huko Instagram suala la uaminifu wa watanzania. Amehadithia alichofanyiwa na kijana aliyemuamini. Huko nyuma amewahi kuuliza WHAT IS TANZANIA'S COMPETITIVE ADVANTAGE -Akimaanisha nini ambacho tunaweza kusema hichi kinatutambulisha kitaifa.

Juzi kati I-SOKO mfumo wa kuwezesha wanawake kufanya biashara afrika mashariki imeanzishwa. Kilichojiri malalamishi kwamba watanzania hatuaminiki.

Kihehe tunasema sema we have a people problem. Tatizo ni kubwa lakini tunaogopa kulijadili kwakuwa ni kaa la moto. Au halipo

SOMA KISA HIKI KUTOKA KWA hamis Kigwangalla

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 1:

Kama ukiona elimu ni gharama, ujue haujajaribu ujinga. Vile vile, kama ukiona kutafuta utajiri ni kazi, hebu jaribu umaskini uone.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama umaskini. Tuliouishi umaskini tunaujua. Tukipambana nao kwa kila hali msitushangae. Mara kadhaa tushawahi kurudi nyumbani for lunch na kukuta hakuna kilichopikwa tukaishia kunywa maji na kugeuza shule, maana hata wa kumuuliza chakula kiko wapi hayupo home.

Kutajirika ni katika vitu vigumu kabisa kufanya hapa duniani. Niliwahi kujaribu kutafuta utajiri sikuufikia, nikaishia hapa nilipo! Lakini bado napambana. Si haba, WALLAH sina malalamiko yoyote yale kwa Allah, zaidi zaidi narejesha shukrani tele. Nilipotoka napajua mwenyewe.

Kwenye safari ya kutafuta maisha, kwa kuwa nilikuwa na mbio ndefu na za spidi sana, nimejifunza mengi sana. Huwa najaribu kuandika andika hapa, wenye muda husoma na pengine hujifunza.

Niliwahi kuwa nalima ekari 500 - 600 kwa msimu, nikamuamini kijana wangu mmoja mahiri, mchapakazi, mwenye dini kweli kweli, mwenye elimu na passion ya farming; pamoja na kunifaidisha na kunipa tamaa ya kuwekeza zaidi, alinipiga kweli kweli!

Nikaamini wadogo zangu damu kabisa, wakanipiga. Nikazama. [emoji30]!

Mtaji wa zaidi ya ekari 700 ukaporomoka mpaka ekari 100/200. Wakati unaporomoka, unadaiwa na benki ulipe mkopo wa mtaji uliochukua, unadaiwa na kampuni waliokukopesha matrekta, combine harvesters, planters, unadaiwa na suppliers wa pembejeo etc. Inaendelea…

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE. Part 2!

Wakati huo huo umeshushwa cheo na unaambiwa ukajibu hoja kwa CAG za dhambi ambazo hazikuhusu. Faida moja ya cheo ni kuwa kuna mikopo bankers wanakupa kwa kukuamini tu, tena kwa simu tu. Siku kikiondoka, wadai wote wanaanza kuhaha kukudai kama hawakujui vile. Wakubwa wote hawapokei simu zako. Unabaki peke yako kama siyo wewe vile. Marafiki waliokuwa wanakusalimia kila kukicha hawapokei simu zako wala hawajibu meseji zako.

Ukiwa na roho ndogo utasema umerogwa ama utaugua ugonjwa wa akili. Ama hata utaona maisha hayana maana tena.

Wakati unajaribu kutoka, bei za mazao zinaporomoka! Vita ya Ukraine inaanza na COVID inapandisha bei za mbolea etc.

Mwaka huu bei za mazao nzuri, wanatokea kwelea kwelea [emoji3].

Ili kusimama kwenye maisha, muombe sana Mungu akupunguzie masomo magumu ya kupitia, aidha usihangaike sana kuimarisha misuli ya mwili ili ukivaa suti upendeze, imarisha misuli ya moyo, ubongo na roho(kama nayo ina muscles![emoji3]) ili uweze kukabiliana na nyakati za maanguko. Siku zote jua tu kwamba, baada ya maanguko kadhaa, na kama utaweza kuinuka kila unapoanguka, na kustahimili maumivu ya kila anguko, mwangaza huja na Mungu humuinua mja wake! (Graduation hiyo sasa!)

Maisha ni Marathon. Kutajirika siyo rahisi. Lakini kwani nani alisema umaskini ni raha?

Iendelee ama iishie hapa?

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 3.

Ukitenda wema, tenda kwa watu wengi sana, muhimu ni kuwa usingoje shukran. Kwa hakika wema, ni akiba isiyooza.

Pamoja na uwepo wa watu wengi wa hovyo kwenye maisha yetu, watu ambao hawawezi kukufanyia jambo jema, zaidi zaidi wanajipanga kukuangusha na kukudhuru kila kukicha, tena hawana sababu yoyote ile, huwa wapo watu wachache wema, pengine uliwahi kuwatendea wema basi wanakumbuka ama ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda wema tu. Wapo!

Wabaya wengi wapo lakini wema wachache pia wapo. Jitahidi uwe miongoni mwa wema.

Kwenye maisha yako jitahidi kuwatendea watu wema, bila sababu, hujui nyuma ya tabasamu la mtu aliyekuja mbele yako kuna nini anapitia!

Kuna mtu mmoja alipataga kesi ya uhujumu uchumi, sikuwahi kuwa namjua, wala hakuwa rafiki yangu, na wala namba yake ya siku sikuwa nayo.

Nikaona mambo kwenye mitandao, nikafuatilia nikaona anaonewa tu, bila sababu. Nikaingilia kati kumtetea. Siyo kwa sababu yoyote ile, bali kwa kutamani kuona anatendewa haki.

Nilipoingia nikaambiwa ni maelekezo kutoka juu. Juu kuna Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu. Nikapiga moyo konde nikamuendea hewani bwana mkubwa; akaniuliza swali moja tu “umehongwa shilingi ngapi?” Nikamuambia Mhe. Rais, utakuwa umeshauriwa vibaya, kama unaniamini mimi mshauri wako unisikilize nikupe taarifa yangu kisha utume watu wako wafuatilie, mimi hata huyu mtu simjui na wala sijawahi kuwasiliana naye hata mara moja! Akakata simu.

Baada ya muda kidogo ukweli ulifika mezani kwa bwana mkubwa, akanipigia akasema ulisema kweli. Umenifurahisha. Yule bwana alikuja akaachiwa. Akaja akajua ushiriki wangu kwenye jambo lake. Akanishukuru sana. Akataka kunipa chochote nilikataa. Tukawa marafiki.

Siku moja baadaye kabisa, hapo nishatoka kwenye serikali, napambana na miradi yangu, hali yangu ngumu, sina kitu, naingiza kontena za kiwanda changu akajua akaniita, basi akalipia nusu ya gharama zote za kontena zangu!

Hakujua ni kiasi gani nilikuwa hoi! Usiku nilitafakari sana jambo lile hadi machozi yalinitoka. Niliswali rakaa mbili kumshukuru MUNGU…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 4.

Kila kitu kitapita. Hata uwe unapitia kipindi kigumu namna gani, jua tu kipindi hicho kitapita. Kama upo kwenye raha namna gani, jua tu zitaisha. Hakuna kinachodumu milele chini ya jua. Kila kitu kitapita. Kuna miamba, majabbar anidi, ilipita! Iko wapi leo hii?

Basi, maneno haya yatoshe kutunyenyekeza, kutushusha na kutukumbusha kuwa watu wema zaidi ya wabaya.
Mimi Nina kanuni moja kwenye maisha yangu; kama ni kuonewa, basi acha nionewe mimi, lakini siyo mimi nionee mtu mwingine. Kama ni kudhulumiwa, acha nidhulumiwe mimi lakini siyo mimi kumdhulumu mtu. Huwa naamini wema ni akiba isiyooza lakini ubaya ni deni lisilofutika! Ubaya utakurudia tu.

Watu kama mimi huchukuliwa kama watu imara na wagumu kweli kweli, na wenye mamlaka makubwa sana, kwamba tunaweza kufanya lolote na kumfanya mtu chochote, lakini amini nakuambia binafsi nimeonewa na kudhulumiwa mara nyingi na wengine kuliko unavyoweza kudhania.

Kuna kijana wangu mmoja, na wapo wengi, sema ntatolea mfano huyu mmoja, aliwahi kunipiga parefu sana. Kwa mara ya kwanza nililia machozi ya uchungu sana mbele ya wanangu. Na mbele ya mama yangu, nikiwa mtu mzima!

Tumelima, tumejaza stock kwenye magodown yetu na ya kukodi. Tumetazama soko tukajua bei zitapanda, tukanunua na mzigo mwingine kwa wakulima wengine tukatunza. Kwamba tutauza baadaye bei zikipanda. Biashara ya mazao siyo rocket science, ukiwa na mtaji tu, ukatunza stock siku bei zikipanda unauza kwa faida unatengeneza pesa nzuri.

Kumbe dogo ananiambia amepata mzigo wa kutosha, natuma hela, kumbe ananunua kidogo, anamhonga store keeper, wanaweka rekodi sawa, dogo anakula hela. Uko zako mjini, busy na majukumu ya serikali, unajenga nchi! Simu inaita tena baada ya siku tatu, unaambiwa kuna mkulima mwingine mkubwa anauza mzigo wake, unapiga kadhaa, unakopa hela unasukuma kwenye stock!

Kumbe unanunua Moet, VSOP etc. Dogo anafunga bar, anaagiza slay queens kutoka Dar, anawapa bata la hatari!

Dogo umempa gari, Nissan Patrol, matrekta, combine harvesters na mashine zote, na mamlaka ya kusimamia kampuni yako, basi anatukana na kuchimba mkwara kila mtu kwa jina lako! Inaendelea…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 5.

Anaogopwa kuliko hata unavyoogopwa wewe mwenyewe! Hakuna anayekupa taarifa na wewe uko busy na ujenzi wa Taifa!
Kumbe Taifa lako binafsi la Kigwangalla Corporation linaangamia! [emoji24][emoji174]

Wakati wa kulima, dogo anakupa hesabu ya kulimia ekari 400, kumbe amelima ekari 300. Ekari zako 100 amewakodishia watu wengine wanalima, halafu wewe anakuletea hesabu za mahitaji ya ekari zote 400 wakati wote - kuanzia mbegu, mashine za kulimia, kuvuruga, vibarua wa kupanda, madawa, mbolea, palizi, kuvunia, usimamizi.

Mwishoni kule anakupa hadi na idadi ya gunia alizovuna na kutunza godown. Hesabu yake na hesabu ya store keeper ziko sawa.

Bei zinaanza kupanda, wewe unachekelea unajua huu ndiyo ule mwaka wangu wa kupiga hela ndefu, ntanunua na G Wagon yangu (my dream car), ntajenga na ile lodge yangu, na zile apartments zangu! [emoji3]. Ntalipa na madeni yangu yote ya mikopo, nitaongeza uwekezaji wangu kwenye hisa na T-bonds! Kumbe maskini unajenga zako magorofa hewani! [emoji24][emoji25][emoji174] ushapigwa!

Mtu mmoja akaniambia amekutana na ‘mdogo wangu’, yule anaitwa Kigwangalla, anayesimamia miradi yangu ya mashamba alikuwa club na warembo (ni maarufu sitowataja majina!) akampa offer! Nikashtuka.

Nikamcheki dogo, nikamuambia nimepata salamu zake. Nikaona nimtume kijana mmoja wa ofisini kwangu Dar, na mke wangu, wakakague stock. Akasikia kuwa wanakuja. Akaanza mbinu na wenzake, eti wachome godown ili kupoteza ushahidi! [emoji174][emoji24][emoji30]

Anayetoa hizo taarifa ni mdada mmoja ambaye alikuwa rafiki wa mwamba, kumbe alimsikia akiongea kuhusu madumu ya petrol kumwagwa usiku kwa akili sana ili kupoteza ushahidi. Kwamba, kwanza wangetoa mpunga zaidi kutoka godown, wabakishe kidogo, halafu kwa kuwa huwa tunamwaga pumba za mpunga kwenye sakafu, wakinyunyiza petrol kidogo tu moto utakuwa mkali sana kiasi kwamba hautoweza kuzimika, kila kitu kitateketea!

Huyo dada akasikia huruma sababu alijua wizi waliokwisha kunifanyia halafu wakichoma tena hicho kidogo, wachome na godown langu, na ndani humo Kuna mashine zangu zote - trekta kubwa3, stock ya mbolea, madawa… #HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 6.

…madawa ya mimea na combine harvester, itakuwa mbaya sana! Akamuambia ndugu yangu mmoja.

Ndugu akanitafuta toka asubuhi, wapi! Siku hiyo nilikuwa Ikulu kwenye cabinet, mule hamuingii na simu. Tumetoka, naingia kwenye gari, la kwanza kuwasha simu, nakutana na meseji Lukuki! Baada ya mimi kukosekana jamaa zangu waliamua kuripoti polisi, ulinzi ukawekwa!

Nilisikia kama nimechomwa kitu moyoni. Machozi yalinitoka bila kupigwa! Bila kutoa sauti. Sitokuja kusahau.

Nilifika nyumbani nikamkuta mama yangu sebuleni, niliangua kilio kama niliyefiwa na mtoto ama mzazi. Katika ukubwa wangu, nimewahi kufikwa na mambo mengi, lakini sijawahi kulia hata siku moja. Siku hii nililia bila kujali wanangu wanatazama wala nini. Mama yangu alinikumbatia kwa nguvu na kunituliza.

Nilijiuliza sana nimemkosea nini huyu dogo? Na wenzake? Mpaka leo sijawahi kupata majibu ya maswali yangu. Vijana wa kitanzania mna la kujifunza hapa. Huyu dogo na wenzake niliwapa gari ya kutembelea, mapikipiki, mashine ambazo wakimaliza kufanya kazi kwangu wanakodisha kwa wengine wanapata hela ya kula na matanuzi (ambayo mimi siichukui), kila kijana mmoja nalipia gharama ya kuanzia kumlimia na kumtunzia shamba lake; ekari 30 (huyo mkubwa wao), ekari 15 wale wasaidizi wake wawili. Kwenye ekari 15 unapata kati ya 30 - 40m kwa mwaka. Matukio ya hivi ni mengi kwenye story za wajasiriamali wengi hapa nchini.

Vijana wanadanganyika sana na maisha ya superstars, wanataka wayaishi bila jasho. Wengine wameishia kujidhalilisha na wengine wamefikia hata kushikishwa ukuta! Kama huna kipaji mdogo wangu, usitamani maisha ya wenye navyo. Fanya kazi kwa bidii, jipe muda wa kujitafuta, na wa kutafuta nafasi yako maishani. Ukifika utakula maisha yako ya halali kabisa.

Usikubali kuingia kwenye kundi la vijana wanaotafuta ajira lakini hawataki kufanya kazi. Wala usilikurubie kundi la vijana wanaotafuta ajira ili wakapige deal! Kila kijana anataka awekwe kitengo chenye ‘michongo’! Jamani nchi haijengwi namna hiyo. Hela haitafutwi namna hiyo. Nakuhakikishia, hela ya hivyo ukiipata haitokaa. Itakimbia tu.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIBA UBORA WAKE! Part 7.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani kuwa kama mimi, basi nikuambie ukweli kuwa mimi najiona ‘Muomba Allah’ tu, sijafika popote na kiukweli hata hapa padogo nilipofikia, siyo kwa madili, dhulma, ubadhirifu na wala siyo kazi rahisi. Uwe tayari kutokwa machozi, jasho na damu!

Halafu; kwenye maisha yetu pesa, vitu, vyeo havileti furaha ya kweli, na wala havina thamani ya kweli. Vitu vyote vyenye thamani ya kweli kwenye maisha huwa havishikiki na havinunuliki. Usipoteze utu na imani yako kutafuta vitu vinavyoshikika.

Swali la ‘what did I do to deserve that?’ Halijawahi kunitoka. Usiulize huyu dogo mengine ya kijamii niliyowahi kumfanyia ni mangapi? Sema sipendagi kusema wema niliofanyia watu, Ila jua tu nilim-treat kwa heshima kupindukia, harusi yake niliwekeza na kuisimamia zaidi ya nilivyofanya kwa mdogo wangu niliyemuachia ziwa la mama!

Imagine rafiki zangu walivyojitoa, hata sijawahi kuwaambia dogo alivyoninyoosha! Dan La Kairo alitoa Range Rover yake mpya Autobiography kumpa dogo akajiendesha na mkewe! Miaka mitatu tu baadaye anataka kuchoma mali yangu! Dah! #HK #Fighter #NjeYaBox Iendelee ama tuishie hapa kwa sasa?
Ile kauli ya " @ Soma ule nchi" ilitengeneza wezi wengi sana katika nchi hii.

Wanasiasa walitengeneza wizi na ujanja ujanja kuwa mfumo rasmi wa maisha ya watanzania.

Aliyeko serikalini anaibia serikali, aliyeko kwa mhindi anamuibia mhindi, aliyeko kwenye biashara ya mume wake anamwibia mume wake, aliyeko kwenye biashara ya baba yake anamuibia baba yake.

Wanasiasa ndiyo walitengeneza kizazi cha namna hii kuwa utajiri unapatikana bila kufanyia kazi na ukiwa serikalini unapaswa kuishi nche ya kipato chako matokeo yake ndiyo haya.

Watanzania hawaaminiki kwa lolote bila kujali elimu zao, umri wao na nyadhifa zao, achilia mbali imani zao.

Tunatengeneza jamii ya isiyo na maadili lakini pia isiyo utashi wa kufanya kazi.

Hivi leo ni mtanzania yupi unaweza kumnyooshea kidole kuwa mfano bora kwa watu kwenye hili Tabaka la juu ?

Anachokilalamikia Kigwangala ni kitu kiko wazi tu hata kwa yeye mwenyewe uadilifu wake unatia mashaka sana. Anataka apate paka katika kizazi cha panya ? Anajidanganya panya hawezi kuzaa na kulea paka.

Kizazi hiki kisicho na maadili yoyote kilitengenezwa na siasa isiyojua kesho ya jamii yake.
 
Ukitafsiri hadith ya HK kwa lugha yeyote ile halafu ukatafuta gugu au search engine yeyote ile kwa kutumia part(sehemu yeyote ile) katika hiyo hadithi;utakutana na stori kama hiyo Duniani kote! Yaani utaweza kudhani ame kwapua na kubandika(copy and paste) vile kwa kufanana fanana na stori zingine.

Hakika yamemkuta, na ninawajua wengi kama HK. Mhindi, Mzungu, Mkenya wote have something in common, nayo ni lack of trust..hawana wakuwaamini kwa 100% kwa lugha nyingine nyepesi tu ni Uaminifu(trustworthiness) ni hulka ya binadamu. Watu wote bila kujali dini rangi nchi au jinsia yake...Hivyo basi kuwapachika Watanzania kwa ujumla kuwa hawaaminiki ni kosa kubwa sana. Tupnuguze kujishusha chini kiasi hicho na kuwaacha hawa wapotoshaji kama huyu ninayemnukuu ambaye anadai ni sababu za "Ujamaa"
Mbongo ukimpa kazi kitu cha kwanza akilini mwake ni atakuibiaje. Na kwa ujinga linaenda kwa mganga eti usifurukute!!! Ujamaa tuliopitia ndiyo umezaa hii tabia ya wizi.
....ipo siku weye huo uwakili wako utakapo kurudia... karma will devour you, hiyo tabia unayotaka kutumia kuwatukana Watanzania kila kukicha itakumaliza vilivyo. Ulaaniwe kwa jina la Mungu. Ulegee na ushindwe.
 
Mtu mwenye kampuni top management unakuta white people....ukimpa Mbongo kampuni inakufa...totally...ni ukweli mchungu na mbaya ila ni kwl
Top management ni kwa ajili ya kulinda interest, mfano crdb ,nmb,uba,etc etc, na hao top management hawatumiwi pesa ovyo kama alivyokuwa anafanya kigwa, wanakuta kuna rules za kufuata,ukikiuka unafukuzwa kazi. Suala ni misingi.
 
Leo asb Hamisi Kigwangalla ameliamsha tena huko Instagram suala la uaminifu wa watanzania. Amehadithia alichofanyiwa na kijana aliyemuamini. Huko nyuma amewahi kuuliza WHAT IS TANZANIA'S COMPETITIVE ADVANTAGE -Akimaanisha nini ambacho tunaweza kusema hichi kinatutambulisha kitaifa.

Juzi kati I-SOKO mfumo wa kuwezesha wanawake kufanya biashara afrika mashariki imeanzishwa. Kilichojiri malalamishi kwamba watanzania hatuaminiki.

Kihehe tunasema sema we have a people problem. Tatizo ni kubwa lakini tunaogopa kulijadili kwakuwa ni kaa la moto. Au halipo

SOMA KISA HIKI KUTOKA KWA hamis Kigwangalla

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 1:

Kama ukiona elimu ni gharama, ujue haujajaribu ujinga. Vile vile, kama ukiona kutafuta utajiri ni kazi, hebu jaribu umaskini uone.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama umaskini. Tuliouishi umaskini tunaujua. Tukipambana nao kwa kila hali msitushangae. Mara kadhaa tushawahi kurudi nyumbani for lunch na kukuta hakuna kilichopikwa tukaishia kunywa maji na kugeuza shule, maana hata wa kumuuliza chakula kiko wapi hayupo home.

Kutajirika ni katika vitu vigumu kabisa kufanya hapa duniani. Niliwahi kujaribu kutafuta utajiri sikuufikia, nikaishia hapa nilipo! Lakini bado napambana. Si haba, WALLAH sina malalamiko yoyote yale kwa Allah, zaidi zaidi narejesha shukrani tele. Nilipotoka napajua mwenyewe.

Kwenye safari ya kutafuta maisha, kwa kuwa nilikuwa na mbio ndefu na za spidi sana, nimejifunza mengi sana. Huwa najaribu kuandika andika hapa, wenye muda husoma na pengine hujifunza.

Niliwahi kuwa nalima ekari 500 - 600 kwa msimu, nikamuamini kijana wangu mmoja mahiri, mchapakazi, mwenye dini kweli kweli, mwenye elimu na passion ya farming; pamoja na kunifaidisha na kunipa tamaa ya kuwekeza zaidi, alinipiga kweli kweli!

Nikaamini wadogo zangu damu kabisa, wakanipiga. Nikazama. 😩!

Mtaji wa zaidi ya ekari 700 ukaporomoka mpaka ekari 100/200. Wakati unaporomoka, unadaiwa na benki ulipe mkopo wa mtaji uliochukua, unadaiwa na kampuni waliokukopesha matrekta, combine harvesters, planters, unadaiwa na suppliers wa pembejeo etc. Inaendelea…

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE. Part 2!

Wakati huo huo umeshushwa cheo na unaambiwa ukajibu hoja kwa CAG za dhambi ambazo hazikuhusu. Faida moja ya cheo ni kuwa kuna mikopo bankers wanakupa kwa kukuamini tu, tena kwa simu tu. Siku kikiondoka, wadai wote wanaanza kuhaha kukudai kama hawakujui vile. Wakubwa wote hawapokei simu zako. Unabaki peke yako kama siyo wewe vile. Marafiki waliokuwa wanakusalimia kila kukicha hawapokei simu zako wala hawajibu meseji zako.

Ukiwa na roho ndogo utasema umerogwa ama utaugua ugonjwa wa akili. Ama hata utaona maisha hayana maana tena.

Wakati unajaribu kutoka, bei za mazao zinaporomoka! Vita ya Ukraine inaanza na COVID inapandisha bei za mbolea etc.

Mwaka huu bei za mazao nzuri, wanatokea kwelea kwelea 😀.

Ili kusimama kwenye maisha, muombe sana Mungu akupunguzie masomo magumu ya kupitia, aidha usihangaike sana kuimarisha misuli ya mwili ili ukivaa suti upendeze, imarisha misuli ya moyo, ubongo na roho(kama nayo ina muscles!😀) ili uweze kukabiliana na nyakati za maanguko. Siku zote jua tu kwamba, baada ya maanguko kadhaa, na kama utaweza kuinuka kila unapoanguka, na kustahimili maumivu ya kila anguko, mwangaza huja na Mungu humuinua mja wake! (Graduation hiyo sasa!)

Maisha ni Marathon. Kutajirika siyo rahisi. Lakini kwani nani alisema umaskini ni raha?

Iendelee ama iishie hapa?

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 3.

Ukitenda wema, tenda kwa watu wengi sana, muhimu ni kuwa usingoje shukran. Kwa hakika wema, ni akiba isiyooza.

Pamoja na uwepo wa watu wengi wa hovyo kwenye maisha yetu, watu ambao hawawezi kukufanyia jambo jema, zaidi zaidi wanajipanga kukuangusha na kukudhuru kila kukicha, tena hawana sababu yoyote ile, huwa wapo watu wachache wema, pengine uliwahi kuwatendea wema basi wanakumbuka ama ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda wema tu. Wapo!

Wabaya wengi wapo lakini wema wachache pia wapo. Jitahidi uwe miongoni mwa wema.

Kwenye maisha yako jitahidi kuwatendea watu wema, bila sababu, hujui nyuma ya tabasamu la mtu aliyekuja mbele yako kuna nini anapitia!

Kuna mtu mmoja alipataga kesi ya uhujumu uchumi, sikuwahi kuwa namjua, wala hakuwa rafiki yangu, na wala namba yake ya siku sikuwa nayo.

Nikaona mambo kwenye mitandao, nikafuatilia nikaona anaonewa tu, bila sababu. Nikaingilia kati kumtetea. Siyo kwa sababu yoyote ile, bali kwa kutamani kuona anatendewa haki.

Nilipoingia nikaambiwa ni maelekezo kutoka juu. Juu kuna Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu. Nikapiga moyo konde nikamuendea hewani bwana mkubwa; akaniuliza swali moja tu “umehongwa shilingi ngapi?” Nikamuambia Mhe. Rais, utakuwa umeshauriwa vibaya, kama unaniamini mimi mshauri wako unisikilize nikupe taarifa yangu kisha utume watu wako wafuatilie, mimi hata huyu mtu simjui na wala sijawahi kuwasiliana naye hata mara moja! Akakata simu.

Baada ya muda kidogo ukweli ulifika mezani kwa bwana mkubwa, akanipigia akasema ulisema kweli. Umenifurahisha. Yule bwana alikuja akaachiwa. Akaja akajua ushiriki wangu kwenye jambo lake. Akanishukuru sana. Akataka kunipa chochote nilikataa. Tukawa marafiki.

Siku moja baadaye kabisa, hapo nishatoka kwenye serikali, napambana na miradi yangu, hali yangu ngumu, sina kitu, naingiza kontena za kiwanda changu akajua akaniita, basi akalipia nusu ya gharama zote za kontena zangu!

Hakujua ni kiasi gani nilikuwa hoi! Usiku nilitafakari sana jambo lile hadi machozi yalinitoka. Niliswali rakaa mbili kumshukuru MUNGU…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 4.

Kila kitu kitapita. Hata uwe unapitia kipindi kigumu namna gani, jua tu kipindi hicho kitapita. Kama upo kwenye raha namna gani, jua tu zitaisha. Hakuna kinachodumu milele chini ya jua. Kila kitu kitapita. Kuna miamba, majabbar anidi, ilipita! Iko wapi leo hii?

Basi, maneno haya yatoshe kutunyenyekeza, kutushusha na kutukumbusha kuwa watu wema zaidi ya wabaya.
Mimi Nina kanuni moja kwenye maisha yangu; kama ni kuonewa, basi acha nionewe mimi, lakini siyo mimi nionee mtu mwingine. Kama ni kudhulumiwa, acha nidhulumiwe mimi lakini siyo mimi kumdhulumu mtu. Huwa naamini wema ni akiba isiyooza lakini ubaya ni deni lisilofutika! Ubaya utakurudia tu.

Watu kama mimi huchukuliwa kama watu imara na wagumu kweli kweli, na wenye mamlaka makubwa sana, kwamba tunaweza kufanya lolote na kumfanya mtu chochote, lakini amini nakuambia binafsi nimeonewa na kudhulumiwa mara nyingi na wengine kuliko unavyoweza kudhania.

Kuna kijana wangu mmoja, na wapo wengi, sema ntatolea mfano huyu mmoja, aliwahi kunipiga parefu sana. Kwa mara ya kwanza nililia machozi ya uchungu sana mbele ya wanangu. Na mbele ya mama yangu, nikiwa mtu mzima!

Tumelima, tumejaza stock kwenye magodown yetu na ya kukodi. Tumetazama soko tukajua bei zitapanda, tukanunua na mzigo mwingine kwa wakulima wengine tukatunza. Kwamba tutauza baadaye bei zikipanda. Biashara ya mazao siyo rocket science, ukiwa na mtaji tu, ukatunza stock siku bei zikipanda unauza kwa faida unatengeneza pesa nzuri.

Kumbe dogo ananiambia amepata mzigo wa kutosha, natuma hela, kumbe ananunua kidogo, anamhonga store keeper, wanaweka rekodi sawa, dogo anakula hela. Uko zako mjini, busy na majukumu ya serikali, unajenga nchi! Simu inaita tena baada ya siku tatu, unaambiwa kuna mkulima mwingine mkubwa anauza mzigo wake, unapiga kadhaa, unakopa hela unasukuma kwenye stock!

Kumbe unanunua Moet, VSOP etc. Dogo anafunga bar, anaagiza slay queens kutoka Dar, anawapa bata la hatari!

Dogo umempa gari, Nissan Patrol, matrekta, combine harvesters na mashine zote, na mamlaka ya kusimamia kampuni yako, basi anatukana na kuchimba mkwara kila mtu kwa jina lako! Inaendelea…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 5.

Anaogopwa kuliko hata unavyoogopwa wewe mwenyewe! Hakuna anayekupa taarifa na wewe uko busy na ujenzi wa Taifa!
Kumbe Taifa lako binafsi la Kigwangalla Corporation linaangamia! 😭💔

Wakati wa kulima, dogo anakupa hesabu ya kulimia ekari 400, kumbe amelima ekari 300. Ekari zako 100 amewakodishia watu wengine wanalima, halafu wewe anakuletea hesabu za mahitaji ya ekari zote 400 wakati wote - kuanzia mbegu, mashine za kulimia, kuvuruga, vibarua wa kupanda, madawa, mbolea, palizi, kuvunia, usimamizi.

Mwishoni kule anakupa hadi na idadi ya gunia alizovuna na kutunza godown. Hesabu yake na hesabu ya store keeper ziko sawa.

Bei zinaanza kupanda, wewe unachekelea unajua huu ndiyo ule mwaka wangu wa kupiga hela ndefu, ntanunua na G Wagon yangu (my dream car), ntajenga na ile lodge yangu, na zile apartments zangu! 😀. Ntalipa na madeni yangu yote ya mikopo, nitaongeza uwekezaji wangu kwenye hisa na T-bonds! Kumbe maskini unajenga zako magorofa hewani! 😭😪💔 ushapigwa!

Mtu mmoja akaniambia amekutana na ‘mdogo wangu’, yule anaitwa Kigwangalla, anayesimamia miradi yangu ya mashamba alikuwa club na warembo (ni maarufu sitowataja majina!) akampa offer! Nikashtuka.

Nikamcheki dogo, nikamuambia nimepata salamu zake. Nikaona nimtume kijana mmoja wa ofisini kwangu Dar, na mke wangu, wakakague stock. Akasikia kuwa wanakuja. Akaanza mbinu na wenzake, eti wachome godown ili kupoteza ushahidi! 💔😭😩

Anayetoa hizo taarifa ni mdada mmoja ambaye alikuwa rafiki wa mwamba, kumbe alimsikia akiongea kuhusu madumu ya petrol kumwagwa usiku kwa akili sana ili kupoteza ushahidi. Kwamba, kwanza wangetoa mpunga zaidi kutoka godown, wabakishe kidogo, halafu kwa kuwa huwa tunamwaga pumba za mpunga kwenye sakafu, wakinyunyiza petrol kidogo tu moto utakuwa mkali sana kiasi kwamba hautoweza kuzimika, kila kitu kitateketea!

Huyo dada akasikia huruma sababu alijua wizi waliokwisha kunifanyia halafu wakichoma tena hicho kidogo, wachome na godown langu, na ndani humo Kuna mashine zangu zote - trekta kubwa3, stock ya mbolea, madawa… #HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 6.

…madawa ya mimea na combine harvester, itakuwa mbaya sana! Akamuambia ndugu yangu mmoja.

Ndugu akanitafuta toka asubuhi, wapi! Siku hiyo nilikuwa Ikulu kwenye cabinet, mule hamuingii na simu. Tumetoka, naingia kwenye gari, la kwanza kuwasha simu, nakutana na meseji Lukuki! Baada ya mimi kukosekana jamaa zangu waliamua kuripoti polisi, ulinzi ukawekwa!

Nilisikia kama nimechomwa kitu moyoni. Machozi yalinitoka bila kupigwa! Bila kutoa sauti. Sitokuja kusahau.

Nilifika nyumbani nikamkuta mama yangu sebuleni, niliangua kilio kama niliyefiwa na mtoto ama mzazi. Katika ukubwa wangu, nimewahi kufikwa na mambo mengi, lakini sijawahi kulia hata siku moja. Siku hii nililia bila kujali wanangu wanatazama wala nini. Mama yangu alinikumbatia kwa nguvu na kunituliza.

Nilijiuliza sana nimemkosea nini huyu dogo? Na wenzake? Mpaka leo sijawahi kupata majibu ya maswali yangu. Vijana wa kitanzania mna la kujifunza hapa. Huyu dogo na wenzake niliwapa gari ya kutembelea, mapikipiki, mashine ambazo wakimaliza kufanya kazi kwangu wanakodisha kwa wengine wanapata hela ya kula na matanuzi (ambayo mimi siichukui), kila kijana mmoja nalipia gharama ya kuanzia kumlimia na kumtunzia shamba lake; ekari 30 (huyo mkubwa wao), ekari 15 wale wasaidizi wake wawili. Kwenye ekari 15 unapata kati ya 30 - 40m kwa mwaka. Matukio ya hivi ni mengi kwenye story za wajasiriamali wengi hapa nchini.

Vijana wanadanganyika sana na maisha ya superstars, wanataka wayaishi bila jasho. Wengine wameishia kujidhalilisha na wengine wamefikia hata kushikishwa ukuta! Kama huna kipaji mdogo wangu, usitamani maisha ya wenye navyo. Fanya kazi kwa bidii, jipe muda wa kujitafuta, na wa kutafuta nafasi yako maishani. Ukifika utakula maisha yako ya halali kabisa.

Usikubali kuingia kwenye kundi la vijana wanaotafuta ajira lakini hawataki kufanya kazi. Wala usilikurubie kundi la vijana wanaotafuta ajira ili wakapige deal! Kila kijana anataka awekwe kitengo chenye ‘michongo’! Jamani nchi haijengwi namna hiyo. Hela haitafutwi namna hiyo. Nakuhakikishia, hela ya hivyo ukiipata haitokaa. Itakimbia tu.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIBA UBORA WAKE! Part 7.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani kuwa kama mimi, basi nikuambie ukweli kuwa mimi najiona ‘Muomba Allah’ tu, sijafika popote na kiukweli hata hapa padogo nilipofikia, siyo kwa madili, dhulma, ubadhirifu na wala siyo kazi rahisi. Uwe tayari kutokwa machozi, jasho na damu!

Halafu; kwenye maisha yetu pesa, vitu, vyeo havileti furaha ya kweli, na wala havina thamani ya kweli. Vitu vyote vyenye thamani ya kweli kwenye maisha huwa havishikiki na havinunuliki. Usipoteze utu na imani yako kutafuta vitu vinavyoshikika.

Swali la ‘what did I do to deserve that?’ Halijawahi kunitoka. Usiulize huyu dogo mengine ya kijamii niliyowahi kumfanyia ni mangapi? Sema sipendagi kusema wema niliofanyia watu, Ila jua tu nilim-treat kwa heshima kupindukia, harusi yake niliwekeza na kuisimamia zaidi ya nilivyofanya kwa mdogo wangu niliyemuachia ziwa la mama!

Imagine rafiki zangu walivyojitoa, hata sijawahi kuwaambia dogo alivyoninyoosha! Dan La Kairo alitoa Range Rover yake mpya Autobiography kumpa dogo akajiendesha na mkewe! Miaka mitatu tu baadaye anataka kuchoma mali yangu! Dah! #HK #Fighter #NjeYaBox Iendelee ama tuishie hapa kwa sasa?
alalamike afanye atavyofanya ila aina ya maisha tunayoishi watanzania ni mfumo ulioletwa na watawala hakuna kitu kinaibuka tu from no were ila wakitaka kutulaumu vijana kwanza tuwaulize wao mali wanazomiliki zote ni za halali viongozi wetu na watendaji wetu ambao wengi ni wazazi wetu je mali zao ni za halali.??

watoto siku zote tabia wanaadopt kutoka kwa wazazi wajitazame wao na wajisahihishe then warudi kwetu watusahihishe..
tofauti na hapo ni kupigia mbuzi gitaa tu.
 
Nilikuwa nawaza kuandika uzi wa namna hii kutokana na changamoto na uzoefu niliokutana nao katika harakati za kutaka kutengeneza maisha bora KWa familia yangu na jamii KWa ujumla. Lakini kwakuwa bwana kigwa kaandika ujumbe umewapata wahusika...

Nakumbuka katika harakati za maisha kuna biashara nilianzishisha,, nikamuweka mdogo wangu.. aiseh SAsa sijui alichoka au hakuitaka... Aliharibu sana aiseh...! Kwakuwa ni ndugu nikaona nipotezee tu nimepata elimu fulani katika hilo... Haya kuna ndugu wa pembeni alikuja kunitembelea akaniambia e bana nitakaa wiki 2 tu! Nikasema haina shida njoo... Alivyo kuja siku hiyo nilikuwa nasimamia biashara yangu mwenyewe.. alivyo fika akaona hakuamini maana alikuwaga na dharau sana... SAsa sijui iliwasa tu moyoni kuwa ana hakikisha ananifilisi... E bwana eeh! Ile mdogo wangu alivyo maliza dharula yake nami nikawa naendelea na mengine jamaa KILA day anakwenda pale ofisini atashinda asubuhi hadi jioni na atafosi atumie bajeti ya ofisi... Nilikuwa sijui kuja kugundua ni siku napitia hesabu nikajua nikashangaa wewe inakuaje unatumia chakula gharama hii namuuliza SAsa yule mdogo wangu nilie mwachia... Tumboni una mapipa ya lita 200? Kanyamaza tu SAsa hadi vicha unaweka KWa kutumia pesa ya ofisi kwani sikupagi pesa? Kanyamaza tu.... Nilimindi sana nikaona nikwambia ukweli hunikomoi tu mimi hadi wewe unajikomoa bila kujua mambo maana hayatoniharibikia tu mimi... BAdo wewe na wadogo zako na wazazi wetu maana kidogo mimi nina kahaueni badala muwe na bidii na uaminifu mnasikiliza ndugu wengine we haya... Kwakuwa baada ya kupiga hesabu nikaona hapa hadi nifanye haki itakuwa tete tu labda nikope... Nikaona niipotezee tu ijifie taratibu... Nilivyo ipotezea yule jamaa nae akawa ana kazana kwenda halafu ikifika jioni anasikia naongea na simu kama nimepagawa nakaripia watu hovyo KWa sababu ya mishe nilizo wapa nikawaamini na zikafeli yeye kumbe akisikia vile ana furahi.. na KWa upande wa pili wa mdogo wangu alivyo ona nimeicha biashara ijifie nae baadhi ya mambo yakawa magumu akaona amwambie mama kuwa yule ndugu ndo kasabisha yeye tokea aje kutwa hapa anafosi matumizi yake yaingizwe kwenye bajeti ya ofisi... Mama akamjibu kwanini ulinyamaza hana majibu... Mama kanitonya... Ikabidi nimchane tu jamaa kuwa aondoke kwangu maana SAsa ni miezi 3 na ulisema wiki 2.... Daahh! Nilisikitika sana..

Kuna mwengine nae kaomba chombo ya moto KWa ajili ya biashara akasema mimi nitakupa faida.. fulani yule hawezi sijui anakusumbua... Haya Sawa chukua chombo hii... Mwezi umepita mtu kimya unamuuliza vipi chombo mbovu hii namuuliza KWa nini usiniambie? Hana majibu yanayo elewaka( Hapo kuna mtu ananiambia chombo inapiga Kazi vibaya mno) nikamwambia leo jioni ilete(huwa ananielewa nikongeaga kitu huwana nahakikisha nakitekeleza au kinatekelezwa)... Imefika jioni naona muamala... Nikampigia hii ndo jioni ilete chombo majibu yake SAsa! Oohhh! Najua kwako hii biashara kwahiyo mambo yasiwe magumu nimeazima nikutumie... Nikamwambia hiyo si mbovu SAsa unakaa nayo ya nini? Ilete nikipata pesa nitairekebisha, jibu lake ooh! Nitairekebisha.... Nikaona isiwe tabu kesho irekebishe... SAsa sijui ndo alienda kuharibu? Ila hesabu anatuma lakini kumbe sijui anamipango yake... Imefika wakiti ananipa taarifa chombo ipo KWa Fundi naenda KWa Fundi chombo haitamaniki... Na sijui walipanga na Fundi? Nikapiga hesabu ya vifaa original pesa niliyo toa na ni zaidi hata ya hesabu aliyonipa KWa siku zote... Naye Fundi kama ilivyo destri ya Vijana wengi wa kitanzania pia kafanya udhulmati wake (aliyo yafanya itoshe tu kusema sio Fundi mtengenezaji ni Fundi muharibifu). Nikaona ataniumiza kichwa pamoja na kuingia hasara nikaona nichukue siklepa langu maana lishakuwa siklepa kwanguvu nikaondoka nalo likae tu home maana linafanya Kazi badala linipe faida linanitia hasara tu...

Nakubaliana na baadhi ya wanajamvi humu somo la maadili muhimu... Kokote kwenye mikusanyiko lisemwe, na Katika familia lisemwe na kutendwa na pia liwekwe mashuleni kuanzia chekechea hadi university.......

Japan wamefanikiwa sana katika hilo.. somo la maadili lipo mashuleni... Kuna jamaa mmoja mbongo alikuwa anafundisha shule ya Kati huko nchini japani unaweza sema KWa bongo huku ni kama sekondari... Siku kuna Mwanafunzi alisahau kamera darasani ile kamera ilikaa wiki nzima pale pale hadi yule Mwanafunzi anafika darasa lile anaikuta vile vile..... Bongo SAsa hata uangushe bahasha iliyo tuna watu hata hawajui kuna nini watatembea nayo... Watafungulia hukohuko... Kama wakikuta makaratasi ambayo hayana faida kwao watayatupa bila kujali wewe uliye yaangusha unafaida nayo hata kama wanakujua...
Pole mkuu ila apo kwenye MAADILI kwa nchi hii Kila sehemu tatizo labda tufe wote wazaliwe wapya tuanze 1
 
Leo asb Hamisi Kigwangalla ameliamsha tena huko Instagram suala la uaminifu wa watanzania. Amehadithia alichofanyiwa na kijana aliyemuamini. Huko nyuma amewahi kuuliza WHAT IS TANZANIA'S COMPETITIVE ADVANTAGE -Akimaanisha nini ambacho tunaweza kusema hichi kinatutambulisha kitaifa.

Juzi kati I-SOKO mfumo wa kuwezesha wanawake kufanya biashara afrika mashariki imeanzishwa. Kilichojiri malalamishi kwamba watanzania hatuaminiki.

Kihehe tunasema sema we have a people problem. Tatizo ni kubwa lakini tunaogopa kulijadili kwakuwa ni kaa la moto. Au halipo

SOMA KISA HIKI KUTOKA KWA hamis Kigwangalla

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 1:

Kama ukiona elimu ni gharama, ujue haujajaribu ujinga. Vile vile, kama ukiona kutafuta utajiri ni kazi, hebu jaribu umaskini uone.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama umaskini. Tuliouishi umaskini tunaujua. Tukipambana nao kwa kila hali msitushangae. Mara kadhaa tushawahi kurudi nyumbani for lunch na kukuta hakuna kilichopikwa tukaishia kunywa maji na kugeuza shule, maana hata wa kumuuliza chakula kiko wapi hayupo home.

Kutajirika ni katika vitu vigumu kabisa kufanya hapa duniani. Niliwahi kujaribu kutafuta utajiri sikuufikia, nikaishia hapa nilipo! Lakini bado napambana. Si haba, WALLAH sina malalamiko yoyote yale kwa Allah, zaidi zaidi narejesha shukrani tele. Nilipotoka napajua mwenyewe.

Kwenye safari ya kutafuta maisha, kwa kuwa nilikuwa na mbio ndefu na za spidi sana, nimejifunza mengi sana. Huwa najaribu kuandika andika hapa, wenye muda husoma na pengine hujifunza.

Niliwahi kuwa nalima ekari 500 - 600 kwa msimu, nikamuamini kijana wangu mmoja mahiri, mchapakazi, mwenye dini kweli kweli, mwenye elimu na passion ya farming; pamoja na kunifaidisha na kunipa tamaa ya kuwekeza zaidi, alinipiga kweli kweli!

Nikaamini wadogo zangu damu kabisa, wakanipiga. Nikazama. [emoji30]!

Mtaji wa zaidi ya ekari 700 ukaporomoka mpaka ekari 100/200. Wakati unaporomoka, unadaiwa na benki ulipe mkopo wa mtaji uliochukua, unadaiwa na kampuni waliokukopesha matrekta, combine harvesters, planters, unadaiwa na suppliers wa pembejeo etc. Inaendelea…

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE. Part 2!

Wakati huo huo umeshushwa cheo na unaambiwa ukajibu hoja kwa CAG za dhambi ambazo hazikuhusu. Faida moja ya cheo ni kuwa kuna mikopo bankers wanakupa kwa kukuamini tu, tena kwa simu tu. Siku kikiondoka, wadai wote wanaanza kuhaha kukudai kama hawakujui vile. Wakubwa wote hawapokei simu zako. Unabaki peke yako kama siyo wewe vile. Marafiki waliokuwa wanakusalimia kila kukicha hawapokei simu zako wala hawajibu meseji zako.

Ukiwa na roho ndogo utasema umerogwa ama utaugua ugonjwa wa akili. Ama hata utaona maisha hayana maana tena.

Wakati unajaribu kutoka, bei za mazao zinaporomoka! Vita ya Ukraine inaanza na COVID inapandisha bei za mbolea etc.

Mwaka huu bei za mazao nzuri, wanatokea kwelea kwelea [emoji3].

Ili kusimama kwenye maisha, muombe sana Mungu akupunguzie masomo magumu ya kupitia, aidha usihangaike sana kuimarisha misuli ya mwili ili ukivaa suti upendeze, imarisha misuli ya moyo, ubongo na roho(kama nayo ina muscles![emoji3]) ili uweze kukabiliana na nyakati za maanguko. Siku zote jua tu kwamba, baada ya maanguko kadhaa, na kama utaweza kuinuka kila unapoanguka, na kustahimili maumivu ya kila anguko, mwangaza huja na Mungu humuinua mja wake! (Graduation hiyo sasa!)

Maisha ni Marathon. Kutajirika siyo rahisi. Lakini kwani nani alisema umaskini ni raha?

Iendelee ama iishie hapa?

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 3.

Ukitenda wema, tenda kwa watu wengi sana, muhimu ni kuwa usingoje shukran. Kwa hakika wema, ni akiba isiyooza.

Pamoja na uwepo wa watu wengi wa hovyo kwenye maisha yetu, watu ambao hawawezi kukufanyia jambo jema, zaidi zaidi wanajipanga kukuangusha na kukudhuru kila kukicha, tena hawana sababu yoyote ile, huwa wapo watu wachache wema, pengine uliwahi kuwatendea wema basi wanakumbuka ama ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda wema tu. Wapo!

Wabaya wengi wapo lakini wema wachache pia wapo. Jitahidi uwe miongoni mwa wema.

Kwenye maisha yako jitahidi kuwatendea watu wema, bila sababu, hujui nyuma ya tabasamu la mtu aliyekuja mbele yako kuna nini anapitia!

Kuna mtu mmoja alipataga kesi ya uhujumu uchumi, sikuwahi kuwa namjua, wala hakuwa rafiki yangu, na wala namba yake ya siku sikuwa nayo.

Nikaona mambo kwenye mitandao, nikafuatilia nikaona anaonewa tu, bila sababu. Nikaingilia kati kumtetea. Siyo kwa sababu yoyote ile, bali kwa kutamani kuona anatendewa haki.

Nilipoingia nikaambiwa ni maelekezo kutoka juu. Juu kuna Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu. Nikapiga moyo konde nikamuendea hewani bwana mkubwa; akaniuliza swali moja tu “umehongwa shilingi ngapi?” Nikamuambia Mhe. Rais, utakuwa umeshauriwa vibaya, kama unaniamini mimi mshauri wako unisikilize nikupe taarifa yangu kisha utume watu wako wafuatilie, mimi hata huyu mtu simjui na wala sijawahi kuwasiliana naye hata mara moja! Akakata simu.

Baada ya muda kidogo ukweli ulifika mezani kwa bwana mkubwa, akanipigia akasema ulisema kweli. Umenifurahisha. Yule bwana alikuja akaachiwa. Akaja akajua ushiriki wangu kwenye jambo lake. Akanishukuru sana. Akataka kunipa chochote nilikataa. Tukawa marafiki.

Siku moja baadaye kabisa, hapo nishatoka kwenye serikali, napambana na miradi yangu, hali yangu ngumu, sina kitu, naingiza kontena za kiwanda changu akajua akaniita, basi akalipia nusu ya gharama zote za kontena zangu!

Hakujua ni kiasi gani nilikuwa hoi! Usiku nilitafakari sana jambo lile hadi machozi yalinitoka. Niliswali rakaa mbili kumshukuru MUNGU…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 4.

Kila kitu kitapita. Hata uwe unapitia kipindi kigumu namna gani, jua tu kipindi hicho kitapita. Kama upo kwenye raha namna gani, jua tu zitaisha. Hakuna kinachodumu milele chini ya jua. Kila kitu kitapita. Kuna miamba, majabbar anidi, ilipita! Iko wapi leo hii?

Basi, maneno haya yatoshe kutunyenyekeza, kutushusha na kutukumbusha kuwa watu wema zaidi ya wabaya.
Mimi Nina kanuni moja kwenye maisha yangu; kama ni kuonewa, basi acha nionewe mimi, lakini siyo mimi nionee mtu mwingine. Kama ni kudhulumiwa, acha nidhulumiwe mimi lakini siyo mimi kumdhulumu mtu. Huwa naamini wema ni akiba isiyooza lakini ubaya ni deni lisilofutika! Ubaya utakurudia tu.

Watu kama mimi huchukuliwa kama watu imara na wagumu kweli kweli, na wenye mamlaka makubwa sana, kwamba tunaweza kufanya lolote na kumfanya mtu chochote, lakini amini nakuambia binafsi nimeonewa na kudhulumiwa mara nyingi na wengine kuliko unavyoweza kudhania.

Kuna kijana wangu mmoja, na wapo wengi, sema ntatolea mfano huyu mmoja, aliwahi kunipiga parefu sana. Kwa mara ya kwanza nililia machozi ya uchungu sana mbele ya wanangu. Na mbele ya mama yangu, nikiwa mtu mzima!

Tumelima, tumejaza stock kwenye magodown yetu na ya kukodi. Tumetazama soko tukajua bei zitapanda, tukanunua na mzigo mwingine kwa wakulima wengine tukatunza. Kwamba tutauza baadaye bei zikipanda. Biashara ya mazao siyo rocket science, ukiwa na mtaji tu, ukatunza stock siku bei zikipanda unauza kwa faida unatengeneza pesa nzuri.

Kumbe dogo ananiambia amepata mzigo wa kutosha, natuma hela, kumbe ananunua kidogo, anamhonga store keeper, wanaweka rekodi sawa, dogo anakula hela. Uko zako mjini, busy na majukumu ya serikali, unajenga nchi! Simu inaita tena baada ya siku tatu, unaambiwa kuna mkulima mwingine mkubwa anauza mzigo wake, unapiga kadhaa, unakopa hela unasukuma kwenye stock!

Kumbe unanunua Moet, VSOP etc. Dogo anafunga bar, anaagiza slay queens kutoka Dar, anawapa bata la hatari!

Dogo umempa gari, Nissan Patrol, matrekta, combine harvesters na mashine zote, na mamlaka ya kusimamia kampuni yako, basi anatukana na kuchimba mkwara kila mtu kwa jina lako! Inaendelea…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 5.

Anaogopwa kuliko hata unavyoogopwa wewe mwenyewe! Hakuna anayekupa taarifa na wewe uko busy na ujenzi wa Taifa!
Kumbe Taifa lako binafsi la Kigwangalla Corporation linaangamia! [emoji24][emoji174]

Wakati wa kulima, dogo anakupa hesabu ya kulimia ekari 400, kumbe amelima ekari 300. Ekari zako 100 amewakodishia watu wengine wanalima, halafu wewe anakuletea hesabu za mahitaji ya ekari zote 400 wakati wote - kuanzia mbegu, mashine za kulimia, kuvuruga, vibarua wa kupanda, madawa, mbolea, palizi, kuvunia, usimamizi.

Mwishoni kule anakupa hadi na idadi ya gunia alizovuna na kutunza godown. Hesabu yake na hesabu ya store keeper ziko sawa.

Bei zinaanza kupanda, wewe unachekelea unajua huu ndiyo ule mwaka wangu wa kupiga hela ndefu, ntanunua na G Wagon yangu (my dream car), ntajenga na ile lodge yangu, na zile apartments zangu! [emoji3]. Ntalipa na madeni yangu yote ya mikopo, nitaongeza uwekezaji wangu kwenye hisa na T-bonds! Kumbe maskini unajenga zako magorofa hewani! [emoji24][emoji25][emoji174] ushapigwa!

Mtu mmoja akaniambia amekutana na ‘mdogo wangu’, yule anaitwa Kigwangalla, anayesimamia miradi yangu ya mashamba alikuwa club na warembo (ni maarufu sitowataja majina!) akampa offer! Nikashtuka.

Nikamcheki dogo, nikamuambia nimepata salamu zake. Nikaona nimtume kijana mmoja wa ofisini kwangu Dar, na mke wangu, wakakague stock. Akasikia kuwa wanakuja. Akaanza mbinu na wenzake, eti wachome godown ili kupoteza ushahidi! [emoji174][emoji24][emoji30]

Anayetoa hizo taarifa ni mdada mmoja ambaye alikuwa rafiki wa mwamba, kumbe alimsikia akiongea kuhusu madumu ya petrol kumwagwa usiku kwa akili sana ili kupoteza ushahidi. Kwamba, kwanza wangetoa mpunga zaidi kutoka godown, wabakishe kidogo, halafu kwa kuwa huwa tunamwaga pumba za mpunga kwenye sakafu, wakinyunyiza petrol kidogo tu moto utakuwa mkali sana kiasi kwamba hautoweza kuzimika, kila kitu kitateketea!

Huyo dada akasikia huruma sababu alijua wizi waliokwisha kunifanyia halafu wakichoma tena hicho kidogo, wachome na godown langu, na ndani humo Kuna mashine zangu zote - trekta kubwa3, stock ya mbolea, madawa… #HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIKA UBORA WAKE! Part 6.

…madawa ya mimea na combine harvester, itakuwa mbaya sana! Akamuambia ndugu yangu mmoja.

Ndugu akanitafuta toka asubuhi, wapi! Siku hiyo nilikuwa Ikulu kwenye cabinet, mule hamuingii na simu. Tumetoka, naingia kwenye gari, la kwanza kuwasha simu, nakutana na meseji Lukuki! Baada ya mimi kukosekana jamaa zangu waliamua kuripoti polisi, ulinzi ukawekwa!

Nilisikia kama nimechomwa kitu moyoni. Machozi yalinitoka bila kupigwa! Bila kutoa sauti. Sitokuja kusahau.

Nilifika nyumbani nikamkuta mama yangu sebuleni, niliangua kilio kama niliyefiwa na mtoto ama mzazi. Katika ukubwa wangu, nimewahi kufikwa na mambo mengi, lakini sijawahi kulia hata siku moja. Siku hii nililia bila kujali wanangu wanatazama wala nini. Mama yangu alinikumbatia kwa nguvu na kunituliza.

Nilijiuliza sana nimemkosea nini huyu dogo? Na wenzake? Mpaka leo sijawahi kupata majibu ya maswali yangu. Vijana wa kitanzania mna la kujifunza hapa. Huyu dogo na wenzake niliwapa gari ya kutembelea, mapikipiki, mashine ambazo wakimaliza kufanya kazi kwangu wanakodisha kwa wengine wanapata hela ya kula na matanuzi (ambayo mimi siichukui), kila kijana mmoja nalipia gharama ya kuanzia kumlimia na kumtunzia shamba lake; ekari 30 (huyo mkubwa wao), ekari 15 wale wasaidizi wake wawili. Kwenye ekari 15 unapata kati ya 30 - 40m kwa mwaka. Matukio ya hivi ni mengi kwenye story za wajasiriamali wengi hapa nchini.

Vijana wanadanganyika sana na maisha ya superstars, wanataka wayaishi bila jasho. Wengine wameishia kujidhalilisha na wengine wamefikia hata kushikishwa ukuta! Kama huna kipaji mdogo wangu, usitamani maisha ya wenye navyo. Fanya kazi kwa bidii, jipe muda wa kujitafuta, na wa kutafuta nafasi yako maishani. Ukifika utakula maisha yako ya halali kabisa.

Usikubali kuingia kwenye kundi la vijana wanaotafuta ajira lakini hawataki kufanya kazi. Wala usilikurubie kundi la vijana wanaotafuta ajira ili wakapige deal! Kila kijana anataka awekwe kitengo chenye ‘michongo’! Jamani nchi haijengwi namna hiyo. Hela haitafutwi namna hiyo. Nakuhakikishia, hela ya hivyo ukiipata haitokaa. Itakimbia tu.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani…#HK #Fighter #NjeYaBox

NJE YA BOX: MAISHA KATIBA UBORA WAKE! Part 7.

Kama unahisi ‘nimefika mbali’ na unatamani kuwa kama mimi, basi nikuambie ukweli kuwa mimi najiona ‘Muomba Allah’ tu, sijafika popote na kiukweli hata hapa padogo nilipofikia, siyo kwa madili, dhulma, ubadhirifu na wala siyo kazi rahisi. Uwe tayari kutokwa machozi, jasho na damu!

Halafu; kwenye maisha yetu pesa, vitu, vyeo havileti furaha ya kweli, na wala havina thamani ya kweli. Vitu vyote vyenye thamani ya kweli kwenye maisha huwa havishikiki na havinunuliki. Usipoteze utu na imani yako kutafuta vitu vinavyoshikika.

Swali la ‘what did I do to deserve that?’ Halijawahi kunitoka. Usiulize huyu dogo mengine ya kijamii niliyowahi kumfanyia ni mangapi? Sema sipendagi kusema wema niliofanyia watu, Ila jua tu nilim-treat kwa heshima kupindukia, harusi yake niliwekeza na kuisimamia zaidi ya nilivyofanya kwa mdogo wangu niliyemuachia ziwa la mama!

Imagine rafiki zangu walivyojitoa, hata sijawahi kuwaambia dogo alivyoninyoosha! Dan La Kairo alitoa Range Rover yake mpya Autobiography kumpa dogo akajiendesha na mkewe! Miaka mitatu tu baadaye anataka kuchoma mali yangu! Dah! #HK #Fighter #NjeYaBox Iendelee ama tuishie hapa kwa sasa?
Doh! Watu wamepitia mengi
 
Ukitafsiri hadith ya HK kwa lugha yeyote ile halafu ukatafuta gugu au search engine yeyote ile kwa kutumia part(sehemu yeyote ile) katika hiyo hadithi;utakutana na stori kama hiyo Duniani kote! Yaani utaweza kudhani ame kwapua na kubandika(copy and paste) vile kwa kufanana fanana na stori zingine.

Hakika yamemkuta, na ninawajua wengi kama HK. Mhindi, Mzungu, Mkenya wote have something in common, nayo ni lack of trust..hawana wakuwaamini kwa 100% kwa lugha nyingine nyepesi tu ni Uaminifu(trustworthiness) ni hulka ya binadamu. Watu wote bila kujali dini rangi nchi au jinsia yake...Hivyo basi kuwapachika Watanzania kwa ujumla kuwa hawaaminiki ni kosa kubwa sana. Tupnuguze kujishusha chini kiasi hicho na kuwaacha hawa wapotoshaji kama huyu ninayemnukuu ambaye anadai ni sababu za "Ujamaa"

....ipo siku weye huo uwakili wako utakapo kurudia... karma will devour you, hiyo tabia unayotaka kutumia kuwatukana Watanzania kila kukicha itakumaliza vilivyo. Ulaaniwe kwa jina la Mungu. Ulegee na ushindwe.
Ujamaa huzalisha wezi na wabinafsi. Hilo halina ubishi.
 
Kwa capital yake alitakiwa aajili external auditors, ina maana yeye mahesabu alikuwa hapeleki tra? Auditor wake hakuwa akimshauri? Risiti alikuwa anapewa kila akituma pesa?

Ndio maana nanukuu kariakoo kuna mfanyabiashara alisema ,ukimtoa mtu wa tra umpe duka na mtaji atachemka.
Alikuwa analima kwa Mpesa tu.
 
Japokuwa suala la uaminifu limekuwa ttz kubwa kwa watu wengi nchi hii lakini hili janga muheshiwa ni kama alilitengeneza mwenyewe
Haiwezekani mradi mkubwa kama huo ww uwe unatuma tu pesa kwa mtu
 
Wakati huo huo umeshushwa cheo na unaambiwa ukajibu hoja kwa CAG za dhambi ambazo hazikuhusu. Faida moja ya cheo ni kuwa kuna mikopo bankers wanakupa kwa kukuamini tu, tena kwa simu tu. Siku kikiondoka, wadai wote wanaanza kuhaha kukudai kama hawakujui vile. Wakubwa wote hawapokei simu zako. Unabaki peke yako kama siyo wewe vile. Marafiki waliokuwa wanakusalimia kila kukicha hawapokei simu zako wala hawajibu meseji zako.

Ukiwa na roho ndogo utasema umerogwa ama utaugua ugonjwa wa akili. Ama hata utaona maisha hayana maana tena.
Majuto ni mjukuu ndugu mheshimiwa.

Na hapo unalia kia hujalala selo Miezi sita unaliwa na kunguni kwa Kesi ya kubambikiwa.
imagine
 
Kwa maana hiyo tunakubaliana na Kigwangwala kwamba tatizo lipo. Niliwahi kuenda na Aikaeli katika hooteli yake saa 2 usiku jumamosi miaka hiyo. Wataliii 130 wameingi.Tanesco imekata wanatumia mishumaa vyumba vyote ebu fikiria hartari yake amna mafuta ya jenerator. Kwa nini? Mkuu wa stores hayupo. Jikoni mishumaa kuwalisha watalii 130 wanaolipa dola mia kabla ya kukwea kilimanjaro. Mkuu mapokezi hayupo. GM hakuwepo. Yaani mamemneja wa5 wote ambao ukiacha mshahara, posho , simu , makazi na magari wote waliondoka Arusha kutanua. Wakamuacha binti pekee mapokezi.Ilibidi Aikaeli awe chef mie nikawa mapokezi mpaka saa 7 usiku huku dereva akifuata mafuta jenereta ikawashwa. Aikaeli akawa anawaza afanyeje sheria inanitaka niajiri watanzania lakini nikiwapa fursa ndio kama hivi. Sasa nini kifanyike BLACK MOVEMENT
Aikael Mbowe?
 
Very motivating story,
Ila kichwa cha habari,kinataka kuonyesha kwamba vijana wa TZ,wote sio waaminifu,"a people problem"sio kweli,
Hata yeye kingwangala aliwahi kuwa kijana,mbona ni muaminifu?
Aliyopitia kwenye safari yake ya Maisha,siyo ya pekee yanaweza kutokea Duniani kote,
Kuhusu vijana kupenda kutafuta ajira,lakini hawataki kazi,lipo sana,ni matokeo ya uozo wa elimu yetu na malezi,
Sasa kijana anaona vijana wenzake,waliobahatika kupata ajira,tpa,nssf,bot,ndani ya muda mfupi,wana ukwasi wa kutisha,bila jasho,na yeye atatamani tu,
 
Ukisoma vitu anavyoandika sijui dhuruma sijui na moyo wa upendo anandika akiamini wapiga kura wake asilimia 90 wapo maporini na hawapo katika hizi social media

Yani ni hivi hakuna mtu kauzu na mdhurumati na mwenye roho mbaya ya umimi kama kigwangala anajisifu sijui nasaidia watu acheni awapige maneno mtandaoni hakuna mtu mbinafsi kama kigwangala muulizeni chuo chake cha uguzi kwanini hakina wakufunzi jamaa alipi mishahara yeye kisa waziri mbunge basi fundisha tu analipa anavyotaka ukidai sana unasikia nenda mahakamani, vistory vyake nje ya box nje ya box yeye ashukuru JK kumshika mkono akapata ubunge akapata mianya ya kupiga pesa ndio hivyo hana uhustler wowote aache wahadaa vijana kwa story za kutunga tunga tu maana anavyoandika asilimia 80 ni fiction

Alishapewa msaada wa computer na tasisi moja hivi akiwa kama mbunge aziwasilishe katika shule za jimbo lake, mwamba zile computer zote akapeleka katika chuo chake binafsi cha afya walimu wanambiwa na mfadhili waende chukua computer kapewa mbunge wao, walimu wanaenda kumuuliza anaanza watisha ooh tafunga mtu vitisho kibao, yani uyo kigwangala ni msanii kama wasanii wengine tu
 
Kwa maana hiyo tunakubaliana na Kigwangwala kwamba tatizo lipo. Niliwahi kuenda na Aikaeli katika hooteli yake saa 2 usiku jumamosi miaka hiyo. Wataliii 130 wameingi.Tanesco imekata wanatumia mishumaa vyumba vyote ebu fikiria hartari yake amna mafuta ya jenerator. Kwa nini? Mkuu wa stores hayupo. Jikoni mishumaa kuwalisha watalii 130 wanaolipa dola mia kabla ya kukwea kilimanjaro. Mkuu mapokezi hayupo. GM hakuwepo. Yaani mamemneja wa5 wote ambao ukiacha mshahara, posho , simu , makazi na magari wote waliondoka Arusha kutanua. Wakamuacha binti pekee mapokezi.Ilibidi Aikaeli awe chef mie nikawa mapokezi mpaka saa 7 usiku huku dereva akifuata mafuta jenereta ikawashwa. Aikaeli akawa anawaza afanyeje sheria inanitaka niajiri watanzania lakini nikiwapa fursa ndio kama hivi. Sasa nini kifanyike BLACK MOVEMENT
Poa kigwa
 
Back
Top Bottom