Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?

Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?

Rais Magufuli ni mbeba maono Kwa jinsi uchumi wa Tanzania unavyokuwa kwa kasi hadi 2025 tutakuwa tumeipiku south Africa.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

Ujerumani iliwahi kuwaua binadamu zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya (European Powerhouse)

Kwanini wao hawajatafunwa na laana hii ya asili kutoka kwa babu zao?

Je, hii dhana ya laana ya asili (Ancestral/Generational Curse) ipo sahihi kweli?

Kama ipo sahihi, kwanini iwepo Afrika tu na sio Ulaya?


Laana ya Asili kama inavyofafanulia na Mtumishi Joel Osteen (American Preacher & Televangelist)
=============
Laana ya vizazi inaaminika kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa sababu ya uasi dhidi ya Mungu. Ikiwa ukoo wako umepewa laana ya talaka, uchumba, umaskini, hasira au mifumo mingine isiyo ya kimungu, unaweza kuwa chini ya laana ya ukoo.

Familia zetu zina ushawishi mkubwa juu ya maendeleo yetu, pamoja na ukuzaji wa mifumo yetu ya dhambi. Watu wengine wanadai kwamba laana za kifamilia au kizazi hupitishwa kwa njia ya kizazi.

Imani hii inatokana na vifungu vya Agano la Kale ambavyo vinasema kwamba Mungu "huwaadhibu watoto na watoto wao kwa dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne" (Kutoka 34: 7).

Ikiwa familia zinarithi laana za kiroho au la, ni dhahiri kwamba mifumo ya dhambi hupitishwa kupitia familia. Kila mtu hutenda dhambi; lakini kama vile utamaduni, kabila, na jinsia zinavyoongoza mwelekeo wetu wa dhambi katika mwelekeo fulani, ndivyo pia familia zetu.

Tunarithi tabia nyingi na mapenzi ya kitu fulani kutoka kwa wazazi wetu ambao sio ushawishi mzuri kwetu au kwa wengine. Tunapopata tabia ya imani au imani ambayo inaathiri vibaya maisha yetu au wale wanaotuzunguka, hii inajulikana kama laana ya kizazi. Ni upande uliojificha wa tabia uliopitishwa kupitia vizazi.

KIINGEREZA KIDOGO: Many Africans, Christian or not, live in fear of generational curses. When misfortunes hit, they want to know who might have bewitched them.

Non-Christians may turn to the witchdoctor while believers seek a deliverance minister to diagnose their problem and prescribe necessary spiritual steps forward. But why is this so?

HISTORIA NDOGO YA MAUAJI YA WAYAHUDI BARANI ULAYA (HOLOCAUST)
==========
Holocaust, yalikuwa ni mauaji ya halaiki ya Vita vya pili vya dunia kwa Wayahudi wa Ulaya. Kati ya mwaka 1941 na mwaka 1945, Ulaya nzima ambayo ilikuwa inakaliwa na Wajerumani, Ujerumani ya wa Nazi na washirika wake waliwaua Wayahudi wapatao milioni sita, karibu theluthi mbili ya idadi ya Wayahudi wote wa ulaya kwa wakati ule.

Mauaji hayo yalifanywa kwa watu wengi kwa njia za upigaji wa risasi kwa halaiki ya watu;sera ya mauaji ya kutokomeza watu kupitia kazi katika kambi za mateso; na katika vyumba vya gesi na gari za gesi katika kambi za kuangamiza za Wajerumani, haswa Auschwitz, Belzec, Chelmno, Majdanek, Sobibór, na Treblinka katika Poland iliyokaliwa na Wajerumani.

UCHUMI WA UJERUMANI KWA UFUPI
=============
Pamoja na Pato la Taifa la zaidi ya Euro trilioni 3.4, uchumi wa Ujerumani ulikuwa mkubwa zaidi barani Ulaya mnamo mwaka 2019. Chumi zenye ukubwa sawa za Uingereza na Ufaransa zilikuwa chumi za pili na wa tatu kwa ukubwa barani Ulaya wakati wa mwaka jana, ikifuatiwa na Italia na Uhispania.

Uchumi mdogo kabisa katika takwimu hii ni ule wa taifa dogo la Balkan la Montenegro, ambalo lilikuwa na Pato la Taifa la Euro bilioni 4.66 tu, karibu mara 74 ndogo kuliko uchumi wa Ujerumani.

Uchumi wa Ujerumani umekuwa ndio uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya tangu mmwaka 1980, hata kabla ya kuungana tena kwa Ujerumani Magharibi na Mashariki. Uingereza, kwa kulinganisha, imekuwa na bahati wakati huo huo na ilikuwa na uchumi mdogo kuliko Italia mwishoni mwa miaka ya 1980.

Uingereza pia ilipata mapigo makubwa zaidi ya chumi zingine kubwa wakati wa anguko la uchumi wa mwishoni mwa miaka ya 2000, ikimaanisha uchumi wa Ufaransa ulikuwa wa pili kwa ukubwa barani kwa muda baadaye. Uchumi wa Uhispania ulikuwa wa tano kwa ukubwa Ulaya katika kipindi hiki cha miaka 38, na kutoka 2004 kuendelea umekuwa na thamani ya zaidi ya Euro trilioni moja.

Tazama takwimu kutoka chanzo sahihi hapo chini.

View attachment 1559175

Kwanini Ujerumani haijawahi kutafunwa na laana hii ya asili ya babu zao licha ya kuwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6 badala yake inazidi kuneemeka kiuchumi?

Mpaka Engineers bora wapo kwao>>> Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Je, dhana hii ya laana ya asili ipo sahihi kweli?

ANGALIZO: Hii mada haizungumzii Wayahudi kama taifa teule la Mungu bali inazungumzia roho za binadamu wa asili ya Uyahudi. It's all about humanity and not ethnicity.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Asante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati, Mungu akupe afya uendelee kututumikia.
 
Sikubaliani maana kabla ya vita vya pili vya dunia walikuwa milioni 12,vita imeisha wako milioni 15,
Hizi story ni sawa na story za joshua kusinamisha jua na kuua maadui 500,000 kutwa,,,hata bomu la atomic halikuweza kuua watu wote hao,leo eti mishale na mapanga iweze
😂 😂 😂 hizi dini hizi daah !!!
 
Hii mambo ya kiimani zaidi

Binafsi Mimi siamini hio dhana ya laana asili yani uovu wa babu yangu laana inipate hadi mimi kisa mtiririko wa damu aaahh, hilo swala halikubaliani na akili yangu....

Pia kwa upande wa imani yangu ya dini (uislamu) hilo jambo halikubaliani nalo , kwenye Quran tumeambiwa kila nafsi italipwa kwa aliyoyachuma mwenyewe mazuri au mabaya na ikasema baba hana jukumu kwenye dhambi za mtoto pia mtoto nae hivyo hivyo

2:281

"Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa."

Lakini kuna kitu kinafahamika kana dhima mtiririko wa dhambi kwa kosa la mtu mwengine , lkn dhambi hiyo unaipata ukiwa umeshiriki kwenye uovu huo mfano sehemu za kufanyia zinaa zinajebgwa nawe ukashiriki kujenga basi dhambi zitazo chumwa pale nawe zitakuhusu kwasababu ya mchango wako hta ukiwa umekufa bado dhambi zako zitazid kumiminika
 
absolutely Africa ndio nchi ya maziwa na asali naamini siku wa Africa tukiamka na kuungana (japo ni kitu wazungu wanapigania kisifanikiwe) tutaishi kwa amani sana sanaa sanaa hutosikia watu wanauana kisa madini kama Congo leo mtu mweusi anapewa hela kulinda migodi ya mabeberu wanayo chimba na kuchukua madini kibabe kweli?

Leo unasoma biblia unaambiwa hakuna taifa lililo teseka zaidi ya wana wa Israel

kwa akili zetu na historia tulizosoma mpaka leo nani ameteseka kama mtu mweusi nani ameuliwa kama mtu wa Africa sasa leo zinakuja propaganda eti wao ndio taifa teule na ndio la wapi tangu lini?

Tuseme tuu ukweli marekani ni kibaraka wa uingereza kwa siri au hata kujulikana na marekani wanashirikiana na kibaraka wao swahiba kabisa Israel ili kueneza propaganda

Israel wana uwezo wa kueneza kila propaganda kwasababu wameweza kuteka soko la media dukani wenye asili ya huko ndio wamiliki wa kubwa wa hisa za vyombo vikubwa duniani

leo watu wana enda Israel nchi ya ahadi wakati kama africa ndio asili na binadamu wa kale walikaa hapa
Okay...
 
Leo kivipi historia ya miaka elfu mbili iliyo pita uaminishwe majengo na magofu yapo israel wakati Ethiopia,sudan na misri wana vitu halisi kabisa kama vilivyo elezwa kwenye hivi vitabu vya imani

Africa tuamke

2020 APOCALYPSE YEAR
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom