Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?

Hitler aliteketeza roho za watu achana na suala la Uyahudi kwanza. Kwanini hawa jamaa hawatafunwi na laana badala yake wanazidi kuneemeka?...
Kama hoja yako haitokani na porojo za ukiifanyia ubaya Israel unalaaniwa, suala lako la kwamba kuua roho za watu kunaleta laana umelitoa wapi?!

Kama hoja yako haitokani na porojo za Israel ni Taifa Teule, kwanini hukumtaja Stalin ambae anaaminika kuwa ndie ameua rohho nyingi zaidi pengine kuliko hata huyo Hitler?! Kwanini isiwe Wajapan ambao na wenyewe waliua mamilioni ya roho?! Kwanini wasiwe Wachina, hususani kipindi cha Mao ambao waliua mamilioni ya Wachina wenzao?
 
Pili, kwamba wayahudi ni binadanu bora zaidi au mungu aliwapendelea hiyo ni kulingana na nyakati za kipindi hicho na namna jinsi mungu alivyokuwa anashughulika na matatizo ya binadamu more (direct) kuliko sasa hivi.
Mkuu, ni wapi nimezungumzia kuwa Wayahudi ni bora zaidi ya wanadamu wengine?...
 
Mkuu, ni wapi nimezungumzia kuwa Wayahudi ni bora zaidi ya wanadamu wengine?...
Mkuu umetoa hoja kwa kutumia wayahudi na mimi nimejibu hoja kutumia wayahudi kama mfano.( sababu tayari kuna utaratibu wa kuwachukulia wayahudi kama wateule wa mungu nadhani ndio sababu hata wewe ukaja nahoja kama hii ukiwatumia wayahudi kama mfano)
 
Majority ya wazungu Ulaya hawaamini ktk dini. Hivyo hizo dhana za taifa teule na stori za laana kwa atakayeliadhibu hilo taifa hawazizingatii...tuendelee kuamini hivyo sisi waafrika.

Hujatenda haki kutumia data za GDP ulizoziweka za nchi mbalimbali ktk kujenga hoja ya nguvu kati ya nchi mbali mbali ulizoelezea. Hii ni kwa kuwa umelinganisha GDP za nchi zenye watu lukuki (mfano Germany ina watu zaidi ya 83 milioni) na nchi nyingine ambazo zina watu kiduchu (mfano Norway ina watu takriban 5 milioni) . GDP per capita ndiyo itaakisi zaidi uchumi wa nchi hizo na kuzi-rank nchi hizo pasi na uonevu wowote. Kwa Data hizi, Germany ni ya 12.
 
Majority ya wazungu Ulaya hawaamini ktk dini. Hivyo hizo dhana za taifa teule na stori za laana kwa atakayeliadhibu hilo taifa hawazizingatii...tuendelee kuamini hivyo sisi waafrika.
Mkuu, siwazungumzii Wayahudi kama taifa teule la Mungu bali ninazungumzia roho za binadamu wa asili ya Uyahudi. I am taking humanity and not ethnicity...
 
Mkuu umetoa hoja kwa kutumia wayahudi na mimi nimejibu hoja kutumia wayahudi
Mkuu, suala ni humanity na sio ethnicity. Hata kama wangekuwa ni wajaluo, wahaya ama wamakonde waliuawa na Hitler huko Ulaya, bado ningehoji juu ya suala la Ujerumani kutokutafunwa na hii inayoitwa laana ya asili...
 
Hii ni kwa kuwa umelinganisha GDP za nchi zenye watu lukuki (mfano Germany ina watu zaidi ya 83 milioni) na nchi nyingine ambazo zina watu kiduchu (mfano Norway ina watu takriban 5 milioni) .
Mkuu, hiyo Norway ina ushawishi gani katika siasa za Ulaya na Dunia? Norway iliwahi kutawala nchi ngapi hapa duniani ukilinganisha na Ujerumani?...
 
Kuna baadhi ya watu na nchi nyingine duniani humu wanasema holocaust is a hoax. Kwamba hakuna Wayahudi milioni 6 waliouliwa. Hizo figure ni siasa zenye makusudio maalum na dunia inaaminishwa hivyo kwa sababu za kifisadi
 
Achana na hizo mambo mkuu....Hakuna kitu inaitwa Karma...bt survival of the fittest do exist...ndo mana unajiuliza hayo maswali.
 
Hitler aliteketeza roho za watu achana na suala la Uyahudi kwanza. Kwanini hawa jamaa hawatafunwi na laana badala yake wanazidi kuneemeka?...
Huchukua muda kidogo kwa mfano dola ya kirumi ilikuwa ndio yenye nguvu ikitawala dunia lakini baada ya askari wake wa kirumi kumuua Yesu dola ya kirumi ilisambaratika na sasa Italia ni kiinchi kidogi tu cha hovyo

Pili kuna mjerumani mtu wa Mungu Martini Luther aliyeanzisha imani ya kiprotestanti duniani kazi yake yaweza kuwa sababu ya ujerumani kutopigwa na laana hadi sasa
Ulutheri imo pote duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…