Mtaalam
Folk Part II , nakusalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nina ndoto nyingi sana nilizoota
1. Niliota nipo maeneo ya soko la samaki la Ferry kona ya kwenda Ikulu nimesimama na mwenzangu akapita Mheshimiwa Jakaya Kikwete raisi mstaafu anaendesha gari Escudo nyekundu akatuita huku anatabasamu Vijana twendeni tukapanda gari tukaondoka. Hii ina maana gani ?
2. Niliota ndoto nyingine kumhusu Msichana fulani ambaye tunatoka Wilaya moja na wote ni kabila moja na tumefanana kwa vitu vingi sana, ikiwemo Siku ya kuzaliwa japo nimempita karibia miaka mitano na miezi mitano na siku kama 9 hivi. Ananipa Sufuria ndogo nyeupe mpya kabisa huku akipiga goti na anatabasamu hii ina maana gani ?. Hizi ndoto kumhusu huyu binti nimeota zaidi ya ndoto saba ambazo ni kama series kabisa
🙂🙂
3. Ndoto nyingine niliota tupo kwenye mazoezi kama ya wale Vijana wa JKT tumesurubika sana, tukawa tumekaa chini tukiwa tumechafuka sana na tumenyoa vipara yaani ni kama mazoezi ya Kijeshi. Sasa akatokea Dada ambaye ni kama Secretary wa Boss akaanza kusema " Mwenye nidhamu na aliyefaulu mafunzo yetu ni ( .....................) Akamtaja jamaa mmoja ambaye ni mshikaji wangu tulisoma wote Shule ya Msingi na Secondary lakini tukaja kutengana baada ya Mimi kuhama ile Shule, Sasa yule Secretary wa Boss alivyomtaja yule Jamaa akatokea Boss akasema hakuna wewe kaa chini , njoo MANYANZA, sasa wakati nainuka nataka kwenda kwa boss huku nakimbia yule jamaa akanishika Tshirt ili nianguke lakini nilimpiga ngumi nzito na akaniachia huku akivuja damu puani na mdomoni, nilivyoinuka nikawa namkimbilia Boss nilipofika kwa Boss akaninyanyua juu huku akinipongeza. Na huyu jamaa ambaye niliyempiga ngumi kafariki mwaka huu kwa ajali ya gari hapa hapa Dar es Salaam na nilikuwa naenda sana kumtembelea na kumsafisha wakati mwingine. Je hii ndoto ina maana gani ?
4. Nimeandika ndoto ya kwanza kumhusu huyo Binti, Kuna siku nilimuota Mama yake Mzazi, wapo kwenye Kibasi kidogo hiace mbuga za Wanyama yeye na Wakina Mama wengine, Kile Ki Hiace kikaharibika ghafla na wale wakina wote wakamkimbia na Yeye akawa anahuzunika na akaonekana kama ana umwa ugonjwa wa tumbo na Mimi nilikuwa juu ya mti nikashuka nikaenda kumpa pole huku nimemshika begani akaanza kutabasamu na furaha ikamrudia tena. Je hii ndoto nayo ina maana gani ?
Zipo ndoto nyingi sana nisaidie maana ya hizo ndoto. Kiimani na Kiuhalisia wa maisha yetu Sisi Binadamu