Imani za dini zinatupumbaza mno watanzania. Mno. Wewe mtu anakutendea uovu huo, unamwacha. Ni dhambi kwa sababu unapomwacha hujamsaidia. Mhalifu ni mhalifu tuu, peleka kwenye vyombo vya sheria aadhibiwe, akirudi mpokee. Atakuwa GM mzuri kabisa maana amefundishwa huko maana ya kufanyakazi na uadilifu. Watanzania wengi wanadhani kumfunga mtu jela ni dhambi. Hamna. Gereza ni vyombo vya Mungu pia kuifanya dunia mahala pa amani. Ona sasa, mtu anafikia hatua ya kutaka kuteketeza mali za mamia ya mamilioni! Kweli? Huyo anakuua pia, tena mchana kweupee!
Nina mtoto alijifanya ameshindikana; Peleka shule, tena hizi za gharama, wapi! Geuza na kugeuza, wapi! Wananchi wakanishauri kuwa nisimlazimishe hataki shule, kwani wote lazima wasomee? Nikawaelewa. Nikampeleka kusomea udereva, nikampatia motokaa, akashirikiana na mafundi anaiba vipuri, gari mwisho wa siku likakaa juu ya mawe. Navumilia ila moyo unaniuma kwelikweli. Akakwiba kwa mtu akafungwa, Nikamtoa. Si unajua Bongo ukiwa na "kitu kidogo" hakuna jambo gumu. Nikamweka dukani, akapora. Aah, akili zikanirudi. Utu wangu ukanirudia. Utu wa ndani kabisa. Nikahisi kuwa na hatia kwa kuendelea kumdekeza wakati Serikali imeajiri vyombo vyenye vijana wasomi waliosomeshwa hadi shahada juu ya kurekebisha tabia za watu. Nikampeleka gerezani. Mapolisi, mahakimu, maafisa magereza walinipongeza sana, walisema, Bongo tungekuwa na wazazi kama wewe tungetengeneza kizazi cha vijana kilicho bora bora kabisa. Kijana alifundishwa adabu kule. Watu wamesomea mambo haya bwana. Tena alikaa miezi mitatu tu. Aliporudi sikuamini. Jambo la kwanza alitubu kwa machozi mengi Nimsamehe. Nilimsamehe. Ni mtoto, kama mzazi sikuwa namwadhibu ili ateseke bali a-reform. Baada ya hapo Akaokoka. Aliomba shamba, nikampatia na vitendeakazi vyote. To cut story short, sasa hivi ni kijana mzuri, mzuri mno na ndiyo tegemeo langu.
Mhe: Kigwangala, ulikosea kijana huyo ulitakiwa kumpeleka jela. Ange-reform na kuwa chombo chenye kufaa. Kwa kumwacha ataendeleza ujinga wake. Polisi, mahakama, na gereza, vipo kwa ajili ya watu kama hao, ukimwacha atakufa ktk dhambi zake na akifa anakwenda Jehanamu. Damu yake mwenyezi Mungu ataitaka mikononi mwako mhe. Kigwangala.
Over.